Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 8

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikiz)

 • Anapenda kuunda na ufundi.
 • Anapenda kuzunguka mpaka apate kizungzungu, kuruka sehemu ndefu na kudondoka ghafla (kuporomoka).

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anapendelea michezo yenye kanuni za kufuata.
 • Anapenda kuomba kibali /ruhusa.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anatumia maneno na sentensi alizokariri
 • Anaanza kuainisha na kutenga hisia na majibu ya watu

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 5

Mtoto wa umri huu:

 • Anaweza kuvaa mwenyewe isipokuwa kufunga viatu.
 • Anaweza kuruka na kutua na mguu mmoja.
 • Anaweza kutupa mpira na kudaka.
 • Anauliza maswali mengi na ana shahuku.
 • Anaigiza wengine.
 • Anatambua herufi na namba.
 • Anaweza kuiga kuimba nyimbo, hadithi.
 • Anashirikiana na wenzake kwenye michezo.
 • Anasaidia watu nyumbani.
 • Anaelewa hisia za watu wengine.

Ukuaji wa kimwili katika umri huu

 • Anakomaa kiakili
 • Anaweza kusimama na mguu mmoja bila kuyumba
 • Anashuka ngazi bila kujishika
 • Anakimbia na kusimama bila kuanguka
 • Anaweza kuruka juu ya matofali na miguu yote bila kuanguka
 • Anaweza kuruka urefu wa hatua tatu na kutua na miguu yote

Maendeleo ya mtoto katika jamii ndani ya miezi hii

 • Anapenda kujitegemea lakini bado anatumia mda wake na wazazi wake.
 • Mtoto aliye na miaka 5 anapenda kujihusisha na mengi, na mara nyingi atakataa msaada wako.
 • Wanafanya usafi wenyewe, wakati mwingine bila kuamriwa.
 • Wapenda kubembeleza wenzake hasa kama walihusika katika ugomvi.
 • Wanaweza kujielezea wanavyohisi, mfano “huzuni, hasira, kuchanganyikiwa , uoga,kuvunjika moyo” n.k
 • Wanakua kipaji cha kuwasiliana na kujadiliana na marafiki zake katika michezo yao.
 • Wanaweza kuwa na rafiki mmoja kipenzi.
 • Wana vipaji vingi vya kushirikiana na rafiki zake wengine.
 • Wanashiriki katika kazi za vikundi shuleni na wanaweza kusubiria zamu yao kuongea au kufanya onyesho.
 • Wazazi na walimu ni watu muhimu kwao, na chanzo cha habari na faraja.
 • Wanaanza kufuata kanuni na sheria na wakati mwingine wanakumbusha wenzao, bila maelekezo ya mwalimu au mzazi.

Hatua za ukuaji katika kuongea na kujifunza

 • Wanaelezea mahitaji, hisia, na mawazo yao.
 • Wanapenda kupata habari zaidi.
 • Wanafanya suluhisho la matatizo na kuchunguza mawazo yao.
 • Wanafanya mipango ya vitu wanavyohitaji.
 • Wanashauri wenzao na kutetea mada.
 • Wanatengeneza na kuhadithia hadithi.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 4

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaruka kwa mguu mmoja.
 • Anashuka ngazi bila kushika ukuta.
 • Anaimba nyimbo alizosikia katika vipindi vya watoto.
 • Anataja majina ya baadhi ya rangi na maumbo.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anataja jina lake lote.
 • Ana misamiati ya maneno 1500.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anaweza kushika mpira.
 • Anahesabu zaidi ya kumi.
 • Anazitambua herufi zote.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 11

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaruka sehemu ndefu na kutua na miguu.
 • Ana usikivu wa dakika 8-12.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anaweza kutumia zipu na vifungo vya nguo zake.
 • Anaanza kusema uongo.

Mwanao anaweza kuwa hodari katika (watoto wachache wanaweza)

 • Anaendesha baiskeli.
 • Anaweza kutenganisha kati ya kitu halisi na kisicho halisi.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 10

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anavaa mwenyewe
 • Anapiga mswaki na kunawa mikono mwenyewe
 • Anacheza kwenye makundi na wenzake

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kaimarika katika uchoraji.
 • Vipaji vyake vinaanza kuchipua.
 • Anashirikiana na wenzake.
 • Anapungua kimwili sasa anavyokubaliana na maisha.
 • Anachora picha inayoeleweka inaweza kuwa picha ya familia.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anajua siku ya leo na kesho.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 9

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Mwenye aibu.
 • Anaweza kukunja karatasi mara tatu.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anapungua kimwili sasa anavyokubaliana na maisha.
 • Anachora picha inayoeleweka inaweza kuwa picha ya familia.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anaweza tafuta kitu hata ukificha sana.
 • Anapanga vizuri maumbo na rangi katika makundi yake.
 • Anamalizia sentensi

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 7

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kupanda na kushuka ngazi bila kuyumba au kuhitaji msaada.
 • Anaendesha baiskeli ya watoto vizuri.
 • Anashika penseli vidoleni vizuri.
 • Anaweza kufunga vifungo vikubwa.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anaweza kuvaa viatu mwenyewe lakini hawezi kufunga kamba.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anatambua baadhi ya maneno na herufi.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 6

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaelewa utaratibu wa siku nzima.
 • Anapanda, kuteleza na kubembea kwenye sehemu za kuchezea.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Amejifunza kutembea kwa njia ya ubunifu na atakua huru.
 • Ameelewa dhana ya maneno kama juu, chini, kuzunguka.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anaelewa kinyume cha maneno
 • Anaelewa vipimo tofauti mfano wewe ni mrefu kiasi gani / kuna maji kiasi gani kwenye kikombe

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 5

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anatumia misamiati ya maneno karibia 900.
 • Anaelewa maneno kama “ndani” “nje” “nyuma” na “mbele ya”

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anajaribu kufanya mawazo yake kwa vitendo.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anatengeneza muundo na maumbo, na kujifunza kuyataja na kuyatambua.
 • Anaweza kuainisha picha za watu, wanyama, chakula, usafiri n.k.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 4

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anacheza na wenzake michezo ya kuigiza-baba na mama.
 • Anaweza kufanya maongezi na wewe.
 • Anashirikiana na kumpa rafiki yake nafasi ya kuchezea midoli yake.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Ameweza kuelewa uhusiano wa wingi wa kitu, namba na vipimo.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Jasiri katika uwezo wa kufanya kitu.
 • Anapenda kutumia muda wake na mama na baba.