Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 3

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anajifunza maneno mapya haraka.
 • Amejifunza kazi za ndani ndogo ndogo kama kurudisha midoli yake.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anaweza kujizuia haja kubwa na ndogo.
 • Anaruka urefu mfupi.
 • Anatoa msaada ukiwa unamuogesha.

Mwanao anaweza kuwa hodari katika (watoto wachache wanaweza)

 • Anatengeneza marafiki wenye vitu vinavyofanana.
 • Anatumia lugha sahihi muda mwingi.
 • Anaweza kuhesabu mpaka kumi.
 • Anabeba kinywaji bila kumwaga.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 2

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anapanda ngazi kwa uangalifu.
 • Anachora maumbo vizuri kwa penseli.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anaweza kubeba vitu vidogo, bado anahitaji msaada kufunga kamba za viatu na vifungo.
 • Anapenda kucheza na wenzake.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anabeba kinywaji bila kumwaga
 • Kudaka mpira.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Mwezi 1

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anazunguka haraka zaidi.
 • Anajua namba moja na mbili.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anakula mwenyewe.
 • Anaweza kuvaa na kuvua koti.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kuruka, kukimbia na kupanda ameweza kufuzu.
 • Anaelewa uelekeo unapomuelekeza.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanaweza)

 • Anapata na wenzake vizuri kuliko hapo awali
 • Anashirikiana midoli yake na wenzake
 • Anaelewa wimbi kubwa la hisia ikiwemo hasira, furaha, woga na huzuni

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanaweza)

 • Anakula mwenyewe
 • Anaweza kutaja jina la maumbo na rangi

Mwanao anaweza kuwa hodari katika (watoto wachache wanaweza)

 • Kuruka, kukimbia na kupanda ameweza kufuzu

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 11

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kudhibiti usogeaji wa viungo vyake.
 • Anaelewa vizuri maana ya “yangu” “yake”.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanazifikia)

 • Uwezo wake wa kuona umeimarika.
 • Ni rahisi kumuacha nyumbani bila kusumbua.

Mwanao anaweza kuwa hodari katika(watoto wachache wanazifikia)

 • Anaruka kwa mguu mmoja.
 • Anachora duara.
 • Anavaa bila msaada.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 10

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaonyesha huruma kwa wenzake.
 • Matumizi ya neno HAPANA katika maombi yako.
 • Anaweza kuongea sentensi nzima.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanazifikia)

 • Utambuzi wa herufi vizuri.
 • Anaanza kupendelea chakula aina moja

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anachagua sana, na kuonyesha kuridhishwa na kitu au kutoridhishwa.
 • Kushika lugha zaidi ya moja.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 9

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kutumia choo vizuri na kukojoa kitandani mara kwa mara.
 • Anaelezea na kutaja anachokiona kwenye picha.
 • Analala unono na kusahau uoga wa usiku.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anafuzu kuweka kitu sehemu moja.
 • Anaelewa ombi mfano niletee kikombe mezani.
 • Anatafuta kusifiwa na kuruhusiwa kufanya kitu.
 • Anaongea na kueleweka mda mwingi.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kujisaidia mwenyewe mchana.
 • Anaonyesha aina nyingi za hisia

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 8

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kuhesabu.
 • Anatofautisha rangi tofauti.
 • Anajifunza kusoma herufi.
 • Anacheza na kujumuika na wazazi.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Muoga usiku kulala mwenyewe lakini atashinda uoga huu.
 • Anatengeneza marafiki

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Muelewa wa hadithi na anaweza kuitikia maongezi.
 • Anaweza kutumia choo mchana na usiku vizuri.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 7

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anagundua maumbo tofauti kama duara
 • Shahuku inaongezeka
 • Aibu inaongezeka

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anaweza kuvaa baadhi ya nguo kama shati.
 • Anaweza kusimama na miguu moja na kisha mwingine.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anauliza maswali mengi kama “kwanini ndege zinapita juu ya nyumba?” au “watoto wanatoka wapi”

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 2 na Miezi 6

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaongea sentensi fupi ya kueleweka nyenye maneno 3-4.
 • Anaosha vyombo na wewe au dada yake.
 • Anaweza kuruka na miguu yote miwili.
 • Anapanga vitu kwa ukubwa na rangi.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anapenda kucheza na rafiki zake
 • Yuko tayari kufundishwa kujisaidia

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Anaweza kuendesha baiskeli za watoto zenye magurudumu matatu.