Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Zifahamu Dalili za Ujauzito wa Mapacha

Mambo gani yanaongeza nafasi ya kupata ujauzito wa mapacha.

Jenetiki (vinasaba)  ni jambo la muhimu litakalo kuwezesha kupata watoto mapacha, nyinginezo ni kama vile;

  • Watoto wa kupandikizwa, ni njia ya kitaalamu inayofanyika pamoja na njia nyingine za uzazi kama vile IVF (in vitro fertilization) ambapo zaidi ya yai moja la mwanamke huwekwa kwenye mfuko wa uzazi, ambapo huongeza nafasi ya kupata mapacha.
  • Baada ya miaka 30 mwili wa mwanamke huzidisha utoaji wa homoni FSH (follicle stimulating hormone) ambayo husababisha kuachiliwa zaidi ya yai moja kwenye mfuko wa kizazi ambayo pia huchangia kuleta mapacha.
  • Kama umepita urefu wa kawaida na BMI yako ni 30 au zaidi nafasi ya kupata mapacha huongezeka.
  • Kama tayari wewe ni mama wa mapacha basi una nafasi ya kupata mapacha tena.
  • Utafiti wa madktari umeonyesha wamama wasiotumia nyama wana nafasi kubwa ya kupata mapacha. Kupungua kwa kiwango cha mapacha miaka ya 1990 ilisababishwa na matumizi ya madawa ya kukuzia ng’ombe kwa ajili ya maziwa na nyama.

Wanawake wa kinaigeria wana nafasi kubwa sana ya kupata mapacha kutokana na kula mazao kama mihogo na viazi. Kama haupo kwenye nafasi yoyote iliyotajwa hapo juu bado una nafasi ya kupata mapacha.

Utajuaje kama umepata ujauzito wa mapacha?.

  • Kiwango cha juu cha homoni, ambayo husababisha kuongezeka kwa kiwango cha magonjwa ya asubuhi katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za ujauzito wakati mwingine unaweza kupata ugonjwa wa asubuhi kujulikana kama “hyperemesis gravidarum” na pia kichefuchefu.
  • Ujauzito wa mapacha unaleta uchovu sana, kulala, na kujisikia vibaya, wiki mbili au tatu za mwanzo za ujauzito. Kulisha watoto wawili inahitaji usingizi wa kutosha na chakula bora kwa ajili ya mwili wako ili uweze kufanya kazi vizuri.
  • Hamu ya kula inaongezeka, kwani mwili wako unahitaji chakula cha kutosha kwa ajili ya kukuza watoto vizuri
  • Mfuko wa uzazi huwa mkubwa kwasababu umebeba zaidi ya kiumbe kimoja,hii inasababisha tumbo kuwa kubwa.
  • Mabadiliko ya jinsi unavyojisikia ni kitu cha kawaida kwasababu kiwango cha homoni kinaongezeka ili kuweza kustaimili ukuaji na maendeleo ya watoto, hali hii inaonekana sana wiki sita tangu ujauzito.
  • Ujauzito hutambilika sana baada ya kipimo cha mkojo au damu,baada ya kipimo hichi unaweza kupata uhakika kama una ujauzito wa kawaida au wa mapacha. Vilevile ujauzito wa mapacha unapelekea kuwa na mstari tumboni wenye rangi iliyokolea.

Tukiachana na hizo kuna ishara nyingine ambazo zinatofautisha ujauzito wa kawaida na ule wa mapacha.

Ishara zaidi za ujauzito wa mapacha

Kulingana na ishara za mwanzounaweza kutambua kama una ujauzito wa mapacha .lakini kuna ishara zaidi zinazoweza kukupa muafaka zaidi:

  • Wakati una ujauzito wa mapacha unaweza kuongezeka uzito haraka sana kuliko kubeba mtoto mmoja tu.
  • Uchunguzi wa mara kwa mara wa daktari wako unaweza kukusaidia kujua umri wa mtoto na ukuaji wake, kama kipimo hiko kinaongezeka kwa sentimita moja kila wiki basi ni ishara moja kuwa unatarajia kupata mapacha.
  • Kusogea kwa mtoto tumboni hutokea mapema sana wakati ukiwa na ujauzito mapacha kuliko mtoto ule wa mmoja.
  • Kuelekea mwisho wa miezi mitatu ya kwanza, daktari anaweza kuchukua kipimo kiitwacho “Doppler heartbeat count” kuweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto. Kama umebeba mapacha utasikia mapigo ya moyo mara mbili.
  • Ujauzito wa mapacha huambatana sana na kukosa pumzi, hii ni kwasababu ya ukuaji wa mfuko wa uzazi unaobana mapafu hivyo kusababisha kukosa hewa.
  • Nyonga kuuma ni ishara mojawapo ya ujauzito wa mapacha kwani kukua kwa mfuko wa kizazi kusio kwa kawaida husababisha nyonga kuuma kwani uzito unaongezeka na kukandamiza nyonga.
  • Maumivu ya uzazi ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito wa mapacha na unahitaji uangalizi wa madaktari kwa haraka.
  • Maumivu ya mara kwa mara ya mgongo ni ishara ya kuongezeka uzito kwa haraka, na kuongezeka kwa homoni ndani ya mwili. Kusimama wima na kuweka kifua mbele huweza kusaidia kukufanya upumzike vyema. Na kuvaa viatu visivyo na soli ndefu pia husaidia, wakati mwingine epuka kukunja magoti kwa muda mrefu wakati wa kukaa.
  • Kupata haja ndogo mara kwa mara, ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito. Lakini wakati una ujauzito wa mapacha haja ndogo inaongezeka zaidi kwasababu mfuko wa uzazi unakandamiza kibofu cha mkojo hivyo kusababisha kupata haja ndogo mara kwa mara.  Ni vizuri pia kupata haja kubwa, hakikisha unakula vyakula laini na vimiminika vya kutosha.
  • Kuongezeka kwa mapigoya moyo ni jambo lingine linaloweza kukupa uhakika kwamba unatarajia mapacha. Ongezeko la damu kwenye mwili linaweza likawa moja ya sababu.
  • Mwili wako unahifadhi maji mara mbili zaidi wakati ujauzito wa kawaida, ambayo yanakusaidia kuepuka tatizo la “edema”. Maji yanahifadhiwa mwilini ili kurudishia yale yaliotoka. Matunda kama matikiti maji, tofaa, machungwa, mapeasi na mananasi yanasaidia kuhakikisha mwili una maji ya kutosha. Acha kuvuta sigara na hakikisha ulaji wa chumvi ni wa kiwango kidogo.
  • Uchunguzi wa “Alpha fetoprotein test (APF)” unaofanyika baada ya miezi sita kuhakikisha kiwango cha protini kinatolewa na kijusi kwenye maini yake. Kiwango cha tofauti cha APF kinaweza kuonyesha uwepo wa mapacha kwasababu kitaongezeka mara mbili.

Tukiachana na hayo kuna ishara nyingine za kuonyesha uwepo wa mapacha ambazo ni sawa na ujauzito wa kawaida.

  • Harufu ya baadhi ya vyakula itakuchefu na kukufanya usikie kichefuchefu.
  • Ujauzito wa mapacha unahitaji mzunguko mwingi wa damu kuhakikisha ukuaji bora wa watoto, ongezeko la damu husababisha shinikizo la damu kuongezeka hasa katika mishipa ya damu ya miguu ijulikanayo kama “varicose veins”. Hatahivyo mkandamizo wa mtoto katika mfuko wa uzazi unaongeza upana wa mishipa hasa ile ya kizazi.
  • Matatizo ya mmeng’enyo wa chakula kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, kiungulia nk. Epuka vyakula vyenye viungo,mafuta mengi na kunywa maji yakutosha, pia kula kidogokidogo kwa mara nyingi uwezavyo.
  • Kukosa usingizi ni kitu cha kawaida sana hasa ukiwa na maumivu ya mgongo, nyonga kukata,kichefuchefu na kuchoka. Kulala kwa ubavu na kuweka mto katikati ya miguu yako na tumbo lako.
  • Katika wiki ya nne mpaka ya tano ya ujauzito wa mapacha unaweza kuwa na matiti yanayowasha na kuuma. Hii ni kwasababu ya mabadiliko ya homoni ndani ya mwii wako mpaka wiki ya sita, chuchu nazo huzidi kuwa nyeusi na kuuma pia, kuvaa sidiria za uzazi zinaweza kusaidia kupunguza maumivu.
  • Ujauzito wa mapacha unaweza kuongeza zaidi uwezekano wa kupata msongo wa mawazo baada ya kujifungua. Kwasababui inamchukua mama muda mrefu zaidi kubadili ratiba baada ya kujifungua. Tofauti na ujauzito wa kawaida mama wa mapacha anachoka zaidi kwasababu inambidi awalishe zaidi. Mazoezi kidogo na mapumziko yakutosha huweza kusaidia katika kipindi hiki. Unaweza kuongea na wazazi wengine juu ya taratibu na mambo gani yafanyike kutoka kwenye ujuzi walionao kwenye uzazi wa mapacha.

Tumbo kubwa ni ishara ya ujauzito wa mapacha. Lakini haimaanishi kwamba unatakiwa kuongezeka kilo kuliko ujauzito wa kawaida.

Vipimo Muhimu vya Kufanya Kabla ya Kupata Ujauzito

Sote tunajua umuhimu wa kufanya vipimo na matibabu husika ili kuhakikisha afya njema kwa mama mjamzito mtarajiwa na usalama wa mtoto wake anayekuja. Wataalamu wengi kwa sasa wanashauri wanawake waanze kumuona mkunga wao kabla hata ya kuanza kupata ujauzito.

Inawezekana ikashangaza kwa nini uanze kuwa na wasiwasi wa ujauzito kabla ya hata kuwa nao, ila daktari wako au mkunga anaweza kukufanyia vipimo na kuwa na uhakika wa kuwa wewe na mwenza wako hamna matatizo yaliyojificha yanayoweza kuleta madhara kwenye ujauzito au uwezo wenu wa kupata ujauzito. Daktari wako anaweza pia kukupa ushauri kuhusu mazoezi, lishe, mfumo wa maisha na virutubisho vya asidi ya foliki. Utafiti unaonyesha wanawake wanaomuona daktari au mkunga kabla ya kupata ujauzito wanaongeza uwezo wao wa kupata ujauzito na kupunguza matukio ya mimba kuharibika au mtoto kuzaliwa na matatizo.

Kinachotokea wakati wa uchunguzi

Wakati wa uchunguzi wa awali kabla ya ujauzito, daktari wako au mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi na vipimo mbalimbali kujua kama upo tayari kwa ujauzito. Baadhi ya uchunguzi utakaofanyika ni kama ifuatavyo:

1. Uzito

Kupima uzito ni muhimu ili kujua kama uzito wako ni sahihi kwa urefu wako na aina ya mwili wako. Kama sivyo, daktari wako atashauri mabadiliko mbalimbali kwenye lishe yako, mazoezi au madawa ili kuweza kurudisha uzito wako kuwa kawaida. Uwiano wa mwili na uzito (BMI) kati ya 18.5 na 22.9 ndio sahihi kwa wanawake.

2. Kipimo cha mkojo

Kipimo cha mkojo kugundua kama kuna maambukizi kwenye njia ya mkojo au figo ni mojawapo ya vipimo muhimu kabla ya kupata ujauzito.

3. Vipimo vya magonjwa mfumo wa uzazi wa wanawake

Vipimo hivi hufanywa kuchunguza uwepo wa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (uterine fibroids), uvimbe wenye maji (cysts) au uwepo wa maambukizi kwenye nyonga (PID). Pia kipimo hiki kinaangalia uwepo wa matatizo ya hedhi ikiwemo hedhi zisizo na utaratibu na pia uwepo wa matatizo yoyote yanayoweza kuleta shida kwenye ujauzito.

4. Uchunguzi wa matiti, nyonga na tumbo

Uchunguzi wa nyonga na njia ya uzazi yanaangalia uwepo wa fangasi au trichomona (trichomoniasis) ambayo yanaweza kuleta matatizo kwenye ujauzito. Tumbo linafanyiwa uchunguzi kuangalia kama kuna matatizo yoyote yanayoweza kuleta shida kwa uwezo wa ukuaji wa ujauzito. Matiti yanachunguzwa kama kuna uwepo wa uvimbe utakaohitaji ufuatiliaji wa karibu.

5. Kipimo cha Shinikizo la Damu (Blood Pressure)

Shinikizo la damu linapimwa ili kugundua uwepo wa shinikizo la juu au la chini kwani zote zinaweza kuleta matatizo kwenye ujauzito.

6. PAP Smear test (Kipimo cha ute wa mlango wa uzazi)

Uchunguzi wa ute wa mlango wa uzazi ni kipimo kimojawapo kitakachofanywa ukikutana na daktari kabla ya ujauzito. Kipimo hiki kinafanywa kwa daktari kuingiza kifaa maalumu kwenye uke (speculum) ili aweze kuona mlango wa mfuko wa uzazi (cervix). Daktari baada ya hapo hupanguza mfuko wa uzazi kwa kutumia pamba maalumu ili kupata ute ute uliopo kwenye mlango wa uzazi. Pamba hii na ute ute uliopatikana hutumwa maabara ili kuweza kufanyiwa uchunguzi. Kipimo hiki huchunguza kama umepata maambukizi ya magonjwa ya ngono kama kisonono, kaswende, HIV au Hepatiti B.

7. Vipimo vya damu

Vipimo vifuatavyo vya damu vinafanywa ili kugundua uwepo wa magonjwa mbali mbali:

  • Upungufu wa vitamini D
  • Wingi wa damu (Himoglobini)
  • Glucose (Kipimo cha sukari kwenye damu)
  • Aina ya damu (Rh factor)
  • Rubella
  • Varicella
  • Kifua kikuu (TB)
  • Hepatiti B
  • Toxoplasmosis
  • Thyroid
  • Maambukizi ya Ngono.

8. Magonjwa ya kurithi (Genetic conditions)

Zungumza na daktari wako kama kwenye familia yako kuna historia ya magonjwa ya Thalassemia, Cystic Fibrosis au Down`s Syndrome ili uweze kufanyiwa uchunguzi zaidi.

9. Matumizi ya uzazi wa mpango

Mtarifu daktari kuhusu njia ya uzazi wa mpango uliyokuwa unatumia. Njia nyingi za uzazi wa mpango haziathiri ni muda gani utachukua mpaka kupata ujauzito baada ya kuacha kuzitumia. Ijapokuwa, kama umekuwa ukitumia njia ya uzazi wa mpango ya sindano, inaweza kuchukua hadi mwaka mmoja kuweza kurudisha uwezo wako wa kupata ujauzito kuwa wa kawaida.

10. Mimba zilizopita

Inashauriwa kuzungumza na daktari wako kuhusu mimba zilizopita, zilizotoka na zile zilizotungwa nje ya mfuko wa uzazi. Ijapokuwa inaweza kuwa ni mazungumzo magumu kwako ila itamsaidia daktari wako kuweza kukupa msaada bora kuelekea kwenye ujauzito wako unaokuja.

Hitimisho

Pamoja na vipimo mbali mbali kama vilivyoelezwa hapo juu, tegemea pia daktari wako kuzungumza na wewe kuhusu lishe, afya yako kwa ujumla, mfumo wa maisha wa kufuata, utaratibu wa mazoezi wa kufuata na aina ya kazi yako na inavyoendana na ujauzito. Mueleze matatizo yoyote unayoyapata kuhusu mzunguko wako wa hedhi, pia matatizo yoyote ya kiafya uliyo nayo kama pumu, kisukari au shinikizo la juu la damu kwani yatamsaidia kukupa ushauri sahihi zaidi.

Ishara za Kupata Mtoto wa Kiume Wakati wa Ujauzito

Magonjwa ya asubuhi

Ukiwa  unatarajia mtoto dalili za awali ni pamoja na kupata magonjwa ya asubuhi,kusikia kichefuchefu ni moja kati ya ishara za kupata mtoto wa kiume.

Mapigo ya moyo kuongezeka

Ukigundua kuongezeka kwa mapigo ya moyo mpaka 140 kwa dakika inaweza kuonyesha kuwa unatarajia mtoto wa kiume.

Kutokwa chunusi ghafla

Kutokwa chunusi wakati wa ujauzito ni moja ya ishara za kupata mtoto wa kiume.

Hamu ya chakula

Wakati una ujauzito wa mtoto wa kiume, utakuwa na hamu sana ya vyakula vichachu na vyenye chumvi.

Nafasi na mkao wa tumbo

Mkao wa tumbo ni ishara moja ambayo inaweza kufanya kugundua jinsia ya mtoto. Kama tumbo lipo kwa chini unaonyesha kuwa utapata mtoto wa kiume.

Mabadiliko ya tabia

Jinsia ya mtoto ambae hajazaliwa huchangia sana mabadiliko ya tabia ya mama. Wamama wenye hasira sana wana matarajio ya kupata mtoto wa kiume.

Rangi ya mkojo

Rangi ya mkojo inapobaadilika na kukolea zaidi ni ishara kuwa unategemea kupata mtoto wa kiume.

Ukubwa wa matiti

Wakati wa ujauzito, matiti huongezeka na kuwa makubwa wakati ukijiandaa kunyonyesha mtoto wako mtarajiwa, wakati una ujauzito wa mtoto wa kiume titi lako la kulia ni kubwa kuliko lile la kushoto.

Miguu kuwa ya baridi

Hisia ya kuwa na mguu wa baridi mara kwa mara ni mojawapo ya ishara ya kuwa na mtoto wa kiume wakati wa ujauzito.

Kukua kwa nywele

Ishara nyingine ni kukua kwa nywele, ukuaji wa nywele unaongezeka maradufu na kukua kwa kasi kuliko kawaida.

Namna ya kulala

Wakati wa ujauzito unahisi uchovu haraka sana,na nyakati hizo ukilala sana ubavu wa kushoto ina maanisha utapata toto wa kiume.

Mikono kuwa mikavu

Mikono kuwa mikavu na kukauka ni ishara mojawapo kuwa utapata mtoto wa kiume.

Kuongezeka uzito

Pamoja na tumbo la duara, kuongezeka uzito ni ishara kuwa unatarajia kupata mtoto wa kiume, tofauti na wakati unatarajia kupata mtoto wa kike uzito wa mama husambaa mwili mzima ukijumuishwa uso.

Vipimo vitakakvyoonyesha jinsia ya mtoto wakati wa ujauzito.

Ultrasound ni kipimo sahihi kinachoonyesha jinsia ya mtoto, kipimo hiki ni sahihi kwa karibia asilimia 90 na huonyesha kwa usahihi jinsia ya mtoto.

 

Ishara za Kupata Mtoto wa Kike Wakati wa Ujauzito

Mapigo ya moyo kuongezeka

Ukitambua kuongezeka kwa mapigo ya moyo,mpaka 140 -160 kwa dakika inaweza kuonyesha kuwa unatarajia mtoto wa kike.

Magonjwa ya asubuhi

Wakati unatarajia mtoto dalili za mwanzo ni kupata magonjwa ya asubuhi, na kichefchefu ni moja kati ya ishara za kupata mtoto wa kike.

Kutokwa chunusi ghafla

Kutokwa na chunusi wakati wa ujauzito ni moja ya ishara za kupata mtotot wa kike.

Nafasi na mkao wa tumbo

Mkao wa tumbo ni ishara moja ambayo inaweza kufanya ugundue  jinsia ya mtoto. Kama tumbo lipo kwa juu au katikati inaonyesha kuwa utapata mtoto wa kike.

Mabadiliko ya tabia

Jinsia ya mtoto ambae hajazaliwa huchangia sana mabadiliko ya tabia ya mama. Wamama wenye hasira sana na wababe huonyesha kuna matarajio ya kupata mtoto wa kike.

Ukubwa wa matiti

Wakati wa ujauzito, matiti huongezeka na kuwa makubwa wakati ukijiandaa kunyonyesha mtoto wako mtarajiwa, kama una ujauzito wa mtoto wa kike titi lako la kushoto linakuwa kubwa kuliko lile la kulia.

Kipimo cha kitunguu saumu

Unapokula kitunguu saumu na harufu yako kubaki kama ile ya kawaida basi unatarajia kupata mtoto wa kike. Ukiwa unatarajia mtoto wa kiume ukila kitunguu saumu harufu hupenyeza kwenye ngozi yako na kubaki mwilini mwako.

Namna ya kulala

Wakati wa ujauzito unahisi uchovu haraka sana,na nyakati hizo ukilala sana ubavu wa kulia inamaanisha utapata mtoto wa kike.

Utafiti wa umbo la kichwa

Kama unatarajia mtoto wa kike, katika kipimo cha “ultrasound” kitaonyesha muundo wa kichwa na taya ya chini kuwa duara kama unatarajia mtoto wa kike.

Kipimo cha baking powder

Chukua baking powder kijiko kimoja changanya na maji kwenye glasi alafu changanya na mkojo wako kidogo, kama utabadilika na kuwa mzito kwa mbali, basi unatarajia mtoto wa kiume lakini baada ya kuchanganya mkojo na mchanganyiko wa baking powder na maji, na hakuna mabadiliko yoyote basi unatarajia mtoto wa kike.

Ulaini wa nywele na mng’ao

Kama nywele zako ni nyembamba na kukatika inamaanisha unatarajia mtoto wa kike, hata hivyo nywele zinazong’aa na kuvutia ni ishara ya kwamba unatarajia mtoto wa kiume.

Rangi ya mkojo

Rangi ya mkojo wako husaidia sana kuweza kutambua jinsia ya mtoto wako, rangi ya njano ya mkojo huashiria sana kwamba unapata mtoto wa kike.

Kutamani kula vitu vitamu

Kutamani kula vitu vitamu kama pipi, chocolate,ice cream ni ishara unatarajia kupata mtoto wa kike. Kutamani vitu vya chumvichumvi ni ishara kuwa unatarajia mtoto wa kiume.

Matiti kuongezeka ghafla

Utatambua kuongezeka ghafla kwa matiti hii ni ishara mojawapo kwamba unatarajia kupata mtoto wa kike. Katika kipindi hiki kama ni mtoto wa kiume mabadiliko hata hayataonekana.

Kuwa mkarimu.

Inasemekana kuwa mkarimu kipindi chote cha ujauzito ni ishara kwamba unatarajia kupata mtoto wa kike.

Dalili 10 za Awali za Ujauzito

Kuwasha, kuvuta kwa chuchu

Kadiri homoni za mimba zinavyoongeza usafirishaji wa wa damu kwenye matiti yako unaongezeka, hivyo unaweza kuhisi hali ya kuvuta kuzunguka chuchu zako.

Hii inaweza kuwa moja ya dalili za awali za mimba, na muda mwingine kugundulika pia ndani ya wiki au zaidi ya baada ya mimba kutungwa. Mara baada ya mwili wako kuzoea ongezeko la homoni, hali hii itapotea.

Maumivu ya tumbo na kuona matone ya damu kwenye nguo za ndani.

Sio kawaida kuchafuka ukiwa karibia wiki 6 za ujauzito. Unaweza kugundua rangi ya pinki kwa mbali au madoa ya kahawia katika nguo zako za ndani(chupi) au wakati unakojoa au kuhisi maumivu ya tumbo kwa mbali. Wataalamu hawana uhakika kabisa kwanini dalili hizi zinatokea katika hatua za awali za mimba. Inasadikika ni kwasababu ya ukuaji wa plasenta.

Kama umekumbwa na tatizo la kutokwa damu ambalo sio kawaida, muone daktari mapema ili kuwa katika hali ya usalama.

Kujisikia kuumwa

Kama una bahati utaepuka kichefuchefu kabisa. Hata hivyo,magonjwa ya asubuhi ni moja ya dalili za awali za kawaida za mimba, dalili hizi zinaweza kuanza mapema katika wiki ya nne. Unaweza kujisikia kuumwa na kichefuchefu. Hali hii inaweza kukupata mda wowote ndani ya siku, mchana au usiku.

Kukua,kuvimba kwa matiti

Mara baada ya kufika wiki ya sita ya ujauzito wako, matiti yako yanakua nyeti zaidi. Inakua sawa na jinsi unavyojisikia kabla ya hedhi.

Unaweza kugundua kwamba maziwa yako yamekua na kuvimba,na mishipa kuonekana chini ya ngozi. Kukua kwa maziwa ni dalili ya kawaida katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

Kujisika kuchoka

Umechoka?Unaweza kushinda kitandani mda wote kadiri mwili wako unavyojitahidi kukubaliana na uwepo wa mtoto ndani yako, tangu mwanzo wa mimba. Homoni za mimba za mwili wako ndio zinakufanya kuhisi umechoka, mwenye hasira na hisia kali.

Uchovu ni dalili ya kawaida ya mimba, na hutokea zaidi katika kipindi cha kwanza cha mimba na hatua za mwisho za ujauzito.

Kupata haja ndogo mara kwa mara

Katika wiki yako ya sita ya mimba utagundua unakojoa sana. Hii ni kwasababu ya mjumuiko wa homoni za mimba, wingi wa damu ndani ya mfumo wako na figo zako kufanya kazi nzito zaidi. Ikiwa utahisi maumivu au kuungua wakati unakojoa, unaweza ukawa na UTI, muone daktari kama unahisi umepata maambukizo ya ugonjwa huu.

Chuchu nyeusi

Mabadiliko ya ngozi ni ya kawaida wakati wa ujauzito. Moja ya mabadiliko ya kwanza ambayo unaweza kuona ni mduara wa ngozi pande zote za chuchu zako (vidogo) unakua mweusi. Hii inaweza kutokea kuanzia wiki ya nane.

Unaweza pia kugundua kwamba  viuvimbe vidogo vya ngozi  vinavyozunguka chuchu zako vinajitokeza zaidi na kuchomoza zaidi. Uke wako pia unaweza kubadilika rangi na kuwa rangi ya pinki ya kukolea ingawa unaweza usitambue

Hamu ya kula kubadilika na hata hisia ya harufu hubadilika

Hamu ya kula inaweza ikawa ni moja ya dalili za mimba/ujauzito. Unaweza kuachana na aina flani za chakula mwanzoni hata kabla hujakosa siku zako.

Utaanza  kutambua hisia ya chuma mdomoni, au kutambua hupati hamu ya kunywa ya kahawa, au chakula ambacho umezoea kula.

 Kukosa hedhi

Ikiwa hedhi yako ni ya kawaida, na imechelewa kuanza, ni bora ukachukua kipimo cha mimba kabla hujagundua dalili nyingine. Kukosa hedhi ni moja ya ishara hakika ya ujauzito.Lakini ikiwa  hedhi yako si ya kawaida au umepoteza uelekeo lini hedhi yako inatarajia kuanza,unaweza usigundue kama hedhi imechelewa. Katika wakati huo matiti yanakua, kichefuchefu na kwenda haja ndogo kila mara zinweza kuwa dalili za mwanzo kuonyesha wewe ni mjamzito.

Kipimo cha nyumbani cha mimba

Vipimo vingi vya mimba vya nyumbani vitakupatia majibu ya uhakika , kama ukisubiri mpaka siku ya kwanza ya kukosa hedhi yako.

 

Jinsi Ujauzito Unavyotokea (Hatua kwa Hatua)

Utungaji mimba hutokea kipindi yai la mwanamke linapokutana na seli za gamete za kiume zilizokomaa (manii). Inaweza chukua dakika 45 mpaka masaa 12 kwa manii kufika katika mirija ya falopiani ambapo mimba hutungiwa. Hata hivyo, manii yanaweza kuendelea kuishi ndani ya mwili wa mwanamke mpaka siku saba, hivyobasi utungaji wa mimba unaweza kutokea siku yoyote katika wiki ifuatayo baada ya kujamiana, kama upo katika siku za kutoa mayai(ovulation).

Ndani ya mwili wa mwanamke: jinsi yai linavyotungwa

Kwa wanawake, uwezekano wa mimba unaanzia katika ovari zake. Hizi ni ogani ndogo mbili zenye umbo la yai zilizoshikiliwa katika kila upande wa mjii wa mimba(uterasi). Ovari zimejazwa mayai ambayo yalitengenezwa kabla ya kuzaliwa. Kila mtoto mchanga wa kike anazaliwa na milioni 1 mpaka 2 ya mayai kwa kila ovari yake.

Mayai mengi yanaanza kufa mapema na mengine kupungua taratibu kadiri unavyozidi kukua. Mara unapoanza hedhi, kawaia kati ya miaka 10 na 14, ni mayai 600,000(laki sita) tu yanaweza kuwepo. Katika umri wa miaka 30, wanasayansi wamekokotoa ni ttakribani mayai 72,000 yanaweza kubakia.
Kuna uwezekano wa kuzalisha mayai 400-500 katika kipindi cha miaka yako ya kuzaa, ambayo ni kati ya hedhi yako ya kwanza na wakati wa kukatika hedhi.

Katika kila mzunguko wa hedhi,mara nyingine baada ya hedhi yako, kati ya mayai matatu na 30 yanaanza kukua katika kila moja ya ovari zako. Yai lililoiva linakua la kwanza kutolewa kupitia mfumo wa utoaji wa mayai(ovulation). Yai linamezwa na mirija ya falopiani iliyokaribu, kuna mirija miwili, kila mmoja una urefu wa 10sm, ambayo inaelekezwa kwenye mji wa mimba kutoka kwenye ovari.

Kawaida utolewaji wa mayai katika ovari(ovulation) ni takribani siku 14 kabla ya hedhi yako ijayo. Muda muafaka wa utolewaji wa mayai unategemea na urefu wa mzunguko wako wa hedhi. Homoni kadhaa wa kadhaa zinafanya kazi pamoja kudhibiti mzunguko wako, kukomaa kwa mayai na muda wa kutolewa mayai (ovulation).

Yai baada ya kutolewa huishi mpaka masaa 24 kwa wastani. Yai hili linahitaji kurutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mda huu ili mimba kutungwa. Kama yai likikutana na mbegu ya kiume yenye afya ikielekea kwenye mji wa mimba, utengenezaji wa kiumbe kipya unachukua nafasi. Kama sivyo, safari ya mwisho ya yai itakua kwenye uterasi na kuharibika.
Ikiwa haujashika mimba, ovari huacha kutengeneza homoni za estrogen na progesterone. Hizi ni homoni mbili ambazo zitasaidia kuhifadhi mimba. Wakati viwango vya homoni hizi vinashuka,ukuta mwembamba ndani ya uterasi unatolewa wakati wa hedhi yako.Mabaki ya mayai yasiorutubishwa hutolewa pia wakati mmoja.

Ndani ya mwili wa mwanaume: jinsi mbegu za kiume (shahawa) zinavyotengenezwa.

Miili ya wanawake hutengeneza yai moja kila mwezi. Hata hivyo miili ya wanaume, inakua katika kazi wakati wote, hutengeneza milioni za mbegu za kiume. Dhumuni pekee la kila mbegu ni kuogelea na kupenya kwa yai la mwanamke.

Kuanzia mwanzo mpaka mwisho inachukua karibu wiki 10 kutengeneza seli mpya ya mbegu ya kiume. Nusu ya mbegu zinazotengenezwa zinaishi wiki chache ndani ya mwili wa mwanaume, na angalau milioni 39 zinatolewa nje ya mwili (ejaculation).Ina maana kwamba wanaume wanapaswa kutengeneza mbegu mara kwa mara katika maisha yao yote ya utu wazima.

Homoni zinazodhibiti utengenezaji wa mayai(ovulation) kwa wanawake zinahamasisha utolewaji wa homoni ya testosteroni kwa wanaume. Testosteroni ni homoni inayohusika na kuzalisha manii. Uzalishaji wa manii huanza ndani korodani, tezi mbili zilizomo katika kifuko kilichokuwa chini ya uume.Korodani(mapumbu) zinapatikana nje ya mwili kwa sababu ni hatari kwenye mazingira ya joto. Ili kuzalisha mbegu bora yenye afya inapaswa kukaa kwenye digrii 34 za sentigredi. Hii ni karibia digrii nne pungufu ya joto la kawaida la mwili. Mara baada ya manii kutengenezwa, yanahifadhiwa katika kila korodani ndani ya mrija unaounganisha korodani na urethra, yenye urefu wa mita sita.

Kabla ya kumwaga mbegu nje ya mwili(ejaculation), mbegu hutolewa na kuchanganywa na shahawa.
Licha ya utengenezaji wa milioni za mbegu na utolewaji kwa njia ya kumwaga nje ya mwili(ejaculation), ni mbegu moja tu inaweza rutubisha kila yai. Jinsia ya mtoto wako inategemea na mbegu ya kwanza kupenya kwenye yai. Mbegu zenye kromosamu Y zinatengeneza mtoto wa kiume, na zile za X zitatengenza mtoto wa kike.

Nini hutokea wakati wa kujamiana

Pamoja na raha zote, miili yenu inatengeneza mvutano ambao utaishia kufika kileleni (climax). Kufika kileleni katika tendo la ndoa kuna kazi muhimu ya kibiolojia. Kwa wanaume, kufika kileleni husababisha shahawa kufika katika uke na kuelekea kwenye via vya uzazi kilomita 10 kwa saa. Kitendo cha kumwaga mbegu(ejaculation), hupatia mbegu mwongozo mzuri kuelekea kwenye yai la mwanamke. Mwanamke hana haja ya kufika kileleni ili mimba itungwe.mibano milaini ya kuta za uterasi zinaweza kusaidia mbegu ya mwanaume kusafiri vizuri kufikia lengo lake, lakini haya yote hutokea bila mwanake kufika kileleni.

Sio wanawake wote, miili yao inatoa yai katikati ya mizunguko yao au mda sawa katika mizunguko yao ya mwezi. Ili kuboresha nafasi yako ya kushika mimba, weka lengo la kujamiana kila siku mbili au tatu za mzunguko wako.

Wakati unapumzika baada ya ngono, kazi ya manii ndo kwanza inaanza

Katika kipindi hiki hakuna kubwa la kufanya zaidi ya kuomba jambo la kushika mimba lifanikiwe.wakati wewe na mwenzi wako mnafurahia tendo la ndoa, kuna mengi yanaendelea ndanu ya mwili wako. Mamilioni ya manii yameanza kazi yao ya kutafuta yai la mwanamke, na ijulikane kwamba hii sio kazi rahisi. Kipingamizi cha kwanza kinaweza kuwa uteute wa kizazi cha mwanamke ambayo unaweza kuonekana kama nyavu isiyoruhusu kuingia kwenye siku zisizofaa kurutubisha yai. Unapokuwa katika siku nzuri za kushika mimba, ni miujiza sana kwani uteute hu wa kizazi unapungua na kuruhusu mbegu yenye nguvu na kuogelea kwa kasi kuvuka.

Kwa mbegu ambayo imefanikiwa kuvuka bado ina safari ndefu mbele. Zinahitajika kusafiri karibia sentimita 18 kutoka kwenye uke kupitia kwenye uterasi(mji wa mimba) mpaka kwenye mirija ya falopiani. Ni mtihani mkubwa ukizingatia usafiri wake ni wa kiwango cha sentimita 2.5 kila dakika 15. Mbegu ya kiume yenye kusafiri kwa haraka zaidi inaweza kukutana na yai katika dakika 45. Inaweza kuchukua mpaka masaa 12 kwa mbegu ya kiume yenye kasi ndogo kufikia yai. Kama mbegu haijakutana na yai katika mirija ya falopiani mda wa kujamiana, inaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke mpaka siku saba. Hii ina maana yai likitolewa(ovulation) ndani ya huu mda unaweza kushika mimba.

Kiwango cha vifo vya manii ni cha juu sana na dazeni kadhaa tu huwahi kulifikia yai. Nyinine hukamatwa,kupotea(pengine kuelekea mrija wa falopiani ambayo sio) au kufa zikiwa katika safari. Kwa wachache wanaofanikiwa kulikaribia yai, bado mpambano ni mkali. Kila mmoja anahitaji kufanya kazi kwa kasi ili kupenya sheli ya nje ya yai na kupita ndani kabla ya wengine. Yai linatakiwa kurutubishwa ndani ya masaa 24 baada ya kutolewa. Mara baada ya manii yenye kazi na nguvu kufanikiwa kupenya kwenye yai, mara moja yai linabadilika na kuzuia manii nyingine kuingia kitendo hiki ni kama kinga inayotolewa na yai mara tu mbegu ya kwanza iko salama ndani.

Sasa maisha mapya yamezaliwa

Wakati wa urutubishaji(muunganiko wa manii na yai),maumbile katika manii na yai huchanganya kuunda kiini kipya ambacho kitaanza kugawanyika haraka. Mjumuiko huu wa seli mpya unajulikana kama blastocyst. Inaendelea kusafiri kutoka kwenye mirija ya falopiani kwenda kwenye mji wa mimba, safari inayochukua siku tatu au zaidi.

Huwezi kuwa mjamzito mpaka mjumuiko wa seli(blastocyst) ijishike yenyewe kwenye ukuta wa uterasi ambayo itakua kijusi na plasenta. Mara nyingine, blastocyst ijishikisha mahali pengine mbali na mji wa mimba (kwa kawaida katika mirija ya fallopian). Hii inaitwa mimba ya ectopic, ambayo ni mimba isiyo ya kawaida na inaweza kuishia katika matibabu ya dharura. Mimba haiwezi kuishi nje ya mji wa mimba uzazi na kwa hali hii inahitaji kutibiwa au kuondolewa kabisa.

Dalili na Ishara kuu 10 kuwa una Ujauzito

1. Kuwasha na kuvuta kwa chuchu

Kadiri homoni za mimba zinavyoongeza usafirishaji wa wa damu kwenye matiti yako, unaweza kuhisi hali ya kuvuta kuzunguka chuchu zako. Hii inaweza kuwa moja ya dalili za awali za mimba, na muda mwingine kugundulika pia ndani ya wiki au zaidi ya utungaji wa mimba. Mara baada ya mwili wako kuzoea  ongezeko la homoni, hali hii itapotea.

2. Maumivu ya tumbo na kugundua kuchafuka

Sio kawaida kuchafuka ukiwa na karibia wiki 6 za mimba. Unaweza kugundua rangi ya pinki kwa mbali au madoa ya kahawia katika nguo zako za ndani(chupi) au wakati unakojoa au kuhisi maumivu ya tumbo kwa mbali. Wataalamu hawana uhakika kabisa kwanini dalili hizi zinatokea katika hatua za awali za mimba. Inafikirika kusababishwa na ukuaji wa plasenta. Kama umekumbwa na tatizo la kutokwa damu ambalo sio kawaida, muone daktari mapema ili kuwa katika hali ya usalama.

3. Kujisikia kuumwa

Kama una bahati utaepuka kichefuchefu kabisa. Hata hivyo,magonjwa ya asubuhi ni moja ya dalili za awali za kawaida za mimba, japo zinaweza kuanza mapema katika wiki ya nne. Unaweza kujisikia kuumwa na kichefuchefu. Hali hii inaweza kukupata mda wowote ndani ya siku, mchana au usiku.

4. Kukua,kuvimba kwa matiti

Mara baada ya kufika wiki ya sita ya ujauzito wako, matiti yako yanakua nyeti zaidi. Inakua sawa na jinsi unavyojisikia kabla ya hedhi. Unaweza kugundua kwamba maziwa yako yamekua na kuvimba,na mishipa kuonekana chini ya ngozi. Kukua kwa maziwa ni dalili ya kawaida katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

5. Kujisika kuchoka

Umechoka? Unaweza jikuta unashinda kitandani mda wote kadiri mwili wako unavyojitahidi kukubaliana na uwepo wa mtoto ndani yako, tangu mwanzo wa mimba. Homoni za mimba za mwili wako ndio zinakufanya kuhisi umechoka, mwenye hasira na hisia kali. Uchovu ni dalili ya kawaida ya mimba, na hutokea zaidi katika kipindi cha kwanza cha mimba na hatua za mwisho za ujauzito.

6. Uhitaji wa kukojoa kila mara

Katika wiki yako ya sita ya mimba utagundua unakojoa sana. Hii ni kwasababu ya mjumuiko wa homoni za mimba, wingi wa damu ndani ya mfumo wako na figo zako kufanya kazi ngumu zaidi. Ikiwa utahisi maumivu au kuungua wakati unakojoa, unaweza ukawa na UTI, muone daktari kama unahisi unao huu ugonjwa.

7. Chuchu nyeusi

Mabadiliko ya ngozi ni ya kawaida wakati wa ujauzito. Moja ya mabadiliko ya kwanza ambayo unaweza kuona ni mduara wa ngozi pande zote za chuchu zako (vidogo) vinakua nyeusi. Hii inaweza kutokea kutoka wiki nane. Unaweza pia kupata kwamba  vifungo vidogo vyangozi  vinavyozunguka chuchu zako vinajitokeza zaidi na kuchomoza zaidi. Vumbu yako na uke hubadilika na kua nyekundu zambarau iliyokolea, ingawa unaweza usione hili.

8. Matamanio ya chakula na kuhisi haraka kwa mabadiliko ya harufu au hisia ya harufu kubadilika.

Mabadiliko katika matamanio ya chakula yanaweza kuwa dalili ya ujauzito. Unawezekana kuacha ladha fulani wakati wa kwanza, hasa kabla hujakosa kuona hedhi yako. Unaweza kuhisi  ladha ya chuma katika kinywa chako, au kushindwa kutumia kahawa yako ya asubuhi au chakula ambacho unachokipenda, kama vile mayai. Hisia yako ya harufu inaweza pia kubadilika, mabadiliko haya yanaweza kuwa makali zaidi kwenye chakula na harufu ya mapishi.

9. Kukosa hedhi

Ikiwa hedhi yako ni ya kawaida, na hedhi yako haijaanza kwa muda, ni bora ukachukua kipimo cha mimba kabla hujagundua dalili nyingine. Kukosa hedhi yako ni moja ya ishara hakika ya ujauzito. Lakini ikiwa  hedhi yako si ya kawaida au unapoteza dira ya hedhi ijayo inakuja lini, unaweza usigundue kama hedhi yako imechelewa. Katika kesi hiyo, matiti ya kukua, hisia za kichefuchefu na kufanya safari za ziada chooni inaweza kuwa dalili za mwanzo kuwa wewe ni mjamzito.

10. Kipimo cha nyumbani cha mimba

Vipimo vingi vya mimba vya nyumbani vitakupatia majibu ya uhakika , kama ukisubiri mpaka siku ya kwanza ya kukosa hedhi yako.

Dalili hatari kipindi cha ujauzito ambazo si za kupuuzia

Hata kama umesoma sana na kuongea na wazazi mbalimbali kuhusu dalili mbali mbali kipindi cha ujauzito, bado itatokea baadhi ya wakati ambapo utakuwa huna uhakika kama unavyojisikia ni kawaida au la.
Dalili zifuatazo ni muhimu kuzipa uzito wake na kuzifuatilia kwa makini. Kama ukizipata dalili hizi ni vyema kuwasiliana na mkunga, daktari wako au kituo cha kliniki ya wajawazito haraka iwezekanavyo.

Nina maumivu tumbo la kati

Maumivu makali au vichomi katikati au juu kidogo ya tumbo, ikiambatana na kchefuchefu na kutapika, inaweza kumaanisha kitu kimoja kati ya vifuatavyo. Unaweza ukawa na:

  • Kuvimbiwa kulikopitiliza
  • Kiungulia
  • Tumbo kuchafuka

Kama upo kwenye miezi mitatu hadi sita ya ujauzitowako, hii inawezza kumaanisha presha mimba ya awali. Hii ni dalili hatari na itahitaji matibabu ya haraka.

Nina maumivu ya tumbo ka chini

Maumivu makali upande mmoja au pande zote kwenye tumbo lako la chini yanahitaji uchunguzi kugundua kama sio kitu cha kushtua.

Kwa kiwango cha chini kabisa inaweza pia ikawa ni dalili za:

  • Mimba nje ya mji wa mimba
  • Mimba kutoka
  • Uchungu uliowahi
  • Uvimbe kwenye kizazi – uliovunjika na kuanza kuvuja damu kwa ndani yake.
  • Kuachia kwa kondo la nyuma (placenta)

Nina homa

Kama una homa na una jotoridi zaidi ya digrii 37.5c, na bila dalili za mafua, ni vyema kumuona daktari ndani ya siku hiyo hiyo.

Kama jotoridi ni zaidi ya nyuzi joto 39c wasiliana au fika kwa daktari wakati huo huo bila kusubiri. Inawezekana umepata maambukizi. Daktari wako atakuandikia dawa za kupambana na bakteria na kushauri upate mapumziko. Kama nyuzi joto za mwili wako zitapanda zaidi ya nyuzi joto 39 kwa muda mrefu itamuathiri mtoto wako tumboni.

Ninaona maruerue (mbili mbili) na nyota nyota

Muone daktari haraka kama, katika miiezi mitatu hadi sita ya ujauzito wako, kuona kwako kunapata shida ya:

  • Kuona mbili mbili
  • Kuona ukungu
  • Kuona giza
  •  Kuona nyota nyota

Matatizo haya kwenye mfumo wa kuona yanaweza yakawa ni dalili za presha mimba ya awali (Pre-eclampsia)

Mikono na miguu yangu imevimba

Kuvimba au kuumuka (oedema) kwenye mikono, uso, macho ni kawaida mwishoni mwa ujauzito. Mara nyingi sio kitu cha kuleta wasiwasi. Lakini kama kuvimba huku ni kukubwa na kumetokea ghafla, kukiambatana na kichwa kuuma na matatizo ya kuona kwako, inawezekana ukawa na presha mimba ya awali (pre-eclampsia). Kama utaona dalili yoyote kati ya hizi wasiliana na daktari bila kuchelewa.

Nina maumivu makali ya kichwa yasiyopungua

Kama maumivu makali ya kichwa yanaendelea kwa masaa mawili hadi matatu, na pia una matatizo ya kuona kwako na kuvimba sana kwa mwili wako, inawezekana ukawa na presha mimba ya awali (pre-eclampsia). Kama presha mimba ya awali ikitokea, mara nyingi huwa ni katika nusu ya mwisho ya ujauzito wako au punde tu baada ya kujifungua.

Ninavuja damu ukeni

Matone au kutokwa na damu kidogo bila maumivu ni kawaida kipindi cha mwanzo cha ujauzito. Inawezekana ni kuvuja kwa damu kunakosababishwa na zile homoni zinazouongoza mzunguko wako wa hedhi ziliendelea kutolewa kwa nguvu ya ziada na kusababisha kuvuja kwa damu kidogo.
Usiwe na wasiwasi kuhusu aina hii ya kutokwa damu, kwani hali hii huondoka yenyewe na si rahisi kumdhuru mtoto wako.
Pamoja na hilo, ni vyema kuwasiliana na mkunga au daktari wako kama utapata kutokwa na damu ukeni katika hatua yoyote ya ujauzito wako. Inaweza ikawa inamaanisha kuna tatizo kubwa kwenye ujauzito wako kama:

  • Kutoka damu tofauti na ilivyo kawaida kwa hedhi yako, inaweza ikawa nyepesi zaidi na nyeusi zaidi kuliko kawaida. Hili pamoja na maumivu makali ya muda mrefu upande mmoja wat umbo lako inaweza ikawa ni dalili ya mimba nje ya mji wa mimba.
  • Kutokwa kwa damu kwingi, ikiungana na maumivu ya muda mrefu ya mgongo au tumbo la chini inaweza kuwa ni dalili ya kutoka kwa mimba.
  • Kutoka kwa damu kwa ghafla kusiko ambatana na maumivu yoyote.

Imepitiwa: April 2017