Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 9

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Ataanza kutoa milio inayotokana na mjumuisho wa silabi.
 • Anajivuta asimame na kukaa.
 • Anagonga, tupa na kudondosha vitu.
 • Anajitahidi kushika kijiko unapomlisha.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanazifikia)

 • Mtoto wako anazunguka kwa kushika vitu kama samani.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Mtoto ataanza kuongea na kunong’ona maneno mengi na kuiga milio na sauti tofauti hasa kipindi hichi anapokaribia kuongea.
 • Kutoa sauti tofauti kama “mamamama” and “bababababa”
 • Anapenda kucheza mchezo wa kujificha “peek-a-boo”

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 8

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anakaa bila msaada
 • Anaita mama au baba au wazazi wote.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kutambaa vizuri.
 • Kusimama kwa kushika vitu

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Ataanza tabia ya kushika kitu kwa nguvu hasa kwa kutumia kidole gumba na kidole cha katikati.
 • Ataonyesha ishara akitaka kitu.
 • Kusimama kwa kushika vitu na kuzunguka sana.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 7

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anafikia vitu kwa kasi ya haraka.
 • Ataanza kutoa sauti kama anaongea.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kutambaa kwenda mbele.
 • Kuokota kitu kwa mkono mmoja na kukisafirisha mkono mwingine.
 • Kukaa bila msaada.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kusimama kwa kushika kitu
 • Kuaga kwaheri.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 6

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Ataanza kutazama nyimbo za watoto

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanaweza)

 • Katika mwezi huu wa sita mwanao ataweza kufikia hatua kubwa za ukuaji kama kujisogeza na tumbo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kuelewa maneno rahisi.
 • Kuitikia unapomuita jina lake.
 • Kutamka silabu moja moja kama ma-ma

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 5

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kutofautisha rangi kuu.
 • Atajiviringisha mpaka atalala na mgongo kama ulimlaza kwa tumbo.
 • Anajifurahisha mwenyewe kwa kucheza na miguu na mikono

Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanaweza)

 • Mtoto atageuka kuelekea sehemu sauti mpya inapotoka.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kukaa (kuketi) bila msaada wako.
 • Kujigeuza akalala na tumbo kama ulimlaza kwa tumbo.
 • Kuweka vitu mdomoni
 • Anaonyesha dalili za kuogopa watu wapya.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 4

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anavutiwa na mfumo wa vitu.
 • Anataka kushika kila kitu na kuweka mdomoni.
 • Ameanza kulia kwa sauti nyororo.
 • Anajitahidi kupata usikivu wako
 • Ataigiza baadhi ya sura utakazomuonyesha

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Mwanao ataanza kujiviringisha,kuwa makini usimuache kitandani mwenyewe.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kuota jino lake la kwanza
 • Kushika chupa yake ukiwa unamlisha.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 3

Hisia za mtoto zitaanza kukua, anaweza kuanza kutumia milio tofauti wakati wa kulia ili kukujulisha nini anataka (anahisi) na kugeuza kichwa chake upande wa pili kuonyesha amechoshwa.

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaweza kutofautisha sura yako na sura za wengine.
 • Ataanza kugeuza kichwa upande wa pili kuonyesha kuchoka au kukerwa na jambo.
 • Atafuatilia kitu kinachosogea kwa macho yake.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kulia tofauti kwa hitaji tofauti-njaa, kubadilishwa nepi, maumivu n.k.
 • Atafungua na kufunga mikono yake.
 • Atafurahi kucheza na watu wengine, atalia pale mtu atakapoacha kucheza nae.
 • Mtoto atagundua sauti yako.
 • Atatengeza viputo na mate yake na kupasua.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kugeuza kichwa upande sauti inapotokea
 • Kujiviringisha na kulala na mgongo kama ulimlaza kwa tumbo.
 • Kutanisha mikono yake na kushika mdoli.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 2

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaanza kutoa sauti, milio ya kitoto na minong’ono.
 • Ataanza kufuatilia vitu kwa macho na kuwagundua watu aliowazoea kwa mbali.
 • Anagundua mkono wake.
 • Atanyanyua kichwa chake juu kwa muda mfupi.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kutabasamu,kucheka
 • Kuinua kichwa digrii 45.
 • Kusogeza miguu na mikono taratibu.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kujiinua unapomlaza tumboni kwako.
 • Kuhimili uzito wake kwenye miguu yake
 • Kukihimili kichwa chake kwa uimara
 • Atajibembeleza mwenyewe kwa kuweka mkono mdomoni.

Ataanza kunung’unika na kusumbua pale anapochoshwa na kitu au mdoli.

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwezi 1

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Atanyanyua kichwa chake ukimlaza tumboni kwako.
 • Ana mwitikio katika sauti atakayosikia.
 • Kuzitambua sura na kushangaa.
 • Ataona rangi nyeusi na nyeupe.
 • Anageuza kichwa kuelekea mwanga unapotokea.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Anafuata muelekeo wa vitu.
 • Anatoa sauti za “ooh” na “ah’’.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kucheka
 • Kunyanyua kichwa digrii 45.