Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Pombe na Sigara Wakati wa Kunyonyesha

Wataalamu wanasema unywaji wa pombe wa mara moja moja hauna madhara wakati unanyonyesha. Pombe inapita kwa urahisi kwenye maziwa, lakini inatoka kwa urahisi kwenye maziwa. Madhara yake kwa mtoto ni sawa na madhara kwako. Kama hakuna madhara ya pombe kwako, basi na kwa mtoto wako madhara ni kidogo pia.

Kiasi cha pombe katika maziwa ya titi kinadumu ndani ya dakika 60-90 baada ya kutumia(ukiwa umekula) na 30-60 baada ya kunywa bila kula chakula. Inachukua masaa 2-3 pombe kupotea ndani ya mwili wa mwanamke.Ushauri wa wataalamu inabidi kusubiri masaa mawili baada ya kunywa pombe kisha umnyonyeshe mtoto wako.

Madhara ya kunywa pombe ni pamoja kupitiliza usingizi kwa mtoto ambaye analala muda mfupi. Pombe kugeuka harufu au ladha ya maziwa yako, na kusababisha mtoto kunyonya kidogo. Kunywa pombe huweza kusababisha uzito mdogo, upungufu wa nguvu, na wasiwasi wa usalama kwa wengine

Mimi navuta sigara. Je, naruhusiwa kunyonyesha?

Wataalamu wanashauri kama wewe unavuta sigara, kunyonyesha ni njia nzuri kwa mtoto wako kupata virutubisho. Tumbaku inaeneza sio tu nikotini bali pia dutu nyingine hatari kupitia maziwa ya mwilini. Kadiri unavyozidi kuvuta sigara ndivyo unavyomuhatarisha mtoto wako. Wataalamu wanashauri kuacha, au kama huwezi kuacha, punguza idadi unayotumia. Kama huwezi kuacha jaribu kupunguza idadi unayotumia, vuta sigara muda kidogo baada ya kunyonyesha na mbali na chumba alicho mtoto ikiwezekana nje kabisa. Kumbuka kwamba moshi wa sigara ni hatari kwa mtoto wako. Ki uhalisia ni vyema ukaanza kuchukua taratibu za kuacha kuvuta sigara kabisa.

Je ni Muda Gani Sahihi wa Kumnyonyesha Mtoto

Kama mama mpya utaanza kugundua ishara na milio ya mwanao inayomaanisha anataka kunyonya, kubembelezwa, kubadilishwa nepi au hitaji lingine. Kwa wakati huu kulia ni njia kuu ya mawasiliano ya mwanao (njia ya kufikisha ujumbe). Angalia ishara hizi ili upate kugundua kama mtoto wako atakuwa na njaa hivi karibuni:

  • Mtoto akiweka mikono mdomoni,kufanya kama anayonya,kutoa ulimi nje,akilamba mdomo,kutoa udenda.
  • Mtoto akijisogeza na kugeukia upande wa mtu aliyembeba.
  • Mtoto akitoa milio na miguno ya kitoto, akijinyoosha, kuamka usingizini.
  • Kulia ni ishara ya mwisho- mtoto akifikia hatua hii ya kulia inaweza kuwa ngumu kumnyonyesha mtoto wako. Kugundua ishara za awali za mtoto wako akiwa na njaa itasaidia kumfanya mtoto ashibe na maziwa mengi kutoka.

Kunyonyesha usiku

Unaweza kugundua mwanao kunyonya zaidi usiku, mara nyingi kila saa kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku. Mchana na jioni maziwa yanakua na fati nyingi zaidi kuliko asubuhi, hivyo mtoto atahitaji aidi maziwa yenye fati nyingi kumsaidia kukua zaidi kwaajili ya siku inayofuata. Mara nyingi baada ya muda huu wa kunyonya usiku mtoto atalala vizuri masaa 3-4. Mara mtoto wako atakapofikisha mwezi mmoja akiwa na uzito mzuri sio lazima kumuamsha katikati ya usiku.

Lishe kwa Mama Mzazi Anayenyonyesha

Unaweza ukala kila kitu. Ladha za vyakula zitaingia kwenye maziwa, na watoto wengi wanapenda.

Mara kwa mara mtoto hutenda au kujibu kutokana na kitu kwenye mlo wa mama – vitu vya hatari sana ni maziwa ya ng’ombe na chakula chenye dutu zenye kufanya uvutikaji wa nafaka haswa kwenye ngano. Kama mtoto wako atapata shida kutokana na kitu ambacho umekula wewe ni vyema ukamchunguza kwa makini. Dalili zinaweza kujumuisha kupiga chafya, kinyesi cha kijani chenye ukamasi au damu na kuwashwa au kujaa gesi tumboni. Kuondoa hatari hizo kwenye mlo wako inaweza kuwa ngumu lakini ni vema kujaribu kwa manufaa ya mtoto wako.

Baadhi ya wamama wana wasiwasi kuhusu kutumia kahawa. Kiasi kidogo cha kahawa kinapita katika maziwa na utafiti unaonyesha matumizi ya kahawa yana tofauti kidogo kwa mtoto wako. Kama una mtoto mwenye kuchangamka sana, na mgumu kukabiliana nae, na mwenye kusumbua wakati wa kulala, fikiria kupunguza matumizi ya kahawa kwenye mlo wako(kahawa, vinywaji vyenye wanga, chai, chokoleti n.k).

Je, kunyonyesha kutanisaidia kupunguza uzito?

Wataalamu wengi wa afya wanashauri kula kalori 300 zaidi ya kawaida kwa siku kwasababu kunyonyesha kunahitaji nguvu ya ziada. Kama hutumii nguvu ya ziada, mwili wako utaanza kutumia virutubisho vinavyotumika kutengeneza maziwa, kuunguza dutu za fati zilizohifadhiwa na kusaidia kupunguza uzito. Kwa kawaida kama unanyonyesha ni vyema ukawa unakula wastani wa kalori 2500 kwa siku. Hizi unaweza kuzipata kwa kuhakikisha unakula mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu.

Kunyonyesha

Hongera kwa kujifungua mtoto wako! Tunajua umechoka na unaweza ukawa unamuangalia mtoto wako kwa furaha sana. Unaweza ukawa unataka kuanza kumnyonyesha, kitu ambaho ni bora kwa afya ya mtoto wako. Shirika la afya duniani na shirika la umoja wa mataifa kwa watoto wanasisitiza kumnyonyesha mtoto wako kwa muda usiopungua miezi sita bila kumpa kitu kingine chochote. Na vile vile uendelee kumyonyesha na kumpa vyakula vingine mpaka atakapofikisha miaka miwili au zaidi. Kama umeamua kumnyonyesha mtoto wako anza mara moja na usikatishwe tamaa na namna mambo yanavyokuwa magumu, kwani kunyonyesha huwa na tabu kidogo mwanzoni.

Masaa 48 ya kwanza na mtoto wako

Muweke mtoto wako kifuani kwako kwa masaa ya mwanzo baada ya kujifungua. Hakikisha ngozi yako nay a mtoto wako zinagusana ili muweze kuanza kujuana mapema lakini pia atapata joto zaidi kutoka kwako. Kwa kawaida baada ya masaa machache mtoto wako ataanza kuhangaika kutafuta chuchu zako. Usiogope kuomba msaada kutoka kwa mkunga au nesi aliyepo karibu kukusaidia kumsogeza kwenye chuchu. Mwanzoni kichanga chako kinaweza kisijaribu kunyonya kabisa na kuweka midomo yake tu kwenye chuchu. Kuwa mvumilivu, pale mtoto wako atakapokuwa amepata nafasi nzuri utasikia kitu kama kinavuta.

Kumbeba mtoto wakati wa kunyonya

Ni vyema kama utamuweka mtoto wako kwenye mkao wa kunyonya masaa mawili baada ya kujifungua. Watoto wanaoanza kunyonya masaa mawili baada ya kujifungua huwa na uwezo wa kunyonya maziwa mengi zaidi siku ya nne ukilinganisha na wale ambao hawakufanikiwa kunyonya masaa mawili baada ya kujifungua. Baada ya hapo wewe na mtoto wako mtakuwa mmechoka sana, pata kumpumzika lakini uamke kila baada ya masaa matatu hivi ujaribu kumnyonyesha. Jaribu kumnyonyesha hadi mara 8 katika masaa 24 ya kwanza baada ya kujifungua. Kwa kawaida ni vyema kumnyonyesha mtoto kila baada ya masaa matatu ndani ya mwezi wa kwanza ili kuweza kuhakikisha kiasi cha maziwa hakipungui na mtoto anaongezeka uzito inavyotakiwa.

Kumuanzishia Mtoto Wako Vyakula Vigumu

Tumefanikiwa kuona picha mbalimbali, rafiki zetu na watoto wao wadogo walio umri mkubwa kidogo wakituma picha kwenye mitandao ya kijamii, watoto wao wakianza kula vyakula vigumu. Maranyingi kuna tabasamu za furaha na saa nyingine kuna sura za kukasrishwa au kutofurahishwa. Lakini kwa pamoja picha hizi zina ujumbe mmoja ambao ni chakula kingi juu ya mtoto kuliko chakula anachokula.

Muda unapita kwa kasi, na siku si nyingi utaanza suala zima la kumuanzisha chakula kigumu mtoto wako. Ikiwa ulifurahishwa na kumyonyesha mtoto wako miezi yote iliyopita, muda utakuja wa kumkalisha mtoto wako na kumuonjesha chakula kigumu. Habari njema ni kwamba wewe na mwenzi wako mna miezi kadhaa ya kumlisha mtoto maziwa au kumnyonyesha.

Ila swali kuu kwa wazazi wengi ni nini na lini, waanze kumlisha vyakula vigumu?

Mashirika makubwa ya afya duniani kama UNICEF na WHO yalikubaliana kuwa kumuanzisha mtoto vyakula vigumu kuanzishwe rasmi kuanzia mtoto akiwa na umri wa miezi sita huku ukiendelea kumnyonyesha.

Wakati wa mwanzoni ni vyema kuanza kumpa vyakula laini ukiwa unamjengea tabia ya kula vitu vigumu taratibu.

Baadhi ya watoto wako tayari kuanzishwa vyakula vigumu wakiwa na miezi mitano na nusu, wakati wengine wanaanza mwezi wa saba, kwa nini yote haya?

Sababu ni rahisi. Kwanza, kusubiri mpaka mtoto wako akiwa na miezi sita ina maana mtoto wako ana ongezeko la mfumo wa kinga tayari kwa kulinda mwili wake kutoka kwenye magonjwa yaletwayo na vyakula. Huu ni umri ambao mfumo wao wa mmeng’enyo unaanza kukua na kushughulikia mmeng’enyo wa fati, protini na kabohaidreti tata bila kuhitaji msaada wa dutu zinazotolewa na maziwa kusaidia mmeng’enyo ndani ya miezi hiyo michache ya kwanza. Kwa sababu hii ndio maana kumuanzisha mtoto vyakula vigumu kabla ya miezi sita hupelekea mtoto kuwa mnene (kiribatumbo) kipindi cha ujana na utu uzima.

Hata baada ya vyakula vigumu kuanzishwa, weka akilini mtoto wako bado atapata virutubisho vingi na kwa wingi kutoka kwenye maziwa ya kunyonya, kwa hiyo usipange kupunguza kumnyonyesha.

Jinsi ya Kumlisha Mtoto kwa Chupa

Vifuatavyo ni vidokezo vinavyoelezea jinsi ya kumlisha mtoto kwa chupa katika hali ya usalama:

Hakikisha umekaa vizuri. Mkao utakao kusadia kumshika mtoto wako vizuri na kumuangalia machoni ukiwa unamlisha. Kumlisha mtoto kwa chupa ni nafasi nzuri ya kuwa karibu na mtoto wako na kumjua zaidi.

Mpakate mtoto wima ukiwa unamlisha kwa chupa. Shika kichwa chake vizuri ili aweze kupumua na kumeza vizuri. Anza kwa kuweka chuchu ya chupa kwenye midomo ya mtoto, mara atakapofungua mdomo mruhusu aivute chuchu ya chupa mwenyewe kwaajili ya kunyonya maziwa ndani ya chupa.

Daima mpatie mtoto mda wa kutosha wa kula.

Mtoto wako atahitaji mapumziko mafupi wakati unamlisha na atahitaji kucheua wakati mwingine. Ikiwa mtoto wako hataki kunywa maziwa tena, msimamishe wima, taratibu mpige ige mgongoni ili acheuwe.

Kumcheulisha Mtoto Baada ya Kunyonya

Baadhi ya watoto wanaonyonya hawahitaji kucheua sana. Wengine wananyonya na wanakunywa maziwa kwa haraka na wanahitaji kucheua. Baadhi ya wamama hujaribu kuwacheulisha watoto kipindi wakiwabadilisha upande wa ziwa, wengine wanasubiri mpaka wagundue mtoto wao ana hali ya kutofurahi au ameshiba.

Baadhi ya wazazi wana wasiwasi juu ya kiasi cha maziwa mtoto anachotoa baada ya kucheua. Muda mwingi mtoto kutapika ina maana mtoto wako amekula zaidi na tumbo limeshindwa kubeba au kuna maziwa yameingia kwenye koo la hewa. Weka akilini sio maziwa tu yanayotolewa mtoto akicheua – kuna mchanganyiko wa makohozi na mate pia. Kwa hiyo mtoto akitapika wakati anacheua, haina maana anapoteza kila alichokula.

Ikiwa, hata hivyo, mtoto wako anaonyesha ishara zifuatazo, unaweza kuzungumza na mtoa huduma ya afya ya mtoto wako: kutapika matapishi au rangi yenye kuonekana kama mashamba ya kahawa, kijani kinachong’aa au matapishi yenye rangi ya njano, kukataa kula mara mbili kwa mfululizo, ukosefu wa uzito, na matapishi yanayoambatana na ishara nyingine za ugonjwa kama vile homa au ugumu wa kupumua.

Je Mtoto Wako Anashiba?

Sheria ya kwanza ya kumnyonyesha mtoto ni kumuangalia na sio kuangalia saa(mda). Kumuwekea mtoto ratiba ya kunyonya kunaweza kuwa hatari katika upatikanaji wa maziwa yako. Lakini kama utamruhusu mtoto wako kuamua muda gani na mara ngapi ananyonya, utakuwa na uhakika mtoto wako anapata maziwa ya kutosha na upatikanaji na usambasazaji wa maziwa yako kuwa imara. Kama mtoto wako amelala kwenye kifua chako upande mmoja wa bega, mbadilishe kuelekea upande mwingine. Ikiwa mtoto wako bado ana njaa, atakula zaidi. Ikiwa hana njaa, jiandae kwa ulishaji ujao.

Ishara zinazoweza kukujulisha mtoto wako anapata maziwa ya kutosha hujumuisha:

Mtoto wako mchanga atanyonya mara 8-12 ndani ya masaa 24.

Mtoto wako anapata choo kila siku baada ya kufikisha siku 4.

Kinyesi cha mtoto wako kinabadilika kutoka nyeusi hadi kijani hadi manjano kadiri anavyokunywa maziwa vizuri (na inapaswa choo kuwa cha njano baada ya siku 4)

Mtoto wako anatakiwa abadilishe nepi 5-6 nzito zilizo loana kila siku baada ya siku ya nne.

Mtoto wako anaongezeka gramu 112 – 196 kwa wiki baada ya kurejesha uzito wa kawaida wa kuzaliwa (kawaida ndani ya siku 10-14).

Watoto wote wana siku ambazo wananyonya sana na siku nyingine ambazo hawanyonyi. Hizi ni tabia za kawaida za unyonyeshaji na sio ishara kwamba kuna kitu sio sawa.

Homoni ya Prolaktini itazalisha maziwa yako. Ikiwa unanyonyesha mara nyingi, kiwango cha homoni ya prolaktini kitaendelea kukaa na kuongezeka kwa wingi. Ikiwa itaongezeka sana na kuwa ya kiwango cha juu, utatengeneza maziwa mengi zaidi na mtoto wako atapata uzito kwa urahisi. Kwa hiyo ni muhimu kuwa unamlisha mara nyingi. Ikiwa unanyonyesha mara kwa mara, kwa muda mrefu, ongezeko la homoni ya prolaktini itashuka. Hivyo ni bora kunyonyesha mara nyingi, yaani mara 8-10 katika masaa 24, na ukitumia karibu dakika 15-45 kwa mlisho mmoja.

Jinsi gani naweza ongeza wingi wa maziwa yangu?

Kutoka kwa maziwa ni njia ya kuongeza utengenezaji wa maziwa. Kama unahisi utokaji wa maziwa ni mdogo kabisa, njia zifuatazo zinaweza kusaidia:

Hakikisha mwanao anatoa maziwa vizuri kutoka kwenye titi lako

Mnyonyeshe kila mara

Badilisha upande kila wakati kila unapomnyonyesha.

Epuka chupa za maziwa, labda kama ni muhimu kwasababu ya matibabu, hakikisha unafikia mahitaji ya mtoto wako kunyonya kutoka kwenye titi lako.

Kamua maziwa na fanya kama ratiba yako, unaweza kukamua maziwa dakika 5-10 kila baada ya kumnyonyesha.

Amka kumnyonyesha au kamua angalau mara moja au mbili usiku.

Fanya Muda wa Kula Uwe Wenye Furaha kwa Mtoto Wako

Haijalishi ni njia gani unatumia, kumwanzishia mwanao vyakula vigumu, unapaswa daima kujitahidi kufanya wakati wa chakula kuwa wa kufurahisha kwa mtoto wako. Kamwe usilazimishe kitu ambacho hakipendi au kuanza tabia ya kujadiliana kuhusu chakula.

Watoto wengi hupitia hatua fulani ya kuchagua chakula au wakati mwingine, kuanzisha tabia tofauti wakati wa kula, lakini ni matumaini kuwa athari hizo zitapungua baadae. Ni vema zaidi kumpa achague na kuangalia anachopenda. Kwa hiyo kufanya kula kuwa tukio la kufurahisha, si kitu ambacho kitaonekana kama kazi kubwa.

Wakati huo huo, kumbuka kwamba bado wanapata lishe yao zaidi kwa kunyonya-hivyo usimlazimishe mwanao kumpa vyakula vingine zaidi ya maziwa yako yenye virutubisho vingi. Muamini mtoto wako akujulishe anachohitaji na uwe nae wakati wote wa chakula, maana ni muda wa kufurahia kwa kuunganika na kushirikiana na mtoto wako

Faida za Kunyonyesha kwa Mama

Tukiongelea zaidi umuhimu wa kumyonyesha mtoto wako, huwa inasahaulika kuwa kuna faida nyingi kwako pia!

Kikubwa sana, mara baada tu ya kujifungua kunyonyesha kunaepusha kutoka damu kupitiliza na kukusaidia kurudisha mfuko wa mimba katika hali ya kawaida kama ulivyokuwa kabla ya mimba mapema zaidi.

Kunyonyesha kunaokoa muda na pesa na hauhitaji muda wa ziada kuandaa.

Hatari ya magonjwa ya mifupa kuwa laini na kuvunjika kwa haraka, pamoja na magonjwa ya mfumo wa uzazi na kansa ya titi yanapunguzwa ukinyonyesha.

Inasaidia kupunguza uzito na kuendeleza asili ya mzunguko wa kushika mimba, ujauzito na kuzaliwa mtoto.

Kama unanyonyesha, kunyonyesha usiku ni rahisi na ina usumbufu kidogo.

Pia kunyonyesha kuna kufanya mwenye furaha, kunyonyesha kunatoa homoni ambazo zinaongeza ujasiri, kujikubali na kupumzika na kusaidia kuunganika kwa mama na mtoto.