Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 8

Sasa mtoto wako anajaribu kusimama, ataimarika mikono yake na macho kipindi hiki. Unaweza kumsaidia kwa kumpatia vishughuli vichache ili kuboresha uwezo wake.

Michezo ya kurusha miguu

Zoezi hili litamsaidia vema mtoto katika uimarikaji wake

  • Mshikilie mtoto kwa upande wa nyuma , mkono mmoja ukimshika kifuani mwake na wa pili ukimsaidia kwa chini.
  • Weka mpira mbele ya miguu yake
  • Sasa msaidie kupiga mpira huku ukiwa umemshikilia.
  • Sema “piga” kila wakati na atafanya hivo.

Kelele

Mwanao atapenda kupiga kelele. Hivyo mpe vitu vya kumsaidia kufanya hivo

  • Unaweza kumpatia sahani na kijiko ikiwa umemuweka katika kiti chake cha kukalia na kumfanyia sauti anayoitaka.
  • Mwanao sasa atataka kutengeneza sauti kama hiyo kwa mikono yake mwenyewe.

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 7

Mtoto wako sasa anasikia na kuzingatia zaidi. Uwezo wake wa kusikia na kuzingatia unachomwambia umeimarika sana na utaendelea kipindi ambacho unamtamkia maneno na kumtambulisha baadhi ya vitu

Vitu vya hadithi

Wakati wa hadithi ni wakati pendwa sana kwa watoto.

  • Nunua au tengeneza vitu vya hadithi kama vile wanyama na miti
  • Tengeneza hadithi kuhusu vitu hivyo, ukiwa umemkabidhi mwanao
  • Mtazame kama atazingatia hadithi na picha ya vitu ulivyomkabidhi kwa pamoja,au kuitikia kwa sauti

Michezo ya kwenye maji

Watoto wanapenda kucheza kwenye maji,angalia jinsi inavyofurahishwa

  • Tumia beseni safi katika zoezi hili.
  • Weka kiasi cha maji katika beseni.
  • Chezea maji kwa kuyapiga piga kumfanya mwanao aone yanavyoruka nje.
  • Mfanye mwanao afanye sawa na wewe.
  • Zoezi hili litamfanya mwanao aimarike viungo vya mwili wake na anaweza kuleta athari.

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 6

Huu ni muda ambao mtoto anapendelea zaidi michezo ya kuchekesha na kupiga, atapata ujuzi mpya na kujihusisha nao.

Albamu ya picha

Mtoto wako ataanza kugundua baadhi ya vitu, rangi na maumbo katika shughuli zake.

  • Tengeneza albamu ya rangi yenye picha za ndugu na marafiki ambao mtoto anaweza kuwatambua.
  • Unaweza kumtengenea mtoto kitabu cha kuandikia pia.
  • Kaa na mwanao ukimuonesha albamu kila siku.
  • Kwa njia hii mtoto atazoea kupitia picha yeye mwenyewe

Jenga tofali

Huu ni wakati ambao mwanao ameimarika macho katika kutazama umbo, huu ni muda mzuri wa kuanza mchezo wa tofali

  • Kwa sasa mtoto wako ana ujuzi mzuri wa kuelewa vitu, na ataanza kubeba, kusogeza na kuangusha vitu.
  • Shiriki kwenye mchezo hadi pale mtoto atakapozoea kufanya hivyo mwenyewe.

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 5

Wakati huu mtoto wako atapendelea zaidi mchezo wa kujificha

Ficha mdoli

Hakikisha unakuwa na mwanao wakati wote wa mchezo pia unaweza kutengeneza eneo kwa boksi au karatasi ili kuzuia mtoto asijiumize

  • Weka mdoli pendwa wa mwanao katika boksi
  • Kisha weka boksi lenye mdoli katika boksi lingine, kisha kwenye boksi kubwa zaidi.
  • Muulize mtoto “mdoli wako upo wapi” na umuonyeshe kwenye boksi.
  • Mtazame mtoto anapojaribu kufungua boksi moja baada ya lingine.
  • Muulize mwanao “mdoli wako uko wapi”mda wote maboksi yamefunguliwa
  • Ona jinsi mwanao atakavyoutoa mdoli uliofichwa

Kuongoza ndege

Huu ni kati ya michezo ya kuvutia zaidi ikiwa utafanya kama mama

  • Wakati huu mtoto atafuata muelekeo wa kijiko wakati unamlisha
  • Cheza mchezo huu na mwanao wakati unampa chakula
  • Tumia kijiko kama ndege na uiongoze taratibu katika muelekeo wa mdomo wa mwanao
  • Wakati anapokea chakula mdomoni sema “ndege imetua”

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 4

Wakati huu mtoto anaendelea katika hatua nyingine ya mawasiliano. Unaweza kucheza naye michezo ya kuingiliana na akashiriki kwa haraka

Kurusha miguu

Mpendwa wako ataupenda mchezo huu

  • Weka kiasi maji inchi 3 hadi 4 kwenye beseni la mtoto.
  • Mkalishe wima kwenye maji kumruhusu aweze kurusha rusha miguu yake kwenye maji
  • Kadri anavyorusha miguu ndivyo jinsi maji yanazidi kumwagika , hii itamfanya kufurahia sana mchezo huu.

Kutambaa

Mchezo huu utasaidia kumpa mtoto ujuzi wa kutosha

  • Katika mwezi wa nne mtoto anapendelea kuanza kusogea.
  • Wakati anajaribu kujivuta muwekee kitu chochote mbele yake mbali kidogo na mikono yake.

Mtazame mtoto anavyojaribu kujivuta mbele kadiri unavyosogea

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 3

Huu ni wakati bora wa kucheza michezo ya simu na mwanao

Mazungumzo kwa simu

  • Mshikishe simu mtoto na uigize kupokea na kuzungumza naye kupitia simu
  • Tengeneza mazungumzo ya mda mfupi kumfanya mtoto aweze kuyapokea
  • Michezo itakua kitu cha kufurahia

Kucheza ngoma

Kucheza ngoma kunafanya kuimarika katika kusikia kwa mtoto

  • Chukua makopo matatu ya plastiki
  • Tumia vijiti au kijiko kupiga ngoma pamoja na mwanao

Hakikisha hii inafanyika chini ya uangalizi wako kumbuka mtoto ni mdogo anaweza kujidhuru na vijiti.

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Miezi 2

Wakati huu mtoto ana miezi miwili na uwezo wake wa kuhisi unaongezeka mshirikishe sauti na vitu vya kuhisi. Anaweza kuhisi vitu vifuatavyo:

Vitu vinavyotoa sauti: utamuona mtoto anaanza kuitikia kelele, sauti tofauti za mziki, ngoma na sauti zinazotoka jikoni nk.

  • Anza kutengeneza sauti mbalimbali, mtoto ataanza kuzizoea.
  • Unaweza kutengeneza karatasi au midoli inayotoa kelele na mwanao ataanza kuifuatia kwa haraka.

Michezo ya kuruka: katika mwezi wa pili mtoto atafurahia michezo ya kusogea huku akizidi kuimarika.

  • Fanya hivi kwa tahadhari, kwanza kaa chini
  • Lala chini na uanze kupishanisha miguu juu chini
  • Sema “juu, chini” kama ambavyo mtoto anatazama
  • Furahia haya

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto wa Mwezi 1

Wakati huu mtoto anakua huru na makini sana katika mazingira nayomzunguka kwahivyo kuboresha mazungumzo kati yenu kuna msaidia kuendelea katika kutambua maneno. Pia wakati huu pua zake zitaendelea kuboreka. Kipindi hichi mtoto anajifunza yafuatayo ikiwa utajihusisha naye sana katika mazungumzo kwa kutumia vitu vifuatavyo:

Mazungumzo kwa bomba

Ni rahisi na nzuri.

  • Unaweza kutengeneza mfano wa bomba karatasi au plastic
  • Sehemu ya kwanza ya bomba weka kwenye sikio lake na sehemu ya mwisho jaribu kuzungumza taratibu
  • Jaribu kumuambia maneno kama “habari mtoto”
  • Anza kuongea kwa kumuigiza mtoto ili aweze kuzoea sauti yako

Midoli ya kuchezea

Utahitajika kumtafutia mtoto midoli, unaweza kutengeneza nyumbani au kununua sokoni

  • Ichukue taratibu na kuipeleka eneo alilopo mtoto
  • Subiri hadi avutiwe kuitazama
  • Itambulishe midoli kwa majina rahisi kama vile “habari naitwa panya Jerry”
  • Ifanye midoli kuzungumza katika hali ya utani , itamfanya mtoto kufurahia mazungumzo

Michezo ya Kusaidia Ukuaji wa Mtoto Mchanga

Kipindi hiki kichanga anaanza kutambua vitu vinavyomzunguka, anatazama na kujaribu kuelewa mazingira yanayomzunguka. Wakati huu uwezo wa mtoto wa kuona una kikomo. Anaweza kuona vitu kuanzia inchi 8 hadi 10 kutoka umbali aliopo, kipindi hichi pia uwezo wake unaboreka katika kuhisi, kuona na kutambua sauti. Unaweza kumuandalia vitu kwa ajili ya kuchezea

Vichekecha: watoto wanapenda sana kuchezea vichekecha, sauti zake pia zinamsaidia mtoto katika mfumo wa kuhisi. Unaweza kuanza kwa kuchukua kichekecha kidogo na kufanya yafuatayo kwa ajili ya mtoto:

  • Jaribu kuweka kichekecho katikati ya vidole vya mtoto
  • Ingawa bado ni mdogo kushika ila atahisi uwepo wa kitu.
  • Unaweza pia kutikisa kichekecho taratibu upande mmoja kwenda mwingine, itamsababishia kupepesa macho kufuatia mlio wa kichekecho.
  • Jaribu usitikise kwa sauti kubwa itamfanya mtoto kuogopa.

Maongezi ya furaha: unahitaji kuwa na mawasiliano ya karibu sana na kichanga

  • Wakati huu anajitahidi kuelewa vitu na sauti zinazomzunguka.
  • Atajaribu pia kuwasiliana na wengine kwa sauti za ishara.
  • Atajaribu kuzungumza kwa furaha na mtoto mwingine.
  • Jitahidi kufanya vitu vya kumchekesha na kumfurahisha kwa sauti na sura za kuchekesha vitamsaidia kuzid kutambua vitu

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 3 na Miezi 8

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikiz)

  • Anapenda kuunda na ufundi.
  • Anapenda kuzunguka mpaka apate kizungzungu, kuruka sehemu ndefu na kudondoka ghafla (kuporomoka).

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

  • Anapendelea michezo yenye kanuni za kufuata.
  • Anapenda kuomba kibali /ruhusa.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Anatumia maneno na sentensi alizokariri
  • Anaanza kuainisha na kutenga hisia na majibu ya watu