Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Vidokezo Muhimu Kusaidia Mtoto Wako Kulala Vizuri

Vidokezo kusaidia mtoto wako kulala vizuri

Wazazi wengine wana watoto ambao wamelala vizuri tangu mwanzo. Kwa wazazi wengine, huenda hawakuwa na masaa zaidi ya matatu ya usingizi usioingiliwa kwa miezi mingi.

Ikiwa mtoto wako ana matatizo ya usingizi mara nyingi, au unashughulika na suala hili mara kwa mara, kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kufanya ili kumsaidia mtoto wako kulala vizuri.

Weka chumba cha mtoto wako kiwe na mwanga hafifu au giza wakati wa kulala. Mwanga hafifu wa usiku ni sawa. Lakini kumbeba mtoto wako katika chumba chake kizuri cha kulala au kuwasha taa katikati ya usiku haiwezi kumsaidia mtoto wako wakati wa usiku. Giza huchochea ubongo kuzalisha homoni ya melatonini, ambayo husaidia mtoto wako kupata usingizi.

Ni muhimu pia kuepuka kumchangamsha mtoto wakati wa kulala. Wakati wa kucheza ni bora na watoto wanahitaji kustawi. Lakini michezo ambayo inasababisha msisimko wa kuendelea kucheza zaidi inapaswa kufanyika wakati wa mchana. Badala yake, fanya shughuli zisizo na msisimuko. Mwimbie au kuzungumza kwa taratibu na mtoto wako ili kumsaidia kupumzika.

Umuhimu wa Ratibu ya Kulala kwa Mtoto

Umuhimu wa kuwa na ratiba ya kulala

Utakuwa umejifunza kutoka kwenye vitabu au wamama na walezi wengine, kuhusu umuhimu wa kuwa naratiba ya kulala kwa mtoto wako. Ratiba tulivu nay a kuzingatiwa itampatia mtoto ishara ya kujua mda wa kwenda kulala. Ratiba hi nzuri ya kulala inaweza kumsaidia mtoto kupumzika na kupotelea usingizini kiurahisi.

Utaratibu mzuri wa kulala ni mda muafaka wa kuungana na mtoto wako. Ni muda mzuri wa kupumzika na kumkumbatia mtoto wako. Ikiwa mtoto wako amekata kunyonya kwa chupa,hakikisha unamnyonyesha vizuri kabla ya kulala. Wakati wa kumbembeleza na kumlaza mtoto ni vizuri na baba yake akahusika katika ratiba hii ili kuwaunganisha baba na mtoto.

Utaratibu mzuri wa kulala unasaidia watoto kujua tofauti ya mchana na usiku, hata watoto wachanga.

Kumsaidia mtoto kuelewa tofauti hii, ungana nae kadiri uwezavyo mchana. Hakikisha chumba kina mwanga wa kutosha. Cheza nae nje kidogo kama hali ya hewa inaruhusu. Shughuli zote hizi zitamsaidia mtoto kuelewa mchana ni mda wa kuwa mchangamfu na kucheza. Wakati wa usiku fanya kinyume na shughuli za mchana,hakikisha chumba kina mwanga duni na tulivu. Mfundishe mwanao kuwa usiku ni wakati wa kulala.

Msaidie mtoto kutulia wakati wa usiku. Unaweza kumuogesha na kumvalisha nguo zake za kulala, kumlisha,kumuimbia nyimbo laini za kulala na kumkumbatia sana. Ondokana na shuhuli zitakzomfanya awe mchangamfu.

Kumbuka kuzingatia utaratibu huu wa kulala na kufanya marekebisho kidogo kadiri mwanao anavyokua.

Mtoto Anahitaji Usingizi Kiasi Gani?

Kiasi gani cha usingizi mtoto wako anahitaji?

Ni muhimu kujua ni kiasi gani mtoto wako anahitaji kulala katika kila hatua ya ukuaji wake. Kuelewa mahitaji ya mtoto wako husaidia kuwa na mpangilio mzuri. Kwa mfano, wakati mtoto wako akiwa mchanga anahitaji usingi mwingi. Watoto wengi wachanga hulala kati ya masaa 16 hadi 18 kwa siku mpaka wafikapo miezi miwili.

Lakini usitarajie usingizi huo mrefu uje wakati wa usiku, wakati mtoto wako ni mchanga, anahitaji kula kila baada ya masaa mawili. Tumbo lake ni dogo sana na hupokea maziwa kidogo kidogo kila anaponyonya. Ni asili kwa watoto wadogo kulala kwa muda mfupi. Kutarajia mtoto wako atalala zaidi inaweza kukufanya uchanganyikiwe.

Watoto wadogo hawajui kujituliza ili walale peke yao bado. Hapa ndipo kubembeleza kunapokua kugumu. Kama unajali juu ya kumuharibu mtoto wako mdogo kwa sababu ya kumbembeleza, usijali. Unaweza kumfundisha kujituliza mwenyewe wakati wa kulala.

Muda ukifika akishaweza kubeba chakula cha kutosha tumboni, atapata uwezo wa kulala muda mrefu usiku. Kati ya miezi miwili na minne, mtoto wako ataweza kulala kwa masaa tano au sita usiku. Ingawa sio masaa nane uliyofikiria, ila bado ni maendeleo kutoka kuamka kila masaa mawili mpaka matatu.

Karibia miezi minne mpaka sita, mtoto wako anaweza acha kunyonya na kulala kwa masaa sita mpaka 12 usiku. Ni vyema kujua, watoto wanatofautianana na haya yanaweza kubadilika, ila utafiti unaonyesha asilimia 60 ya watoto wanalala usiku mzima katika umri wa miezi sita. Kama mtoto wako ni miongoni mwa asilimia 40 ambayo haijafikia hatua hii bado, basi kuwa mvumilivu na subiria. Katika miezi tisa, asilimia 80 ya watoto wanalala usiku mzima.

Tabia Nzuri za Ulalaji Bora kwa Mtoto

Kumfundisha mtoto wako tabia nzuri za ulalaji

Mtoto wako anahitaji vitu vichache muhimu, chakula, kucheza, kulala na mapenzi. Haionekani kama itakua ngumu sana. Ila kila ikija kwenye suala la kulala, mambo huwa hayaendi ipasavyo. Kumfanya mtoto wako alale muda mwingine inakua ni changamoto. Kutoka kwenye kusumbuliwa na tumbo, meno mpaka kwenye woga wa kuachwa, kuna sababu nyingi kwa nini mtoto wako halali. Habari njema ni kwamba, kuna vitu vingi unaweza fanya kukusaidia ili mtoto wako awe na tabia nzuri ya kulala.

Kukuza tabia nzuri za kulala inasaidia mtoto wako kulala kwa urahisi na kupata kila anachotaka. Kumjengea tabia nzuri za kulala inaweza kuzuia matatizo ya kulala kuendelea zaidi.

Moja ya tabia wataalamu wanashauri ni kumuweka mtoto kitandani akiwa amechoka lakini sio akiwa amesinzia. Kila mtoto ni tofauti. Jifunze kugundua jinsi mtoto wako anaonekana akiwa amechoka. Kwa mfano baadhi ya watoto wanasugua macho yao, wanalia au kuvuta masikio yao wakiwa na usingizi. Mtoto wako anaweza kukunja uso au kusumbua akiwa amechoka. Muweke mtoto wako kitandani taratibu huku unamsaidia kupotelea usingizini mwenyewe. Hii inamfundisha kujituliza mwenyewe akishtuka toka usingizini.

Kumuweka mtoto wako kitandani na kupata usingizi muda huo huo siku zote nitabia nzuri kuifikiria. Mtoto wako ana uwezekano wakufuata ratiba hiyo kama itakua thabiti. Usijichoshe kukosa mapumziko ya usingizi au kumuweka mtoto wako kitandani kwa kuchelewa. Rudia ratiba yako ya kumuweka mtoto kitandani mapema kabla hajalala kuliko akiwa ameshalala ili uweze kupata nafuu ya ubembelezaji.

Matatizo ya Usingizi kwa Mtoto

Omba msaada kama unajisika mambo hayaendi vizuri

Wazazi wengi wanapata shida kuwafanya watoto wao walale. Hata kama mambo yalikua yanaenda vizuri, muda fulani matatizo ya kulala yanakuja. Baadhi ya matatizo yanaweza kuanza kwasababu ya suala la kimwili, kama kutoka maziwa bila kutegemea. Muda mwingine kitu cha kihisia kinaweza msababisha mtoto kulia katikati ya usiku. Mfano mtoto wa miezi kumi anaweza kuamka kila mara wakati wa usiku kwasababu ya hofu ya kuachwa wakati mama yake anaenda kazini.

Kama mtoto wako ana matatizo ya kulala na kujisikia kutokuwa sawa, omba msaada. Daktari wa mtoto wako anaweza kuwa msaada mkubwa. Anaweza kudhibiti tatizo, kama kutokucheua au kucheua sana au matatizo mengine ya mfumo wa chakula na kukupatia maoni yenye kukusaidia mtoto wako apumzike vizuri.

Unaweza pia kupata ushauri kutoka kwa majirani zako ambao wana watoto wakubwa, na kujifunza ni yapi walifanya kipindi wakiwa na tatizo kama lako.

Ni muhimu kwa wazazi wa mtoto kuwajibika pamoja kama mtoto wao ana matatizo ya kupata usingizi. Kama mtoto wako ana usingizi wa shida ina maana na wewe pia utakuwa na shida hiyo. Ni hali ya asili kuwa na hasira katika kipindi hiki. Jaribu kuwa makini kwenye hili tatizo na kuwajibika pamoja na mwenza wako. Ikiwa wote mtakua pamoja na kusaidiana, mambo yanaweza kuwa rahisi.

Kumsaidia Mtoto Kulala Usiku Kucha

Nini cha kufahamu kuhusu kulala usiku kucha

Mara nyingi wazazi wana kazi kubwa kuhakikisha mtoto wao analala usiku mzima. Ila kwa watoto, kulala usiku mzima kuna maanisha nini?

Unapofikiria kulala usiku, akili inawaza masaa nane ya usingizi, usioingiliwa. Mtoto wako ana wazo tofauti kulingana na hatua yake ya ukuaji. Kwa mfano, watoto wachanga hulala na kuamka kila usiku. Usiku sio muda wa muhimu sana kwa mtoto mwenye umri wa wiki tatu.

Lakini mara mtoto wako anapokuwa mkubwa kidogo, kulala kwake usiku ni kati ya masaa 6-12. Kwa mara chache za kwanza utaingiwa na wasiwasi kama mtoto wako yuko sawa, ila usijali ni hali ya kawaida na mtoto wako ataendelea kubadilika kadiri anavyokua.