Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 4 na Miezi 2 – (Miezi 50)

Jinsi mtoto wako anavyokua

“Ninaweza kufanya mwenyewe!” mtoto wako anakuambia wakati unamvalisha nguo asubuhi (au wakati anapiga meno mswaki, akisaidia kupanga meza, au ukifanya chochote). Kadiri uwezo wa mtoto wako wa kimota unavyokua, anaweza akawa anasukuma mikono yako mbali kadiri unapotaka kumsaidia kufanya jambo kwani anataka kufanya kila kutu mwenyewe. Hii inaweza kukufanya ukose uvumilivu wa kusubiri, lakini inashauriwa usimuingilie mtoto wako mapema na kutoa msaada kwani yupo kwenye hatua muhimu za mwanzo za kujifunza vitu mbali mbali na kujitegemea.

Katika miaka minne mtoto wako anatakiwa awe anaweza kuvaa nguo mwenyewe, japokuwa anaweza bado akawa anasumbuliwa na zipu na vifungo. Kurahisisha na kumfundisha hatua hii haraka jaribu kuchanganya na kumpa pia nguo ambazo ni rahisi kuvaa, kama suruali zenye mpira wa kuvutika kiunoni au viatu vya kudumbukiza.

Kitu kimojawapo ambacho lazima uendelee kuwa unamsimamia ni wakati wa kupiga meno mswaki. Mtoto wa miaka minne bado hajawa na muungano mzuri wa matendo kuweza kusafisha meno yake kwa ufanisi. Muache asafishe mwenyewe kwa muda halafu uingilie kati na kumsaidia kumalizia hatua za mwisho.

Maisha yako wakati huu.

Hakikisha familia yako yote inatenga muda kwa ajili ya kupata kifungua kinywa. Ni mlo muhimu kuliko milo yote ya siku lakini ndio mlo ambao haupewi kipaumbele. Sababu zinaweza kuwa labda wazazi wapo na majukumu mengi na watoto kutoamka wakiwa na njaa.

Ulaji wa kifungua kinywa ni muhimu sana kwa mtoto wako kwani ubongo utahitaji chakula baada ya kuwa umelala usiku kucha. Hii itamsaidia mtoto wako pia kuwa na usikivu, tabia nzuri na pia kuwa na maendeleo mazuri shuleni bila kusahau kupungua kwa uwezekano wa kupata unene uliopindukia. Utajisikia vizuri na kuwa na uwezo wa kula bora zaidi katika siku kama ukila kifungua kinywa vizuri asubuhi.

Unaweza ukaandaa chakula cha asubuhi kwa ajili ya kifungua kinywa tangu usiku mmoja kabla, ili kupunguza ugumu wa kuandaa kila kitu asubuhi husika.

Mtoto Miaka 4 na Mwezi 1 – (Miezi 49)

Jinsi mtoto wako anavyokua.

“Moja, mbili”, tatu”, mtoto wako anasema akiwa anapanga vitu vyake vya kuchezea. Na mpaka sasa, inawezekana anajua namba ya mwisho atakayofikia ndio kiwango cha vitu vya kuchezea aluvyonavyo. Kitu ambacho anaweza asiwe anajua kwa sasa ni kwamba hata ukivipangilia tofauti vitu vyake vya kuchezea akivihesabu kwa mara nyingine idadi yake itakuwa ile ile. Unaweza ukavipanga mbali mbali zaidi na ukamuuliza akuambie idadi yake. Anaweza akakuambia ana vitu vinne vya kuchezea badala ya vitatu kwa sababu sasa  hivi vipo mbali mbali zaidi.

 

Watoto wanaokaribia kuanza shule wanaelewa kuhusu idadi kulingana na muonekano wa vitu husika. Kama kifurushi kimoja cha vitu vya kuchezea ni kirefu kuliko kingine wataamini kina idadi ya vitu vingi kuliko kile kifurushi kifupi. Hataweza kuwa na uelewa kwamba urefu wa kifurushi sio lazima umaanishe wingi wa vitu ila inawezekana ni vitu vichache ila ni vikubwa zaidi. Hii ni kwa sababu wanazingatia zaidi muonekano wa vitu kuliko uelewa wa idadi, ambao ni uwezo mkubwa zaidi kwa umri wake.

 

Majina ya watoto yana umuhimu sana kwao. Kwa uhalisia jina la mtoto wako inawezekana ndio neno la kwanza atakalojifunza na kulisoma. Wakati fulani akishafikisha umri wa miaka minne anaweza kuanza kuonesha nia ya kuliandika jina lake pia. Wakati fulani ataanza kutambua kuwa baadhi ya herufi zinahusika na jina lake au ni “herufi zake”. Msaidie kwa kuliandika jina lake kwa herufi kubwa na zinazoonekana kwenye karatasi kubwa. Muache afuatilie kwa kidole au kalamu mkitamka kila herufi kwa sauti pamoja.

 

Maisha yako wakati huu

Sikukuu ya kuzaliwa ya mtoto wako iliyopita inaweza ikawa imesababisha kuongezeka kwa midoli au vitu vya kuchezea vya mtoto wako kwenye nyumba. Ni wakati wa kuanza kupunguza na kupanga vitu vya mtoto wako vya kuchezea. Unaweza ukavipunguza na kuondoa vile vitu ambavyo amechoka kuvichezea au alikuwa anavichezea akiwa na umri mdogo zaidi na kuviweka stoo au kuvitupa kama vimechakaa sana. Wakati mwingine unaweza pia ukavigawa kwa ndugu, jamaa au rafiki wenye mtoto mwenye umri husika wa vifaa unavyotaka kupunguza. Ukumbuke kuwa kama utamuuliza mtoto wako kama anahitaji bado kuendelea kuchezea au kutumia kifaa fulani, bado atasema ndiyo kwani ni vigumu sana kwa watoto kuruhusu kutupwa au kuchukuliwa kwa vitu vyao.

 

Inashauriwa pia kama mtoto ana vitu vingi vya kuchezea ni bora kuficha baadhi ya vitu na kuwa unavitoa na kumpa achezee kila baada ya muda fulani. Mtoto mwenye vitu vingi sana vya kuchezea kwa wakati mmoja inamnyima mtoto umakini wa kutulia na kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu. Kuwa na vitu vichache vya kuchezea kunaleta uelewa wa upangiliaji na inapunguza wasiwasi kwako na kwa mtoto wako.

Mtoto Miaka 4 – (Miezi 48)

Jinsi mtoto anavyokua.

Miaka minne ni umri wa kusisimua,wenye nguvu na wakuwasiliana na watu zaidi. Mtoto wako ana ujasiri akiwa anaongea, kimbia, chora na kutengeneza vitu, ujuzi wa mtoto wako uko tayari kukua zaidi. Mwanao atafurahia marafiki walio watu wazima na watoto wa miaka yote kuanzia watoto wadogo mpaka wazee .

Je,mwanao anakatishwa tama na baadhi ya majukumu kama kufunga vifungo vya shati lake? Inaleta maana kwa hatua hii: mikono ya mtoto wako kwa sasa ni mizuri kwa kurusha mpira zaidi kuliko kufunga kamba za viatu, kwa sababu uwezo wa ubongo wake kumuwezesha kufanya hivi haujakua vizuri bado. Uvumilivu bado sio kitu rahisi kwake.

Mtoto wako ataanza kuonyesha kujali au kuwatuliza wengine wanapokuwa na huzuni au hasira. Uwezo wake wa kuelewa hisia kupitia maneno au matendo unakua. Sasa misamiati yake inakua, anaweza onyesha kujali kwa maneno na kuonyesha hisia zake mwenyewe.

Maisha yako

Uwezo wa mwanao kujumuika na wenzake na kuongea nao utamfanya apate marafiki wengi. Mwanao ataalikwa kwenye sherehe nyingi za kuzaliwa na wewe kupata muda wa kutosha kuongea na kujumuika na rafiki zako. Anza kuzoea maana hali hii itaendelea kadiri mwanao anavyokua.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 11 – (Miezi 47)

Jinsi mtoto anavyokua

Zawadi nzuri unayoweza mpatia mwanao sasa hivi, ni boksi kubwa au chocho kitakachokusidia kutengeneza gari, nyumba au roketi. Inaweza sisimua ujuzi,hisia na ustadi zidi ya midoli ya kieletroniki.

Kucheza kwa kuigiza (kimama-mama, kidaktari au kipolisi) kunafanyika sana mtoto akiwa na miaka mitatu.

Watoto wanajifunza kwa kuwaza na kufanya. Wanapoigiza kuwa polisi au mzazi wanapata uhuru wa kuchunguza  kasi ulimwengu wanaoishi. Wanakua na mamlaka. Wanaweza elezea hisia, wanajifunza kujadiliana na kutatua matatizo(kama jinsi gani ya kupika au kuwakamata watu wabaya). Wanajifunza kuelewa matatizo ya watu na kuwaonea huruma.

Maisha yako sasa

Kuwa karibu na mtoto wa miaka mitatu sio jambo la mchezo. Pale mambo yanapokua mengi na kuchanganyikiwa jaribu kupumua, pumua kwanguvu ndani kisha hesabu mpaka tano, bana pumzi yako na hesabu mpaka saba alafu pumua taratibu kwa kuhesabu mpaka nane. Rudia mara nne au tano(funga macho kama unaweza), taratibu utatulia.

Mtoto Miaka 3 Miezi 10 – (Miezi 46)

Jinsi mtoto anavyokua

Kumbukumbu za watoto wa miaka mitatu bado ni ndogo hasa kama ni ya jambo ambalo linawafanya wajisikie vibaya. Wakati huu usishtushwe mwanao atakapo danganya au kukataa jambo alilofanya. Kama jambo limetokea masaa machache yaliyopita anaweza asikumbuke kabisa.

Au kama atakumbuka ila akaelewa halikua jambo zuri. Atajihakikishia na kukuhakikishia hana hatia. Watoto hawawezi kuvumilia kuumia moyo,hivyo watajitahidi kuhamisha tuhuma kwa mtu mwingine.

Tenga muda wa mtoto kujifurahisha mwenyewe badala ya kumfululizia michezo uliyopanga ya kufanya bila kumuacha muda wake wa kufanya yake.

Maisha yako sasa

Unaweza ukawa umesikia ushauri unaosema msimamo unachangia linapokuja swala la nidhamu. Ushauri huu ni kweli.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 9 – (Miezi 45)

Jinsi mtoto wanavyokua

Je,kuna sauti nzuri kama mtoto wako akiwa anacheka? Ni sauti nzuri hasa kama wewe ndo unamchekesha. Watoto wa miaka mitatu wanapenda vichekesho vinavyoonekana. Ni wakati mzuri wa kufanya vituko vichache kumfanya mwanao acheke. Kwa mfano unaweza kuvaa sweta lako nje ndani au kuvaa viatu mikononi. Vitu vya kutokea bila kujua vinaweza mfanya acheke zaidi.

Vitu vya kijinga vinaweza kuwa njia ya kumfundisha mtoto, chukua herufi au namba zipange kwa makosa anaweza kukucheka kwa ujinga wako huo, na kuanza kuzipanga vizuri kama anazifahamu. Yote haya yakiwa yanaendelea mwanao atakua mwenye kucheka sana hii ni nzuri kwake.

Ikiwa mwanao hawezi kuruka, kukimbia au kusimama na mguu mmoja,usijali. Mfumo wa kuratibu mwili wa mtoto unatofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine. Baadhi ya watoto wako tayari kujaribu tangu awali wakati wengine wanapendelea kukaa pembeni na kuangalia mpaka wakiwa tayari kufanya jambo kubwa.

Maisha yako sasa

Kwa wazazi wengi desturi ya kuchukua kumbukumbu za picha za mtoto alipokua mdogo ilikua kubwa,ila kadiri anavyokua hali ile inapungua. Utagundua kuwa kumbukumbu nzuri za mwanao sio picha zilizopigwa vizuri na kuwekwa ukutani, ila matukio ya kila mda na siku. Hivyo basi weka simu au kamera karibu na wewe mda wowote uwe tayari kuchukua kumbukumbu ya tukio fulani ikiwa ni bafuni, wakati wa kulala, wakati wa kula au hata wakati wa kucheza.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 8 – (Miezi 44)

Jinsi mtoto anavyokua

Maswali mengi yanakuja hasa mwanao anapokaribia miaka minne. Maswali kama ni sawa yeye kutumia kompyuta? Kuna siku ambayo hatakunywa uji?

Simu za kupapasa au kompyuta zinaweza kuwa njia nzuri za kujifunza lakini pia sio nyenzo za lazima katika umri huu. Kama mwanao anapendelea na yuko tayari kujifunza kupitia kompyuta na simu tafuta michezo mizuri na “app” za simu (Ubongo Kids – Akili na mimi) zenye michezo ya watoto kukuza ubunifu wake au hesabu na kusoma,kuhesabu,kuzitambua herufi na kuimba pia.

Maisha yako sasa

Nyumba yako kupangiliwa ni vigumu hasa kama unakaa na mtoto mdogo wa miaka mitatu, unaweza kuchanganyikiwa ukifikiria unadhifu wa nyumba sasa. Unaweza panga nyumba yako na muda huohuo mwanao kuvuruga. Polepole mwanao ataweza kurudisha midoli yake kwenye boksi na vitu mahali alipovikuta baada ya kutumia, lakini ni baada ya kuanza kwenda shule.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 7 – (Miezi 43)

Jinsi mwanao anavyokua

Watoto wengi katika huu ustadi wao kwenye michezo unakua. Atapenda kukuonyesha akiruka, akisimama na mguu mmoja,akiendesha baiskeli. Kukuza kipaji chake ni vizuri kila siku apate lisaa limoja la kucheza.

Miaka mitatu mwanao anaweza elewa lini na ilichukua muda gani kufanya. Maneno kama jana na kesho hayaelewi.

Mtoto wako anaweza kuelewa siku za wiki, hivyo mtajie pale unapopata muda. Kwa mfano mkumbushe kuwa jumamosi na jumapili hakuna shule wala kazi na jumapili ni siku ya kanisani na ijumaa msikitini.

Maisha yako sasa

Mtoto wako akionyesha hasira, sio amechoka. Wakati mwingine inaweza kuwa njaa, ugonjwa au kukatishwa tamaa baada ya kushindwa kufanya kitu. Tambua kuwa hisia zake bado duni hasa pale anapotaka kukubaliana na hali au kitu.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 6 – (Miezi 42)

Jinsi mtoto wako anavyokua

Mchakato wa mwanao kujifunza kutofautisha ukweli na ndoto ni wa polepole. Mwaka huu utakua mwaka wa kuvutia kwake kwasababu kila anachowaza kichwani kwake anajua ni ukweli. Ataanza kutoa majukumu kwa vifaa au watu ambapo haiwezekani ila kwa mwanao ni sawa. Mtoto wako ataamini barua zinapaa kutoka kwa aliyetuma mpaka nyumbani. Atafikiri anaweza ongea na ndege na kuna binadamu kwenye mwezi. Itachukua muda mwanao kugundua kuwa vitu vingi anavyofikiria sio vya ukweli mpaka miaka nane.

Maisha yako sasa

Una shida wakati wa kulala? Ratiba yako ya kulala imeharibiwa kwa miaka miwili iliyopita, ni vizuri kuandaa na kurudisha mazingira na tabia nzuri ya kulala. Kwanza hakikisha chumba chako kina giza, hakikisha hakuna komputa au televisheni chumbani kwako(wataalamu wa mambo ya usingizi wanashauri hivyo). Kuna mambo mengi ya kufanya baada ya mwanao kulala kama kuangalia mitandao ya kijamii au kuangalia televisheni, usipoteze muda mwingi kukimbizana nayo, kumbuka mwanao anaamka mapema sana hivyo ni vizuri kulala mapema ili uamke na nguvu nyingi.

Mtoto Miaka 3 na Miezi 5 – (Miezi 41)

Jinsi mtoto anavyokua

Una sababu nzuri ya kujivunia na mwanao mwenye miaka mitati na miezi sita sasa. Uwezo wake wa kusaidia kazi ndogondogo, kukuza lugha yake na mawazo vinaimarika pia, muda huu atajitahidi kuandika jina lake mwenyewe.

Inafurahisha kuanza kuona herufi zinaumbika vizuri. Kuandika ni moja ya hatua ya ukuaji inayotofautiana mtoto mmoja na mwingine. Hivyo, ondoa shaka kama mwanao hana hamu ya kuandika.

Unaweza kumuhamasisha kwa kuweka chaki au karatasi na penseli mahali anapoweza kufikia. Pia unaweza tumia sukari au unga wakati mkiwa jikoni na kuweka kwenye sinia, kasha muonyeshe jinsi ya kuunda maneno.

Watoto katika umri huu wanagundua na kuiga sauti mbalimbali wanazozisikia kutoka kwako au baba yake, au katuni wanazoangalia. Utaweza kumuona akiongea na midoli yake huku akiiga tukio aliloliona hapo awali. Pia mtoto anaweza kugundua kuwa watu wazima wanaongea tofauti kulingana na mtu anayeongea nae, anaweza gundua kuwa unaongea tofauti pale unapoongea na mama yako na unaoongea tofauti unapozungumza na mwajiri wako.

Maisha yako sasa

Baadhi ya wakati hata wazazi wazuri,wenye subira,wacheshi,wanataka kupiga kelele! Kumlea mtoto kunachosha hasa pale usingizi unapokua finyu. Jaribu kutoka na kufanya manunuzi,kutembea mwenyewe ,sikiliza muziki unaopenda.