Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mambo ya Kuzingatia Kiafya Kabla ya Kupata Ujauzito

Haya ni mambo ya kuzingatia ukiandaaa mwili wako kiafya kabla ya ujauzito.

Uzazi wa mpango

Kama ulikuwa umechoma sindano ya uzazi wa mpango, inaweza kuchukuwa wiki 12 kwa homoni zile kuondoka mwilini. Halafu miezi mitatu au hata mwaka kwa uwezo wa kupata ujauzito, na kama ulikuwa ukitumia vidonge inaweza kuchukua mpaka miezi sita kwa uwezo wa mzunguko wako kurudia hali ya kawaida.

Hatahivyo kwa baadhi ya nyakati kama ulikuwa ukitumia vidonge vya uzazi wa mpango havita athiri muda wa kupata ujauzito, ongea na mkunga wako kwa maelezo zaidi.

Historia ya matibabu

Hakikisha mkunga wako anajua historia ya matibabu yako hapo nyuma. Kama inawezekana mwambie kuhusu matatizo yeyote ya kiafya ulionayo na yaliyopo ndani ya familia ikiwemo kama ndugu yeyote wa kike alikuwa na matatizo ya ujauzito. Mkunga wako atakujuza juu ya tatizo lolote utakalo kumbana nalo

Ukaguzi wa mlango wa uzazi

Inajulikana pia kama “cervical smere” kipimo hiki sio cha muhimu wakati wa ujauzito ndio maana hufanyika wakati huu kabla ya ujauzito Kama unatakiwa ufanye kipimo hichi mwakani au zaidi, muulize mkunga wako kama unatakiwa uanze kukipata kabla hujaanza kutafuta mtoto.

Kipimo cha damu na mkojo.

Kipimo hichi kitaangalia kila kitu, ikijumuisha kisukari na anemia, na maambukizi mengine kama yapo. Kipimo hiki hakitatolewa kila mara hivyo ni bora kuongea na mkunga wako.

Kujua tatizo lako mapema ni vyema kwasababu itamsaidia mkunga wako kujua nini kifanyike na kukusaidia vizuri, kwa mfano kama una kisukari  mtoto wako yupo katika hatari ya kupata madhahara mbalimbali, kwahiyo ni vyema kuwa na uangalizi wa karibu kuweza kuangalia kwa kariibu afya yako, ili kuweza kupunguza hatari kwa mwanao.

Jaribu kujua afya yako ya uzazi katika kliniki  na hakikisha unapima maambukizi kama vile UTI, maambukizi ya magonjwa ya ngono kama ulijamiiana bila kutumia kinga.

Pima shinikizo la damu

Shinikizo la damu la kupanda wakati wa ujauzito ni jambo la kawaida, haswa kama una ujauzito mkubwa. Mara nyingi mkunga wako ataangalia atakufanyia kipimo hichi  kila mara ukiwa mjamzito.

Hata hivyo kama tayari ulikuwa na tatizo la shinikizo la damu ni vyema kuchukua kipimo hiki kabla hujapata ujauzito. Hii itawapa nafasi mkunga wako na daktari wako kujua namna gani watakusaidia utakapokuwa mjamzito.

Uzito wenye afya

Kuwa na uzito mkubwa na uzito duni unaweza kuzuia uwezo wako wa kupata ujauzito, au pia unaweza kusababisha matatizo wakati wa ujauzito kwako na kwa mtoto, kwa kawaida lazima uwe na BMI ya 19-25

Kama maisha yako ni magumu  na hakuna msaada, mkunga wako atakua tayari kukupa ushauri, kama BMI yako ni kubwa au ndogo  anaweza akakuelekeza vyakula vya kula ili kupata uzito unaotakiwa kabla ya kupata ujauzito.

Chanjo

Hakikisha kwamba upo kwa wakati katika kupata chanjo kwani huweza kumsaidia mtoto pamoja na wewe. Kuna baadhi ya chanjo ni bora uzipate mapema kabla ya kujapata ujauzito.

Acha kuvuta sigara.

Uvutaji wa sigara unaweza kuleta matatizo kwa mtoto unaongeza pia nafasi ya mtoto kupata matatizo kama mimba kuharibika, na mtoto kuzaliwa akiwa mfu. Kuacha sigara ni ngumu kwa hiyo itakuwa rahisi kama utapata msaada. Muulize mkunga wako kwa msaada zaidi.

Tiba.

Kama unatumia dawa ya aina yoyote, ongea na mkunga wako kama utaendelea kutumia dawa au la? Au kama unatakiwa kubadilisha, lakini wakati mwingine daktari anaweza kukupa dawa ambayo ni salama zaidi wakati wa ujauzito.

Wakati unaanza kujaribu kupata ujauzito itabidi uanze kuachana na dawa za kununua dirishani kama dawa za kutuliza maumivu ambazo sio salama katika ujauzito wako.

Kipimo cha vina-saba (genetic)

Kama una tatizo la vinasaba kama vile cystic fibrosis, au ugonjwa wa kuzaliwa nao kama vile upungufu wa seli nyekundu za damu kwenye damu, unatakiwa ufanye kipimo hichi. Mara nyingi unaweza kupatiwa kipimo ikiwa kuna tatizo ndani ya familia.

Tiba lishe

Mapema uwezavyo anza kutumia tiba lishe ambayo ina (mcg 400) za acidi ya folic kila siku. Endelea kutumia mpaka ukiwa wiki ya 12 ya ujauzito. Unaweza kutumia asidi ya folic kama sehemu ya vitamin muhimu kama vile vitamin A ambayo sio nzuri kwa mtoto kama wewe tayari ni mjamzito.