Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Woga wa Mtoto Kuachwa Peke Yake

Je, watoto wote wanapitia woga wa kuachwa?

Ndio, kwa kiasi fulani. Woga wa kuachwa ni hatua ya kawaida ya ukuaji wa kihisia kwa mtoto na inaanza watoto wanapoelewa vitu na watu vinapaswa kudumu katika maisha yao.

Katika baadhi ya hatua, watoto wengi wataonyesha woga /wasiwasi na kukasirika wanapotenganishwa na mzazi. Ni hali ya kawaida kwa mtoto asiyeweza kujitetea anapotengwa na mtu anayemlinda na kumjali kulia kwasababu ya woga.

Inatokea zaidi lini?

Watoto wanaanza kuonyesha dalili za uoga wa kuachwa mapema sana mwezi wa 6 au 7, ila kwa watoto wengi hali hii inakomaa kati ya miezi 10 mpaka 18 na kupungua miaka miwili.

Kawaida, uoga wa kuachwa unatokea pale unapoenda kazini. Mtoto anaweza kupata woga pia wakati wa usiku unapompeleka kitandani kulala, mara nyingi hali hii inapungua mtoto anapofika miaka miwili.

 

Jinsi gani naweza msaidia mwanangu?

Kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kumsaidia mtoto wako katika hali hii ya uoga wa kuachwa:

Andaa mazingira na mwanao kuzoea watu wengine: wakati wa kurudi kazini ukiwadia,itabidi umuache mtoto nyumbani. Ukirudi kazini jaribu kumuacha na watu ambao tayari anawafahamu kama bibi au babu yake, mdogo wako au dada wako wa kazi. Anaweza kupinga awali lakini atazoe pale anapozungukwa na watu anaowajua.

Andaa utaratibu: Amua utaratibu mzuri mfupi utakaoufuata kila wakati unapomuaga mwanao. Utaratibu unaojulikana kwa mwanao unasaidia kujenga uaminifu kutoka kwa mwanao na uwezo wake wakabiliana na woga wake.

 

Nimwandaaje mwanangu?

Fanya majaribio nyumbani: kabla ya kumuachia mtu mwanao, hakikisha umeshajaribu nyumbani ukiwa nae ili kujenga uaminifu kwa mtoto na kujifunza kila kitu kitakua sawa ukiondoka hata dakika moja au mbili, na utarudi. Kwa dhana hiyo mwanao atakua tayari kuachwa kwa mtu mwingine anayemfahamu. Akitambaa kuelekea chumba kingine kilicho salama muache aende na mpe muda kabla hujamfuata.

 

Siku zote muage mwanao vizuri:  mkumbatie na mpige busu kabla ya kuondoka. Mwambie unapoenda na utarudi saa ngapi, lakini kumbuka kumuaga mwanao kwa muda mfupi tu,na usirudi baada ya kumuaga. Usirudi, wala kukasirishwa pale unaomsikia mwanao analia baada ya kufunga mlango.

Mara unapoondoka, ondoka:  kurudi kumuangalia mtoto kutafanya hali iwe ngumu kwako, mwanao na msaidizi au mtu unayemuachia mtoto.

Kumbuka kumjaribu mwanao kwanza kabla ya kuanza kumkabidhi siku nzima mwanao kwa ndugu au msaidizi wako,unaweza kujaribu kumuacha saa moja na sio zaidi.

Woga wa kuachwa wakati wa usiku

Jitahidi kufanya masaa machache kabla ya kuenda kitandani yenye furaha na amani kwa mtoto, kwa njia hii itamsaidia mtoto kupata usingizi anaotakiwa bila kushtuka katikati ya usiku.

Mkumbatie, msome hadithi na kumuimbia nyimbo nzuri pamoja kabla ya kulala.

Ni sawa kumuendea mwanao pale anapolia mara baada ya kumuweka kitandani- itakusaidia wewe na mwanao wote kujua yuko salama. Hakikisha unafanya muda huo mfupi na usiomuhamasisha kuendelea kukusikiliza ili alale mara moja.

Ikiwa hakuna hata kimoja kimefanya kazi kumsaidia mwanao jaribu kutathimini njia unazotumia kumsaidia mwanao na wewe kukabiliana na woga wa kuacchwa. Hakikisha kuangalia mara ya pili mtu unayemuachia mwanao au sehemu (daycare) wakati mwingine mtu na sehemu unaomuacha mwanao vinaweza visiwe sahihi kwa mwanao.

Rudia mkakati wako wa kumuaga mwanao- fanya maagano yawe mafupi na usirudi kumuangalia anapoanza kulia mara unapoondoka.

Utaratibu wa Muda wa Kulala Mtoto

Vitu vya msingi vitakavyosaidia kupata utaratibu mzuri wa kulala

Kitu cha muhimu ni wewe kurudia utaratibu huohuo kila usiku ili mwanao aweze kukubaliana nao na kujifunza. Ikiwa haupo nyumbani jaribu kufuata utaratibu huo kama inawezekana,itamsaidia mtoto kutulia katika mazingira yake mapya.

Utaratibu huu ujumuishe kukaa nae chumbani kwake zaidi, hii itamfundisha kuwa chumbani kwake ni sehemu nzuri.

Mara unapomuweka mtoto kitandani na kumfunika kumbuka kumbusu na kumtakia usiku mwema. Ikiwa atalia wakati unaondoka, mkumbushe utarudi baada ya dakika tano kumuangalia, baada ya dakika hizo kama hajalala rudia tena  na ondoka dakika tano tena.

Ni nini nijumuishe katika utaratibu wa kulala kwa mtoto wangu?

Hakikisha unamchagulia mwanao michezo na shughuli zitakazomsaidia mwanao kuwa katika hali ya utulivu zaidi ya kumsisimua. Zifuatazo ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya:

Muogeshe

Maji ya moto wakati wa kuoga yatakusaidia kumfanya mwanao awe mkavu na msafi, hii ni njia rahisi ya mwanao kulala. Sio watoto wote wanapenda kuoga, wengine wanasisimuka zaidi wanapooga,ni vizuri kumnawisha miguu na uso na kumuogesha asubuhi.

Mpige mswaki

Utaratibu wa mwanao ujumuishe kupiga mswaki. Ni muhimu kuanza tabia ya kupiga mswaki mapema ili ajifunze kuyaangalia meno yake vizuri kadiri anavyokua.

Mbadilishe nguo kabla ya kulala

Mbadilishe mwanao, nepi mpya au mkumbushe kwenda chooni(kama anaweza). Kisha msaidie kubadilisha na kuvaa nguo za kulala.

Cheza mchezo wenye utulivu naye

Tumia muda wako kucheza nae mchezo kama kadi au kutegua kitendawili (puzzle) kabla ya kulala. Watoto wakubwa wanapenda kucheza kadi au kutegua kitendawili,lakini wadogo wanapenda mcheko wa kujificha. Hakikisha mchezo usiwe mkubwa na kumsisimua mtoto sana.

 

Ongea nae

Iwapo mwanao anaongea au hajaanza kuongea, wakati wa kulala ni muda mzuri wa kuongea nae. Kama mwanao bado mdogo wewe utahusika kwenye kuongea zaidi, lakini bado atapenda kukusikiliza.

Ongea nae kuhusu chochote mlichofanya siku nzima yote, na amejisikiaje. Kama mwanao ni mkubwa muulize jambo zuri na baya lililomtokea siku hiyo, na pia mkumbushe asiwe na wasiwasi wowote. Hii itamsaidia kukabiliana na woga au hofu na badala yake atapata usingizi mzuri.

Msimulie hadithi

Hadithi zitamsaidia mtoto kukuza misamiati na kuongeza upendo wake katika kusoma na kusimulia hadithi. Kama unamsomea mwanao hadithi chagua vitabu vya watoto anavyopenda kila usiku. Anaweza kupenda hadithi moja na kurudia kila siku, usikasirishwe na kitendo hichi ni muhimu katika ukuaji wake.

Muimbie wimbo

Nyimbo nzuri za watoto wakati wa kulala ni njia nzuri ya kumfanya mwanao apotelee usingizini vizuri. Sauti yako nay a mwenzi wako ni moja ya sauti anazozipenda mwanao. Iliwezekana rekodi sauti yako ukiimba na kisha muweke asikilize ikiwa mtu mwinine atamuandaa kulala siku nyingine.

Ugonjwa wa Tetekuwanga kwa Watoto

Ugonjwa wa Tetekuwanga ni nini?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kirusi kinachoitwa “varicella-zoster”, watoto wengi wanapata tetekuwanga wakiwa wadogo na inakua ugonjwa mdogo.

Mara baada ya mtoto kushika kirusi, dalili zinaweza kuchukua wiki moja na wiki tatu kuonekana.

Dalili za ugonjwa wa tetekuwanga

Dalili inayoonekana zaidi ni upele. Inaanza kama kidoti kidogo chekundu na kukua kufanyika lengelenge ndani ya masaa machache. Utaanza kuona kwanza usoni kwa mtoto wako. Viupele vitaanza kuenea kifuani na tumboni, alafu sehemu nyingine za mwili.

Alama na malengelenge yanaweza kuonekana sehemu nyingine, na zitaweza kumsumbua mwanao zaidi kama yametokea maeneo ya mdomoni na shingoni na kuzunguka sehemu zake za siri.

Mtoto anaweza kusikia kuchoka na kuumwa, na anaweza pia kuwa na:

  • homa
  • kuumwa na kupata maumivu
  • kukosa hamu ya kula.

Jinsi gani ugonjwa wa tetekuwanga unatibiwa?

Unaweza kumtibu mwanao tetekuwanga nyumbani, unaweza kutibiwa au kuzuiliwa na antibaiotiki ili vipele visipate maambukizi, ila kiuhalisia ugonjwa wa tetekuwanga hupotea wenyewe baada ya wiki.

Zifuatazo ni njia zinazoweza kumsaidia mtoto mwenye tetekuwanga:

  • Mpatie maji ya kutosha ili asipate upungufu wa maji mwilini.
  • Muogeshe na maji ya uvuguvugu. Jaribu kuongeza magadi soda, hakuna ushahidi kwamba magadi yanasaidia kupunguza muwasho ili wamama wengi wanatumia njia hii sana na inasaidia. Hakikisha unamkausha vizuri baada ya kuoga.
  • Hakikisha kucha za mwanao ni fupi, ili kuepusha mtoto kujikuna na kupata makovu baadae.
  • Mvalishe mwanao nguo za pamba zisizombana kusaidia ngozi yake kutulia na kupunguza muwasho.

Unaweza kumpa mtoto paracetamol ili kupunguza joto la mwili na kupunguza maumivu na kuumwa. Unaweza mpatia mtoto piriton kama ana umri zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuongea na mshauri wa afya.

Ni vizuri mtoto wako kubaki nyumbani mpaka tetekuwanga zitakapo kauka ili kuwalinda wengine wasipate kwasababu inaenea kwa haraka zaidi.

Ikiwa hjawahi kupata tetekuwanga kabla, unaweza kupata sasa kutoka kwa mwanao. Muone daktari kama unahisi una tetekuwanga maana ni ugonjwa mkubwa sana kwa watu wazima. Hii ni muhimu sana kama una ujauzito, au unahisi una ujauzito.

Tetekuwanga inaweza kuwa hatari kwa mtoto ambaye hajazaliwa. Kama ulishapata tetekuwanga mwanzoni, kuna nafasi ndogo sana ya kupata tena.

Ugonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo kwa Watoto

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni nini?

Ugonjwa wa uti wa mgongo ni ugonjwa unaotokea iwapo utando unaofunika uti wa mgongo na ubongo umepatwa na maambukizi na kuvimba. Ugonjwa huu unakua kwa haraka na ni hatari sana.

Ugonjwa wa uti wa mgongo unasababishwa na bakteria au virusi:

  • Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria: Hii ni aina ya maambukizi iliyo hatari sana. Inaweza kuhatarisha maisha na kusababisha ulemavu kama ukiziwi au uharibifu wa ubongo. Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria ambao haujatibiwa unasababisha kuenea maambukizi haraka ndani ya damu (septicaemia), ambayo ni hatari sana.
  • Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na virusi una madhara madogo ukilinganisha na ule unaosababishwa na bakteria. Ingawa dalili kama mafua yanaweza kumsumbua mtoto lakini ana uwezo wa kupona bila matibabu ndani ya siku saba mpaka 10.

Jinsi homa ya uti wa mgongo inavyoenezwa?

Bakteria na virusi vinavyosababisha ugonjwa huu vinaishi ndani ya pua,koo na utumbo wa watu. Vyenyewe haviwezi kusababisha athari. Ugonjwa wa uti wa mgongo unakua pale virusi na bakteria vinaposhambulia na kuambukiza utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo.

Ni nadra sana kwa mtu aliye na ugonjwa huu kuambukiza. Ingawa watu wanaoishi nyumba moja na mtu mwenye ugonjwa huu uliosababishwa na bakteria wanapatiwa antibaiotiki kama tahadhari.

Mtoto wako anaweza kupata bakteria na virusi kwa:

  • Kuguswa au kupigwa busu.
  • Watu kupiga chafya na kukohoa karibu yake.
  • Kuchangia vyakula vya kula na kunywa na vitu vingine binafsi kama msawaki.

Unaweza kumlinda mwanao kwa kufuata usafi mzuri. Safisha mikono baada ya kukohoa, kupiga chafya au kupenga kamasi, au baada ya kutoka chooni au kubadilisha nepi.

Dalili na ishara za ugonjwa wa uti wa mgongo

Dalili za awali za ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria, ambao ni hatari sana ni ngumu kuonekana. Dalili zinaweza kuonekana kama za mafua au kuumwa tumbo ambazo ni kama kuwa na homa. Lakini dalili za ugonjwa huu zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine na zinaweza kuonekana katika utaratibu tofauti

Ukiona dalili zifuatazo mkimbize mtoto hositali haraka:

  • Mtoto ameota upele usiopotea, upele unaoanza kama vipele vidogo vyekundu vinavyokua kwa namba na ukubwa na kubadilika kuwa zambarau-nyeusi.
  • Mtoto kukakama na kushindwa kutulia,asiye na furaha.
  • Analia kwa sauti isiyo kawaida.
  • Ana baridi miguuni na mikononi.
  • Anatapika na kukataa kula.
  • Shingo na mwili kukakama.
  • Hapendi mwanga mkali.
  • Kuhema kwake kumebadilika,wakati mwingine haraka au taratibu kuliko kawaida.
  • Mgongo kuuma.
  • Tumbo kuvimba.
  • Mshtuko wa moyo.

Jinsi ugonjwa wa uti wa mgongo unavyotambuliwa?

Hospitalini daktari wa watoto atamkadiria mwanao haraka, akiangalia dalili na ishara za ugonjwa. Daktari atahitaji kuchukua sampluli ya damu ya mwanao au kimiminika kutoka kwenye uti wa mgongo kuangalia kama ana ugonjwa huu uliosababishwa na bakteria au virusi.

Daktari atachukua sampluli ya utando wa uti wa mgongo kwa kumchoma mtoto sindano nyembamba katika sehemu ya chini ya uti wa mgongo na kutoa kimiminika kutoka kwenye tishu zinazozunguka uti wa mgongo. Kimiminika hicho kinatumwa maabara kupimwa.

Inaweza kuchukua dakika 45 kwa daktari kuchukua kimiminika hicho kwenye uti wa mgongo wa mwanao. Inaweza kuhuzunisha kumuona mwanao akipitia utaratibu huo mkubwa wa kimatibabu. Ukiona unashindwa kuangalia toka nje kidogo atabaki katika mikono salama usiwe na wasiwasi.

Ikiwa daktari atahisi mwanao ana maambukizi yaliyosababishwa na bakteria atakupatia antibaiotiki za mwanao mapema bila kusubiria matokeo ya vipimo. Daktari anaweza kuomba mwanao afanyiwe kipimo cha “CT” kama kinapatikana hositalini kinachopiga picha za muonekano wa ndani wa ubongo kuangalia kama kama kuna uvimbe ndani ya ubongo.

Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo

Matibabu ya ugonjwa huu yanategemea na aina gani ya ugonjwa wa uti wa mgongo alionao mtoto:

Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria
Aina hii inahitaji matibabu ya haraka ya antibaiotiki ndani ya hospitali. Kama mtoto anaumwa sana, anaweza kuwekwa katika wodi za wagonjwa mautiuti.

Matibabu ya mwanao yanategemea na kiasi gani mwanao anaumwa na dalili gani anazo. Matibabu ya aina hii ya ugonjwa wa uti wa mgongo yanajumuisha:

  • Antibaiotiki zinazotolewa kwa njia ya drip katika mishipa ya mwanao kuhakikisha ana dozi ya mara kwa mara.
  • Vimiminika vitakvyomsaidia mtoto kuwa na maji ya kutosha mwilini
  • Hewa ya oksijeni
  • Matibabu ya “steroid” yanayosaidia kupunguza uvimbe kuzunguka ubongo.

Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na virusi

Maambukizi yanayosababishwa na virusi hayaitaji antibaiotiki, hivyo mwanao atahitaji kupumzika na kuangaliwa zaidi. Mtoto anaweza kuumwa kichwa, ananung’unika bila kuacha na kuchoka, na anakataa kula. Atapona ndani ya siku 10,kwa sasa hakikisha:

  • Anakunywa  maji mara kwa mara
  • Unampatia “paracetamol” za watoto kupunguza maumivu ya kichwa.
  • Hakikisha mazingira yanayomzunguka ni tulivu.

Watoto wachanga wanaweza kupata ugonjwa huu?

Ndio. Watoto waliozaliwa kabla ya wiki 37 wana uzito duni, wana hatari za kupata ugonjwa wa uti wa mgongo papo kwa hapo.

Ikiwa mama alikua na ugonjwa wa listeria akiwa na ujauzito na akampatia mtoto kupitia plasenta, inaongeza hatari za mtoto kuzaliwa na ugonjwa huu papo kwa hapo au kuupata baada ya kuzaliwa.

Tatizo la Mtoto Kukosa Choo

Nitajuaje mwanangu wa mwaka mmoja mpaka mitano anakosa choo?

Katika suala la kujisaidia haja kubwa hakuna kinyesi cha kawaida au ratiba ya wakati wa kujisaidia. Cha muhimu ni kipi cha kawaida kwa mwanao. Anaweza akajisaidia kila baada ya kula au baada ya siku moja au zaidi. Watoto wa miaka minne wanajisaidia mara tatu kwa siku na mara tatu kwa wiki.

Kwa kuangalia kinyesi cha mwanao, itakusaidia kujua kama mwanao anapata shida ya choo. Ishara hizo ni kama zifuatazo.

  • Kinyesi kikubwa na kigumu kinachompatia shida wakati wa kujisaidia.
  • Kinyesi kidogo na kigumu kinachofanana na mavi ya mbuzi

Tabia ya mwanao itabadilika na kukujulisha pia. Watoto wenye shida ya choo wana:

  • Jisaidia haja kubwa mara chache zaidi
  • Onyesha ishara za kubana kinyesi, wakati mwingine kusimama na vidole vya mguu.
  • Lalamika tumbo kuuma au kuvimbiwa.
  • Sumbua sana.
  • Poteza hamu ya kula.

Kwanini mtoto wangu anakosa choo?

Ni hali ya kawaida watoto kukosa choo wanapoanza kujifunza kujisaidia wenyewe au wanapoanza shule.

Sababu za kukosa choo kwa watoto ni pamoja na;

  • Kukosa maji na vyakula vya nyuzinyuzi vya kutosha (fibre).
  • Inahusiana na maswala ya kujifunza kujisaidia
  • Msongo wa mawazo au wasiwasi.

Jinsi ya kutibu hali hii.

Onana na daktari mapema kama una wasiwasi mwanao anakosa choo. Kabla ya kumuona daktari unaweza jaribu mambo kadhaa ili kutuliza hali hii:

  • Ongeza ulaji wa matunda na mbogamboga kwa mtoto wako, bila kusahau vyakula ambavyo ni vyanzo vizuri vya nyuzinyuzi (fibre) kama matunda, mboga za majani, maharage na nafaka nzima. Matunda kama tofaa (apple),zabibu, peasi na strawberi.
  • Mhamasishe kunywa maji mengi anagalau glasi sita kwa siku. Inaweza kuwa maji, maziwa au juisi,ili kufanya kinyesi cha mtoto kuwa laini.
  • Mazoezi ya viungo kama kutembea, kupanda na kukimbia kila siku yanasaidia.
  • “Massage” tumbo la mwanao
  • Usimharakishe mtoto kujifunza kujisaidia mwenyewe kama hayuko tayari. Kumlazimisha inaweza kumfanya aogope au awe na wasiwasi unaopelekea mtoto kubana haja kubwa.
  • Watoto wanaokosa choo, mara nyingi hawajui wakati gani wa kujisaidia. Msaidie mwanao kwa kumuhimiza kukaa chooni dakika 10 baada ya kula, au kabla ya kwenda kulala. Utulivu wa mtoto wakati wa kujisaidia unamsaidia mtoto kujisaidia vizuri,hakikisha unamuwekea midoli na michezo karibu na poti lake wakati akijaribu kujisaidia.
  • Zawadi baada ya kujisaidia ni motisha nzuri kwa mwanao ikiwa anabana haja kwasababu ya woga.
  • Ikiwa mwanao anaenda shule hakikisha unajua kama anajisaidia shuleni vizuri. Watoto wengine ni wagumu kujisaida hasa wakiwa mbali na nyumbani.

Vidokezo hivi vinaweza kumsaidia mwanao, ni muhimu kumuona daktari wako pia. Itachukua mda mrefu mtoto kurudia hali ya kawaida kujisaidia akikosa choo kwa muda mrefu.

Wakati huu jaribu kutulia, kukosa choo kwa watoto inaweza kuwa hali ngumu kupambana nayo hasa mwanao anapochafua nguo zake za ndani kila mara. Mpatie usikivu wako na hakikisha una nguo nyingi safi. Tiba sahihi itamsaidia mtoto kurudia hali yake ya awali.

Njia za Kumdhibiti Mtoto Katika Matumizi ya Simu na Luninga

Sio sahihi kumuhamasisha mwanao katika matumizi ya simu na kompyuta katika umri wake lakini luninga ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Hivyo zifuatazo ni njia saba za matumizi sahihi ya luninga na simu:

 

Usimshawishi mwanao katika matumizi ya simu, komputa na luninga ikiwa haonyeshi kuvutiwa navyo

Asichokifahamu mtoto hawezi kukihitaji, hivyo kama hajaonyesha kuvutiwa na simu na kompyuta hakuna sababu ya kumshawishi. Subiri hadi pale atakapoonyesha kutambua na kuvutiwa na vitu hivi kabla hujamtambulisha.

 

Kikomo cha matumizi ya simu, komputa na luninga

Weka kikomo katika mda wa kukaa katika luninga, simu au kompyuta, isiwe zaidi ya dakika 20. Mtoto wako anahitaji mda wa masaa 3 kuwa makini kwa siku ili aweze kukua vizuri. Unapotumia muda mwingi katika luninga mtoto wako atashindwa kuyajua mazingira yanayomzunguka kwa kutembea, kukimbia na kuruka.

 

Weka muda wa kutazama luninga kwa pamoja

Tazama luninga au simu na mwanao huku ukimuelezea na kucheza kwa pamoja. Hii inaweza kumsaidia kama vile ukiwa unasoma kitabu, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa misamiati na uwezo wake wa kutunza kumbukumbu. Pia atapata muda mzuri wa kufurahi na wazazi wake.

 

Chagua michezo sahihi kwa mtoto kwa kuzingatia umri wake

Zingatia michezo ambayo inamsaidia mtoto chini ya miaka mitatu. Michezo hiyo:

  • Iwe na uwiano sawa na umri wa mwanao.
  • Imfanye mwanao acheke
  • Impe mwanao malengo ya kufanikisha.
  • Iwasisitize wazazi kushiriki.

 

Zingatia zaidi michezo si kujifunza

Mtoto wako anatakiwa kuona luninga au simu kama moja kati ya midoli yake. Usijaribu kutumia simu na luninga kama sehemu ya kumfundisha mtoto wa mwaka mmoja kuhusu herufi na kuhesabu. Hakuna ushahidi kuwa michezo ya kompyuta au shughuli nyingine za mtandaoni zina manufaa ya kielimu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili.

Kinyume na hapo, nenda kwenye michezo na shughuli ambazo kiujumla zitamsaidia mtoto kujenga uwezo wa kujifunza kwa haraka. Inaweza kuhusisha kusikiliza wimbo mzuri na kuelewa chanzo na athari, kinyume cha vitu, rangi na utambuzi wa maumbo. Mtoto wako atakua na uwezo mzuri wa kujifunza ikiwa ni hadithi, wimbo au mchezo mzuri.

 

Chagua michezo yenye picha ambayo ni rahisi kuona

Usitarajie mtoto wako kuiga picha zaidi ya moja katika luninga au simu. Itakuwa vigumu mwanao kuelewa na kufurahia michezo au hadithi zinazoonyeshwa sehemu yeney watu wengi kama sinema.

 

Chagua michezo yenye nyimbo nyepesi

Tangu kuzaliwa watoto wanapenda sana nyimbo na sauti za mashairi na uimbaji wa nyimbo. Na hadi wanapokua na umri wa mwaka kurudiarudia nyimbo inawasaidia watoto kuelewa maneno. Pia wanaweza kuanza kujifunza kuhusu kifuatacho.

Kama mtoto wako amefikia umri wa miezi 18, cheza naye kwa kutengeneza sauti za mlio wa kengele na saa, mtoto wa umri huu anapendelea sana hivyo.

Ndoto za Hofu na Kutisha kwa Mtoto

Ndoto za hofu wakati wa usiku ni nini?

Ndoto za hofu wakati wa usiku zinatokea wakati wa kulala, mtoto anaamka na kukaa mara moja kitandani,na kuanza kulia,kunong’ona,kupiga kelele,kulalamika na kujitupatupa akiwa amefungua macho lakini bila kuamka usingizini vizuri. Kwasababu yupo katikati ya kuamka na usingizini anaweza asitambue uwepo wako na asiitikie chochote utakachomwambia. Hali hii inaweza kudumu mpaka dakika 40 na mwanao atarudi kulala na asiwe na kumbukumbu yeyote akiamka kesho asubuhi.

Tofauti kati ya ndoto za hofu na jinamizi usingizini

Tofauti na ndoto za hofu, jinamizi usingizini inamfanya mwanao aamke- anakumbuka ndoto yake na wakati mwingine kuhadithia na atahitaji umfariji katika hili. Kawaida watoto wanapata ndoto za hofu masaa machache baada ya kulala lakini jinamizi ndotoni hutokea katikati ya usiku yaani masaa machache kabla ya kupambazuka (kati ya saa nane na saa kumi na mbili).

Njia rahisi ya kutofautisha kati ya jinamizi usingizini na hofu ndotoni ni kujiuliza ni nani aliathirika zaidi asubuhi. Kama mwanao ataamka akiwa mwenye wasiwasi na huzuni basi ni “jinamizi usingizini” lakini kama ni wewe uliyesumbuka basi ni “ndoto za hofu”. Kuwa na amani kwasababu ndoto za hofu zinakusumbua wewe zaidi ya mwanao anayepitia.

Nifanye nini kama mwanangu ana ndoto za hofu wakati wa usiku?

Usimwamshe. Mtoto mwenye ndoto za hofu ni ngumu kumtuliza hasa kumshika kama unataka kumfariji. Unaweza kuongea nae kwa utaratibu kama yuko hatarini kujiumiza, lakini usimshike. Kabla ya kwenda kulala chukua tahadhari kama mwanao anaota akiwa anatembea usiku, watoto wenye ndoto za hofu wanatoka kitandani wakati mwingine, hivyo basi okota midoli au vitu chini sakafuni vinavyoweza kumtega, hakikisha milango na madirisha yamefungwa.

Chanzo na jinsi ya kujilinda na ndoto za hofu

Hakuna njia ijulikanayo ya kumlinda mwanao katika matukio haya, kwasababu hakuna anayejua nini chanzo chake.

Ndoto za hofu zinazaweza kusababishwa na kukosa usingizi wa kutosha au kunyimwa usingizi. Inaweza kusababishwa pia na msongo wa mawazo au kuchoka sana. Kuna ushahidi pia tatizo hili linarithiwa ndani ya familia. Jambo linalojulikana ni ndoto za hofu hazimaanishi mtoto ana matatizo ya kisaikolojia au amekasirishwa na kitu.

Tatua shida ya mwanao ya kukosa usingizi wa kutosha inayojumuisha kuamka katikati ya usiku na hakikisha anapata usingizi mara kwa mara kwa kufuata utaratibu mzuri wa kulala.

Muda Gani Mtoto Anaanza Kuota Meno

Kumbuka huu ni muongozo tu, watoto wote wanatofautiana wakati wa kuota meno. Ni jambo la kawaida kabisa mtoto kuota meno yake mapema kabisa yaani ndani ya miezi minne au kuchelelwa mpaka miezi 15. Watoto wachache wanaweza kuzaliwa na meno! Kumbuka watoto waliozaliwa kabla ya muda au wenye uzito duni wanaweza kuchukua mda mrefu kuota meno.

Mwezi Mtoto Mchanga
Miezi 5(kawaida miezi 4-7) Meno yanaanza. Fizi za mtoto wako zinavimba na kuwa nyekundu, meno mapya yanaanza kuchomoza. Baadhi ya watoto wanaumia meno yakianza kuota na wengine hawaumii, lakini watoto hawatulii kiujumla. Mkumbatie na kumfariji sana.
Miezi 6( kawaida miezi 5-10) Meno ya kwanza ya mwanao yanaota, mara nyingi meno mawili ya katikati chini (lower central incisors). Ujio wa meno haya utamfanya mwanao kupunguza usumbufu na maumivu.

 

Miezi 7( kawaida miezi 6-12) Meno ya juu ya katikati (the upper central incisors) yanaanza kuota wakati huu.

 

Miezi 9-16( kawaida miezi 9-12) Meno ya juu upande wa kulia kutokea katikati (the upper lateral incisors) yanaanza kuchomoza. Meno ya chini upande wa kulia kutoka katikat ( lower lateral incisors) yanafuata.
  Mtoto mkubwa
Miezi 14( kawaida miezi 12-19)

 

Magego ya kwanza yanaanza kuota upande wa chini na juu wakati mmoja. Magego ni meno yaliyo nyuma katika kinywa cha mtoto yanayotumika kusaga na kuponda chakula.

 

Miezi 18 ( kawaida miezi 16-23) Meno ya pembeni-chonge juu na chini ya kinywa yanaanza, meno haya yanatumika kurarua na kuchana chakula.

 

Miezi 26( kwaida 20-33) Magego ya pili yanaanza kukua juu na chini kwenye fizi.
Miaka miwili na nusu-miaka mitatu Mtoto wako ana meno timilifu ya kwanza 20
Miaka minne Taya na mifupa ya uso inakua na kuruhusu meno ya awali kutoka na meno ya utu uzima kuchukua nafasi. Kung’oa meno ya kwanza kwa mtoto kunaanza wakati huu. Kawaida watoto wa kike wanang’oa meno yao ya kwanza kabla ya watoto wa kiume, mara nyingi ni jino la chini la kwanza linang’olewa.

 

Mlo Kamili kwa Mtoto ni Upi?

Mlo kamili ni nini na kwanini mlo kamili ni muhimu?

Mlo kamili unajumuisha vyakula vingi tofauti, utakao msadia mtoto kupata mahitaji yote muhimu yatakayomsaidia kukua vizuri, kuchunguza zaidi na kuendelea kukua. Mlo kamili utamsaidia kujifunza ladha mpya na kukuza tabia ya kula itakayodumu maishani.

Lakini kumpatia mtoto mlo kamili inaweza kuwa changamoto, hivyo basi usiwe na wasiwasi kama umeshindwa kutimiza.

Vyakula gani mwanangu anahitaji ili kupata mlo kamili?

Vyakula vya wanga

  • Nafaka
  • Tambi
  • Wali
  • Viazi mviringo na viazi vitamu
  • Ndizi za kupikwa
  • Viazi vikuu

Vyakula vinavyotengenezwa na ngano ni vya wanga pia kama mkate. Usimlishe mwanao vyakula vyenye nafaka nzima tu kama unga wa mahindi usiokobolewa, vyakula hivi vinajaza tumbo la mtoto na kupelekea mtoto kuacha kula kabla ya kupata kalori na virutubisho muhumu.

Matunda na mbogamboga

Vyakula hivi ni muhimu kuupa mwili wa mtoto vitamini na madini muhimu yatakayomsaidia mtoto kukua.

Vyakula vyenye madini chuma na protini

  • Nyama
  • Samaki
  • Mayai
  • Karanga
  • Kuku na maharage

Vyakula jamii ya maziwa

Vyakula hivi vina madini ya kalsiamu kwa wingi muhimu katika ukuaji wa mifupa na meno ya mtoto.

  • Maziwa
  • Mtindi
  • Jibini

Maziwa ni chanzo kizuri cha kalsiamu lakini haitaji mengi kama hapo awali alivyokua mchanga. Mpatie 350ml mpaka 500ml kwa siku, usimpatie zaidi ya hapo inaweza kupunguza hamu yake ya kula.

Vyakula gani niweke kikomo kwa mwanangu?

Vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi

Vyakula kama:

  • Keki
  • Biskuti
  • Ice cream

Mwano anahitaji kalori nyingi kumfanya awe na nguvu, lakini vyakula hivi vina manufaa kidogo ya virutubisho. Vinaleta hatari ya mtoto kuwa na kiriba-tumbo.

Vyakula vyenye sukari

Kama pipi na chokoleti, vyakula hivi mwanao asile kila siku. Vina haribu hamu ya mtoto ya kula na kuharibu meno yake.

Vyakula vyenye chumvi.

Watoto wenye mwaka mmoja mpaka mitatu wanatakiwa kg 2 tu za chumvi kwa siku. Miaka 4-6 inaongezeka mpaka 3kg na 7-10 5kg. ni mtihani kuhakikisha mwanao anakula kiwango sahihi cha chumvi kwa siku. Vifuatavyo ni vidokezo vinaweza kukusaidia kumpa mwanaokiwango sahihi:

  • Usiongeze chumvi kwenye chakula chake
  • Weka kikomo kwa mtoto wakokatika ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa tayari nje ya nyumbani kama kuku, mishikaki au karanga.

Samaki wenye mafuta

Samaki wenye mafuta ni chanzo kizuri cha omega-3, vitamin na madini. Samaki wenye mafuta kama “mackerel”-samaki wa jamii ya bangala, “salmon”  “fresh tuna” wana mafuta mengi na inashauriwa usimpatie mwanao sana.

Karanga

Ikiwa mwanao ana tatizo la pumu au alegi ya chakula ongea na msahuri wa afya kabla ya kumpatia chakula chenye karanga.

Mbinu za Kumsaidia Mtoto Kuongea

Ni vipi unaweza kumsaidia mtoto wako kujifunza kuongea?

Kadri mwanao anavojifunza maneno mapya katika michezo ndivyo anavyoyabeba na kuyatumia kila siku. Zipo njia za kumsaidia mtoto wako kujifunza kuzungumza:

  • Zungumza kadri uwezavyo na mwanao. Mtazame usoni na uonyeshe kufurahia anapojaribu kuzungumza na wewe.
  • Zingatia zaidi kile ambacho mwanao anajaribu kusema kuliko jinsi anavyotamka matamshi yake. Jitahidi kumfanya mwanao ajisikie huru anapozungumza na wewe.
  • Pindi anaposema kitu sahihi, mpatie ripoti sahihi. Kwa mfano, unaweza kumwambia “ndiyo, ni sahihi, hichi ni kijiko”.
  • Mfanye mwanao kuona unachomaanisha, kwa kuzingatia unachokifanya na unachozungumza. Unaweza kusema “tunatoa viatu” huku ukimvua viatu vyake kisha “tunaondoa soksi” huku ukimvua soksi zake.
  • Pindi unampatia chakula cha mchana mwanao, weka sahani ya chakula mezani kisha mshike mikono na useme “ni muda wa chakula sasa” ataelewa kuwa chakula chake kipo tayari na kitaletwa mezani ikiwa tayari amenusa harufu na kuona maandalizi ya mezani. Anaweza asielewe maana ya “muda wa kula” kama hataona vitendo.
  • Chukua usikivu wake kwa kutaja jina lake na kumtazama machoni kabla ya kuzungumza naye. Hii itamsaidia kuelewa kuwa unazungumza naye.
  •  Mpe mwanao nafasi nyingi za kuzungumza katika kipindi chote cha shughuli za kila siku. Kama unamuuliza swali muache kwa sekunde 10 ili apate muda wa kukujibu.
  • Fafanua hali mbalimbali kwa kumtambulisha maneno mengi.  Nenda naye matembezi kwenye daladala, mtambulishe vitu anavyoviona na vielezee kwake.
  • Rudia kusema kile ambacho mwanao amejaribu kukuambia, hata kama hajatamka kwa ufasaha. Rudia kwa ufasaha kile alichotamka mtoto wako.
  • Rahisisha mazungumzo yako. Tumia sentensi fupi na zingatia maneno muhimu unapozungumza na mwanao. Hii itamsaidia kuzingatia taarifa muhimu.
  • Zima sauti nyingine zisizohitajika kama vile televisheni na redio. Hii itamsaidia mtoto kukusikiliza kwa umakini unapozungumza naye. Mtoto anapata tabu zaidi kuliko mtu mzima anaposikia kelele.

Nawezaje kumfundisha mtoto kuzungumza kwa kufurahia?

Ni rahisi kupata motisha kwa kufanya kitu unachofurahia. Hivyo utakavyoweza kuzungumza kwa kufurahi na mwanao, hii itamsaidia mtoto kutumia maneno kuweza kujielezea.

Kaa chini sakafu na cheza na mwanao. Muache achague mdoli au mchezo na uzungumze kile anachokifanya. Kwa kujumuika katika michezo na mwanao utampa nafasi nyingi za kumsikia kile anachozungumza kwa mifano sahihi.

Uwe na muda wa kumuigizia mdoli wake anayempenda  zaidi kwa vitendo. Mchanganye mdoli wake katika shughuli za kila siku. Mkalishe mdoli wake mezani kwa ajili ya chai na uanze kuzungumza naye kwa kinachofanyika pale.

Angalia vitabu ukiwa na mwanao hata kama hutamsomea hadithi lakini atasikiliza  na kujifunza zaidi utakapokuwa unazungumzia picha.

Furahi na mwanao kwa kuimba nyimbo za darasa la awali, kwa kuwa kadri unavyofanya hivyo ndivyo ambavyo mtoto wako atapenda kujiunga.

Cheza na mwanao michezo kwenye simu, hii itamsaidia zaidi kujifunza kuchangia katika mazungumzo.

Jaribu kusikiliza michezo kama vile:

  • Michezo ya kupiga makofi, piga kwa mtiririko maalumu kisha subiri kuona kama mtoto wako naye atafanya hivyo.
  • Chagua picha sahihi ya sanamu za wanyama na utengeneze sauti kwa mnyama mmojawapo kwa mfano “moo” kisha usubiri mwanao achukue sanamu ya ng’ombe kati ya sanamu ulizomuwekea.