Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 2

Wakati huu mtoto ana miezi miwili na uwezo wake wa kuhisi unaongezeka mshirikishe sauti na vitu vya kuhisi. Anaweza kuhisi vitu vifuatavyo:

Vitu vinavyotoa sauti: utamuona mtoto anaanza kuitikia kelele, sauti tofauti za mziki, ngoma na sauti zinazotoka jikoni nk.

  • Anza kutengeneza sauti mbalimbali, mtoto ataanza kuzizoea.
  • Unaweza kutengeneza karatasi au midoli inayotoa kelele na mwanao ataanza kuifuatia kwa haraka.

Michezo ya kuruka: katika mwezi wa pili mtoto atafurahia michezo ya kusogea huku akizidi kuimarika.

  • Fanya hivi kwa tahadhari, kwanza kaa chini
  • Lala chini na uanze kupishanisha miguu juu chini
  • Sema “juu, chini” kama ambavyo mtoto anatazama
  • Furahia haya

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Mwezi 1

Wakati huu mtoto anakua huru na makini sana katika mazingira nayomzunguka kwahivyo kuboresha mazungumzo kati yenu kuna msaidia kuendelea katika kutambua maneno. Pia wakati huu pua zake zitaendelea kuboreka. Kipindi hichi mtoto anajifunza yafuatayo ikiwa utajihusisha naye sana katika mazungumzo kwa kutumia vitu vifuatavyo:

Mazungumzo kwa bomba

Ni rahisi na nzuri.

  • Unaweza kutengeneza mfano wa bomba karatasi au plastic
  • Sehemu ya kwanza ya bomba weka kwenye sikio lake na sehemu ya mwisho jaribu kuzungumza taratibu
  • Jaribu kumuambia maneno kama “habari mtoto”
  • Anza kuongea kwa kumuigiza mtoto ili aweze kuzoea sauti yako

Midoli ya kuchezea

Utahitajika kumtafutia mtoto midoli, unaweza kutengeneza nyumbani au kununua sokoni

  • Ichukue taratibu na kuipeleka eneo alilopo mtoto
  • Subiri hadi avutiwe kuitazama
  • Itambulishe midoli kwa majina rahisi kama vile “habari naitwa panya Jerry”
  • Ifanye midoli kuzungumza katika hali ya utani , itamfanya mtoto kufurahia mazungumzo

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto Mchanga

Kipindi hiki kichanga anaanza kutambua vitu vinavyomzunguka, anatazama na kujaribu kuelewa mazingira yanayomzunguka. Wakati huu uwezo wa mtoto wa kuona una kikomo. Anaweza kuona vitu kuanzia inchi 8 hadi 10 kutoka umbali aliopo, kipindi hichi pia uwezo wake unaboreka katika kuhisi, kuona na kutambua sauti. Unaweza kumuandalia vitu kwa ajili ya kuchezea

Vichekecha: watoto wanapenda sana kuchezea vichekecha, sauti zake pia zinamsaidia mtoto katika mfumo wa kuhisi. Unaweza kuanza kwa kuchukua kichekecha kidogo na kufanya yafuatayo kwa ajili ya mtoto:

  • Jaribu kuweka kichekecho katikati ya vidole vya mtoto
  • Ingawa bado ni mdogo kushika ila atahisi uwepo wa kitu.
  • Unaweza pia kutikisa kichekecho taratibu upande mmoja kwenda mwingine, itamsababishia kupepesa macho kufuatia mlio wa kichekecho.
  • Jaribu usitikise kwa sauti kubwa itamfanya mtoto kuogopa.

Maongezi ya furaha: unahitaji kuwa na mawasiliano ya karibu sana na kichanga

  • Wakati huu anajitahidi kuelewa vitu na sauti zinazomzunguka.
  • Atajaribu pia kuwasiliana na wengine kwa sauti za ishara.
  • Atajaribu kuzungumza kwa furaha na mtoto mwingine.
  • Jitahidi kufanya vitu vya kumchekesha na kumfurahisha kwa sauti na sura za kuchekesha vitamsaidia kuzid kutambua vitu