Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Virusi Vya Corona COVID19 na Ujauzito

 

Je, wajawazito na kina mama wanaonyonyesha wanahitaji kujua nini kuhusu virusi vya corona?

Kuna mengi yasiyofahamika kuhusu madhara ya virusi vya corona kwa wajawazito na kina mama wanaonyonyesha. Lakini uelewa wa madhara ya virusi hivi utaongezeka kadiri muda unavyoenda.

Kuwa mjamzito huleta wasiwasi na hali ya sintofahamu kwa wamama wengi watarajiwa, hata kama kila kitu kinaenda sawa.

Wanahitaji kuepuka aina fulani ya vyakula mfano samaki wasiopikwa vizuri na jibini laini. Hii ni kwasababu miili yao inabadilika kwa kiasi kikubwa kila siku na utaratibu wake wa kawaida unaweza kuvurugika.

Taifa la Uingereza ni moja ya nchi ambazo hivi karibuni zimewahusisha wanawake wajawazito katika kundi la watu walio katika hatari za kupata maambukizi haya. Inashauriwa wanawake wajawazito kukaa mbali na mikusanyiko ya watu ili kupunguza nafasi za kushika virusi vya Corona. Inaeleweka, wajawazito wengi na familia zao wana wasiwasi na wamechaganyikiwa kwasababu ya ujio huu wa Virusi vya Corona.

Pamoja yote hayo, ukweli unabaki kuwa hatuna ufahamu wa kutosha kuhusu madhara ya virusi hivi vya Corona COVID-19 kwa wajauzito. Kuwepo kwa ufahamu wa kutosha husaidia kuchukua hatua za uhakika. Uwepo mdogo wa wanawake wajawazito waliopata maambukizi haya pamoja na ufahamu wa kutosha wa Virusi hivi vya Corona kwa ujumla utatusaidia kutoa ushauri wa ziada kwa wanawake wajawazito kuchukua tahadhari mapema.

Mfumo Dhaifu wa Kinga ya Mwili

Mwanzoni ilidhaniwa kipindi cha ujauzito kinga ya mwili ya mwanamke inadhoofika na kumfanya kuwa katika hatari ya kupata maambukizo. Hata hivyo, kama ilivyo vitu vingi vinavyohusiana na mwili wa binadamu ushahidi mpya unaonesha kuwa kinga mwili ya mjamzito hupanda kipindi cha ujauzito, na wakati mwingine huwa ni ya kubadilika badilika.

Mabadiliko haya ya kinga ya mwili kipindi cha ujauzito ni muhimu kwa ajili ya kumpa nafasi mtoto anayeendelea kukua katika hatua tofauti za ujauzito. Kwa mfano katika hatua za kwanza za ujauzito kinga ya mwili inabadilika ili kuruhusu upandikizaji katika mwili. Wakati mwingine mfumo wa kinga unahitaji kujirekebisha katika njia tofauti, mfano mzuri ni wakati mwili wa mwanamke unajiandaa kupata uchungu wa kujifungua.

Jambo la muhimu katika maelezo yote haya ni kwamba kuwa na mfumo wa kinga wenye kubadilika badilika inakuweka katika hatari kubwa ya matatizo ya Virusi vya Corona kama vile shida katika upumuaji na hata homa ya mapafu (pneumonia).

Kitu cha kwanza cha kutiliwa mkazo ni wanawake wajawazito waendelee kuhudhuria miadi yao ya kliniki katika hospitali isipokuwa kama wameambiwa vinginevyo na mkunga au daktari wao.

Kwa sasa hakuna sababu ya kubadilisha mpango wako wa kujifungua, kama uliandaa hapo awali. Mpango wa kujifungua unahusisha mahali unapotarajia kujifungulia (hospitali, zahanati, kituo cha afya, au nyumbani) na aina gani ya dawa za maumivu unatarajia kupata.

Walakini, ikiwa umeonekana na dalili zinazoashiria maambukizi ya Virusi vya Corona, kama kikohozi kikavu au joto kubwa la mwili, kubanwa kifua na kupumua kwa shida,  ni lazima ujitenge (self-isolation) na wasiliana na daktari au mkunga wako haraka.

Vilevile, kwa wanawake wajawazito wenye matatizo mengine ya kiafya wanahitaji kuwa makini zaidi na kukaa mbali na mikusanyiko ya watu ikiwezekana kufikiria kujitenga (self-isolation) kipindi cha ujauzito. Wanawake waliopata ugonjwa wa kisukari, aina ya ugonjwa wa kisukari ambayo ni matokeo ya ujauzito ijulikanayo “Ugonjwa wa Kisukari kipindi cha Ujauzito” (gestational diabetes), wanatakiwa kuchukua tahadhari na kupunguza migusano na watu.

Kuwa mgonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito ni kundi la hatari hata bila kupata Virusi vya Corona, kwasababu ugonjwa huu wa kisukari unaongeza ugumu wakati wa ujauzito na kujifungua. Zaidi ya hapo, viwango vikubwa vya sukari katika damu kwa mda mrefu bila kutibiwa na kuangaliwa vizuri vinaweza kudhoofisha mfumo wa kinga zaidi.

Kutokana na mfumo wa kinga unaobadilika kila hatua wakati wa ujauzito ni vizuri wanawake wasio na matatizo ya kiafya kuchukua tahadhari na kukaa mbali na watu pale inapobidi.

Kama ilivyo wajawazito wengi wanaishi na wenzi wao au mara nyingine mtoto/watoto wao wengine, ushauri huu ni vizuri kufuatwa ili kupunguza nafasi ya kuweka afya ya mama mjamzito katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.

Tahadhari hizo ni pamoja na kufanya kazi ukiwa nyumbani kwa wale wanaoweza, kataa mgusano wa aina yeyote na watu na epuka sehemu za mikusanyiko.

Mwisho kabisa, ili kuwasaidia wajawazito kuwa na ujauzito wenye afya na kinga ya mwili nzuri katika kipindi hiki, ni vizuri kuzingatia mlo bora wenye madini chuma kwa wingi (kama mboga za majani zenye kijani kilichokolea, samaki na mayai) na madini ya foliki ambayo yanapatikana kwenye maharage, kunde, maharage ya kijani n.k. Bila kusahau vidonge vya vitamini vya kila siku ulivyoandikiwa na daktari wako vinasaidia pia.

Je, ninaweza kumpatia mtoto wangu Virusi vya Corona?

Je, kuna uwezekano wa mama mjamzito aliyepata maambukizi ya Virusi vya Corona kumpatia mtoto anayeendelea kukua ndani ya mwili wake?  Hili ni moja ya swali linalowaumiza wajawazito wengi na familia zao.

Ukweli ni kwamba kuna maambukizi mengi ya virusi, bakteria na fangasi ambayo yanaweza kupatiwa mtoto kipindi cha ujauzito, kama vile Virusi vya Ukimwi, Homa ya Manjano, Tetekuwanga, Rubela na Toxoplasmosis (maambukizi yanayosababishwa kwa kula nyama isiyopikwa vizuri na iliyogusana na kinyesi cha paka).

Hakuna ushahidi unaoonyesha Virusi vya Corona vinaweza kumpata mtoto aliye tumboni kama mama mjamzito anayo maambukizi. Ila kwa sababu virusi hivi ni vipya wanasayansi wanaendelea kuusoma ugonjwa huu taratibu na tutegemee taarifa zaidi hapo mbeleni.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la kujitegemea la Kidaktari liitwalo “The Lancet” ambalo liliwafuatilia wanawake 9 waliopatikana na maambukizi ya virusi hivi baada ya kufanyiwa vipimo nchini China, waligundua hakuna mtoto hata mmoja aliyezaliwa na maambukizi haya (ikumbukwe wanawake hawa wote walijifungua kwa njia ya upasuaji). Ijapokuwa idadi ni ndogo ila inatia matumaini.

Pia hakuna ushahidi ulioonyesha kulikuwa na virusi ndani ya kimiminika cha amnion “Amniotic fluid” hichi ni kimiminika kinachomzunguka na kumlinda mtoto wakati wa ujauzito. Pia hakuna ushaidi uliopatikana ndani ya sampuli za damu zilizochukuliwa kutoka katika kitovu cha kila mtoto. Hali hii inaweza kupendekeza kujifungua kwa njia ya kawaida kwa mjamzito aliye na maambukizi ni njia salama, lakini hatuna majibu ya uhakika kuhusu hili kwasababu idadi ya tafiti zilizofanywa ni ndogo sana.

Kwa tafiti zote hizi inaonyesha kuna ushahidi kidogo kuwa watoto wanaweza kupata maambukizi ya virusi hivi kutoka kwa mama zao wakati wa ujauzito.

Je, ninaweza kumpatia mtoto wangu maambukizi kwa njia ya kunyonyesha?

Hakuna uwazi wa kutosha katika suala la maziwa ya mama, hata hivyo hatuwezi fanya hitimisho kama maziwa ya mama yanabeba virusi au la!

Baadhi ya virusi, kama virusi vya UKIMWI vinajulikana kuenezwa kwa njia ya maziwa ya mama, lakini mpaka tulipofikia hakuna ushahidi kuwa Virusi vya Corona COVID-19 vinaweza kuenezwa kwa njia hii pia.

Ushauri uliopo ni kuwa wamama ambao hawana maambukizi haya waendelee kuwanyonyesha watoto wao ila wakumbuke kunawa mikono yao vizuri kabla na baada ya kuwanyonyesha.

Ikiwa mama ataonekana na dalili za kukohoa au joto kubwa la mwili, ni vizuri atumie njia mbadala ya kunyonyesha (mf: vifaa maalumu vya kukamua maziwa) na kumpatia mtu mwingine asiye na maambukizi kumlisha mtoto mpaka atakapo pona.

Kuna ushahidi wa kutosha kuwa maziwa ya mama ni mazuri kwa kuongeza kinga mwili ya mtoto, hivyo kusitisha moja kwa moja kumnyonyesha mtoto wako kunaweza kumuweka katika  hatari ya kupata maambukizi kwa urahisi.

Kadiri muda unavyokwenda, haitaepukika na tutarajie kushuhudia wanawake wengi wajawazito wakipata virusi vya corona COVID-19, hii itapelekea wanasayansi kuweza kutambua zaidi jinsi kirusi hiki kinafanya kazi na ni kwa namna gani kinamuathiri mjamzito. Kwa sasa kuchukua hatua za kujikinga ni muhimu – kuosha mikono kwa maji tiririka, kuepuka kukaa karibu karibu sana ikiwemo kuepuka maeneo yenye mikusanyiko ya watoto, kukaa nyumbani, kuepuka wageni ni njia zinazohitaji kufuatwa kuweza kuwa salama.

 

IMEPITIWA: 19 MARCH 2020

 

 

Begi la Hospitali Unapokwenda Kujifungua

Nini cha kufungasha kwenye begi la hospitali?

Sasa ni wakati wa kukusanya vitu muhimu utakavyohitaji wakati wa uchungu na kujifungua na baada ya mtoto kuzaliwa, hivyo andaa begi lako wakati unakaribia wiki ya 36 ya ujauzito. Hospitali zinaweza kutofautiana kanuni na sheria za kipi unapaswa kubeba na kipi hakiruhusiwi,wasiliana na mkunga wako kufahamu mambo muhimu ya kuongeza kwenye orodha ya mahitaji ya begi la hospitali.

Ni nini nifungashe kwaajili ya uchungu?

Mpango wa kujifungua na kumbukumbu za uzazi ulizoandika pembeni. Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia mama unaopatikana kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya serikalini nchini kwa bei ya shilingi 21000/=. Mfuko huo una:

  • Mipira ya mikono (surgical gloves 4 pairs)
  • Taulo ya kike ya uzazi (maternanity pad)
  • Pamba kubwa (cotton wool gm.500)
  • Nguo ya mtoto (cloth material for new born)
  • Vibana kitovu (2 umbilical cord clamp)
  • Mpira wa kuzuia uchafu
  • Nyembe za kupasulia(surgical blades0
  • Nyuzi za kushonea
  • Bomba la sindano
  • Dawa ya kuongeza uchungu (Misoprostol)

 

Pia ni vyema kufungasha vitu vifuatavyo: 

  • Gauni (dera) ambalo litakusaidia wakati unaugulia uchungu ukiwa unazunguka korido za hospitali. Pia utahitaji lingine baada ya kujifungua, na vema likawa lepesi.
  • Kandambili au malapa rahisi kuvaa na kuvua.
  • Soksi, amini usiamini unaweza hisi baridi miguuni wakati wa uchungu.
  • Gauni lililochakaa kidogo(kuukuu) ya kuvaa wakati wa kujifungua. Haina haja ya kununua gauni jipya wakati wa kujifungua maana unaweza kuchafuka sana wakati uko chumba cha kujifungulia.
  • Mafuta laini(mafuta ya nazi au nyonyo) ya kupaka mwilini ikiwa utapendelea kukandwa wakati wa uchungu.
  • Mafuta maalum(lip balm) ya kupaka midomo, midomo yako inaweza kukauka haraka wakati uko chumba cha kujifungulia.
  • Vinywaji au vitafunio kwaajili yako wakati uko kwenye uchungu. Vinywaji vya kuongeza nguvu ni vizuri au unaweza kutumia glukosi kukusaidia kuendelea.
  • Vitu kama jarida, kitabu au kompyuta ndogo vya kukusaidia kujiburudisha au kukusaidia muda kwenda.
  • Kama una nywele ndefu, vibanio maalumu vya kubana nywele ni muhimu.
  • Mito,ikiwa hospitali inaruhusu, ni vyema kubeba mito ya ziada kutoka nyumbani itakayokusiadia kusikia nafuu.
  • Kama muziki ni moja ya kiburudisho chako ni vyema kubeba simu yenye chaji ya kutosha au “MP3 player”.

 

Mwenza wangu wakati wa kujifungua afungashe nini?

  • Kimiminika cha kupunguza joto (water spray) au feni ya mkononi ya kupunguza joto wakati ukiwa kwenye chumba cha kujifungulia.
  • Viatu salama na vyepesi vya kuvaa wakati mnazunguka kwenye korido.
  • Nguo za kubadilisha.
  • Mirija ya kusaidia kukunywesha maji au kinywaji chochote wakati wa uchungu.
  • Simu na chaja. Simu yenye “stopwatch” au “timer” inaweza kusaidia kujua baada ya muda gani mibano ya misuli ya uterasi (contractions) itaatokea. Mibano ya misuli ya uterasi (contractions) hutokea kwa muda na kurudia tena baada ya muda wakati wa kujifungua. Au kama simu ni ya kupapasa kuna “app” maalumu za kuweza kufanya kazi hii.
  • Kamera ya kidigitali au kamera ya simu, kwaajili ya kuchukua picha au video fupi kama utapendelea wakati wa kujifungua au mda mchache baada ya mtoto kuzaliwa.
  • Vitafunwa na vinywaji. Hutapendezwa msaidizi wako wa kujifungua akiwa na njaa au kiu mbele yako. Akifungasha kinywaji na kitu cha kula ataweza kukaa na wewe zidi kuliko kutoka na kutafuta chakula

Ni nini nifungashe kwaajili ya baada ya kujifungua?

  • Nguo ya kwenda nyumbani. Utahitaji nguo nyepesi na isiyobana kuvaa wakati ukiwa hospitalini na safari ya kwenda nyumbani. Itachukua mda tumbo lako kurudi kama awali, hivyo utahitaji kuvaa nguo za uzazi kwa muda.
  • Muongozo jinsi ya kuanza kunyonyesha,ambayo utaupata wakati wa kliniki za awali na mkunga wako.
  • Sidiria za kunyonyeshea, fungasha mbili au tatu.
  • Vitambaa malumu vya kukinga maziwa yasimwagike.
  • Pedi za uzazi au vitambaa maalumu ambavyo vinaweza kusaidia.
  • Gauni la kulala ambalo linafunguka mbele,litakusaidia siku za kwanza wakati wa kunyonyesha.
  • Mahitaji ya kuoga na usafi wa mwili kama sabuni, mafuta, mswaki na dawa ya mswaki, manukato mapole ya makwapani(deodorant).
  • Taulo na chanuo.
  • Chupi za zamani au chupi za kutupwa baada ya kutumika. Chupi mpya na nzuri zinaweza kuchafuka sana wakati wa kujifungua. Chupi kubwa za pamba ni nzuri hasa kama utafanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua, hazitasugua na kutonesha kidonda.

Nifungashe nini kwaajili ya mtoto?

  • Nguo tatu au nne za kulala na vesti.
  • Blanketi la mtoto, jaokua hospitali inaweza kuwa na joto, mtoto wako atahitaji blanketi kama kutakua na baridi wakati wa kuondoka.
  • Vitambaa vya kumfuta mtoto akicheuwa.
  • Jozi moja ya soksi.
  • Nguo moja kwaajili ya kusafiria kurudi nyumbani.

Manunuzi Muhimu Kipindi cha Ujauzito Unapokaribia Kujifungua

Manunuzi kwa ajili ya mtoto mchanga

Mahitaji muhimu kwa ajili ya mtoto mchanga katika tarehe za mwanzo katika mwezi aliozaliwa tangu siku ya kwanza.

  1. Mahitaji ya mlo

Ni wazo zuri kama utamnyonyesha mwanao. Lakini kutokana na maisha ya sasa akina mama wengi wanapendelea  kumtengenezea mlo  tofauti  utahitaji kufuata kanuni, mahitaji hayo ni kama:

  • Maziwa ya unga
  • Chupa 6 za maziwa
  • Kiosha chupa na begi la kuhifadhia
  • Brashi ya kusafisha chupa pamoja na maji ya uvuguvugu
  • Eproni
  • Mto
  • Kitambaa cha kumkinga mtoto akicheua

Kama utaamua kumlisha maziwa yako kwa chupa utahitaji kitu cha kukamulia maziwa na vifaa vingine kama kiosha chupa na begi la kuhifadhia. Kusafisha chupa kwa majimoto ni muhimu sana hasa katika chupa anazotumia mtoto. Unapaswa kusafisha vema hizo chupa ili kuepuka kubeba uchafu  na maambukizo mengine yanayotokana na uchafu wa muda mrefu.

  1. Mavazi ya msingi

Kwa siku za mwanzo mtoto atahitaji mavazi mengi, hivyo hakikisha umenunua mavazi ya kutosha. Zingatia yafuatayo unaponunua mavazi kwa ajili ya mtoto;

  • Nguo za kipimo chake ingawa anakua kwa haraka
  • Ovaroli zenye mikono mirefu na mifupi ambazo zina vifungo katikati
  • Gloves 2 za mikono ili kumlinda mtoto asijikwaruze
  • Jozi 6 za viatu na soksi pamoja na nguo za kulalia
  • Jozi 6 za nguo za kutokea unapokwenda kuwaona ndugu na marafiki.
  • Kofia 2 za pamba kumlinda mtoto masikio na kichwa kipindi cha baridi.
  • Kwa kutegemea hali ya hewa, nunua jozi 2 za sweta au jaketi.

Nguo za mtoto zisafishwe na kuhifadhiwa sehemu salama kuzilinda kutokana na uchafu.

  1. Malazi

Pindi tuu unaporudi nyumbani mtoto wako atahitaji sehemu ya kupumzikia , unaweza kuchagua sehemu kwa ajili yake pembeni ya kitanda chako. Hakikisha umepata mpangilio wa kitanda kabla ya kichanga  kufika nyumbani. Uangalizi uchukuliwe kabla ya kununua neti,  hakikisha unapata bora na salama. Mahitaji sahihi katika kitanda cha mtoto ni;

  • Kitanda chenye ubora
  • Shuka2 hadi 3 za kufiti
  • Shuka3 hadi 4 zisizopitisha maji
  • Blanketi 3 za pamba

Kama utaenda kuazima au kununua kwa mtumba ni vema kuangalia zilizo bora.

  1. Mahitaji muhimu ya usafi wa mwili

Vifaa kwa ajili ya kumfanya kichanga awe salama na huru wakati wa kuoga. Utalazimika kuwa na vitu vifuatavyo;

  • Kuandaa sehemu salama kwa ajili ya kuoga, utatakiwa kununua beseni.
  • Taulo 2 za kuogea na pakiti 2 za sabuni ya kufulia nguo za mtoto
  • Shampuu ya mtoto na sabuni ya kumuogeshea mtoto wako
  • Losheni na mafuta ya kumpaka mtoto baada ya kuoga
  • Brashi ya kuchania nywele au seti ya vitana na vikatia kucha
  • Usimpulizie manukato mtoto mwilini.

Changamoto za Kupata Ujauzito kwa Wanawake Wenye Umri Zaidi ya Miaka 35

Moja ya sababu inayoleta matatizo ya kuzaa pale umri unapokua mkubwa ni kupevushwa yai mara chache kuliko kawaida. Kadiri wanawake wanapoendelea kukua mizunguko yao ya hedhi inaanza kubadilika na mayai kushindwa kupevushwa kwa wakati. Idadi ya mayai na ubora wa mayai unapungua, mwanamke anapofika umri kati ya miaka 30 mpaka 40. Utafiti unaonyesha ubora wa mayai unaweza kuongezwa ihali idadi yake haiwezi kuongezeka. Virutubisho vya “myo-inositol”, asidi ya foliki na “melatonin” vimeonyesha kuongeza ubora wa mayai na kazi za mfuko wa mayai.

Sababu nyingine zinazofanya kupata ujauzito baada ya miaka 35 kuwa vigumu ni pamoja na:

  • Maambukizi au upasuaji uliosababisha kovu kwenye tishu maeneo yanayozunguka mfuko wa mimba,mirija ya falopiani au mlango wa kizazi cha mwanamke.
  • Ugonjwa wa “endometriosis”.
  • Uvimbe katika mfuko wa uzazi.
  • Upungufu wa uteute ndani ya mlango wa kizazi.
  • Magonjwa ya kudumu/sugu kama shinikizo la damu au kisukari.

Kuharibika mimba pia ni tatizo kubwa kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35. Hii inasababishwa na ongezeko la mabadiliko ya jenetiki za uumbaji. Wanawake wenye umri kati ya miaka 35-45 wana nafasi kati ya asilimia 20-35 ya mimba kuharibika

Ni nini nifanye niongeze nafasi ya kuzaa baada ya umri wa miaka 35?

Kujaribu kujifungua baada ya miaka 35 linaweza kuwa jambo la kuelemea, lakini kuna mambo mengi ya kufanya kukusaidia kushika ujauzito haraka.Yafuatayo ni mambo ya kukumbuka:

  • Andaa ratiba ya kuonana na mtaalamu wa uzazi – wewe pamoja na mshauri wako wa afya mnaweza kupitia historia ya matibabu yako, matibabu ya sasa na maisha yako kwa ujumla. Kwa kufanya hivi, kunasaidia kuyagundua matitizo na wasiwasi wowote hasa unapojiandaa kupata ujauzito baada ya miaka 35.
  • Wanawake wenye umri mkubwa wanachukua mda kupata ujauzito – kuwa na imani pale unapochelewa kupata ujauzito, kumbuka wastani wa namba ya kupata ujauzito kwa wanandoa walio na umri zaidi ya mika 35 ni 1-2 kwa mwaka.
  • Mwanamke aliye na afya kimwili,kiakili na kihisia anaweza kupata ujauzito – pombe,sigara na matumizi ya kahawa(vinywaji vyenye kafeni) zinaweza kupunguza nafasi ya wewe kupata ujauzito. Pia kuwa na uzito mdogo au mkubwa sana inaweza kuingilia ufanyaji kazi wa homoni.
  • Angalia ishara za mwili wako zitakazo kusaidia kujua wakati gani ni wa kufanya ngono ili kupata ujauzito – rekodi jotoridi la mwili na majimaji ukeni ili kujua muda muafaka wa kufanya ngono. Ishara hizi zitakusaidia kujua ni wakati gani yai linapevushwa ndani ya mwili wako na kama yai lako linapevushwa kwa wakati.
  • Mtembele mshauri wako wa afya kama hujafanikiwa kupata ujauzito baada ya miezi sita ya kufanya ngono – Kutana na mshauri wako wa afya kujadili uwezekano wa kupima uwezo wako wa kupata ujauzito. Kwa wakati huu unaweza kumtembelea mtaalamu wa maswala ya uzazi.

Tumia kirutubisho chenye myo-inositol (virutubisho vinavyotumika kutibu watu wenye uvimbe kwenye mfuko wa mayai) kukusaidia kuboresha mayai yako.

Ratiba za Kliniki kwa Mama Mjamzito

Wiki ya 8-12

 Miadi yako ya kwanza ya kliniki inatakiwa kuchukua nafasi wiki ya 10 ya ujauzito ili mkunga wako akufanyie vipimo na uchunguzi mapema kama anahisi ni lazima. Ila inaweza fanyika kati ya wiki ya 8 na 12.

Katika miadi hii, mkunga atakuuliza:

  • Historia yako ya matibabu
  • Unajisikiaje
  • Mlo na maisha yako
  • Kazi yako
  • Wapi ungependa ujifungulie
  • Kama utaendelea kumnyonyesha mwanao

Mkunga wako atakupatia taarifa nyingi. Na atakueleza:

  • Virutubisho gani unapaswa kutumia
  • Faida za uzazi ambazo utakuwa nazo
  • Uchunguzi wa magonjwa ya akili
  • Lini utarajie kipimo cha “ultrasound”
  • Faida na hatari ya baadhi ya vipimo, uchunguzi na vitendo-tiba.

Utapata nafasi nyingi za kuuliza maswali na kuongelea tatizo lolote linalokupa wasiwasi. Ingependeza zaidi kama ukitengeneza orodha ya mambo unayotaka kuuliza kabla ya miadi yako.

Mkunga wako atakuuliza kama anaweza kuchukua damu yako, ambayo itatumika kuangalia kundi la damu yako, viwango vya madini ya chuma na pia kuangalia kama kundi lako la damu ni resusi chanya au hasi (rhesus status), na kama una antibodi au la.

Watahitaji sampuli ya mkojo wako katika miadi hii na kila miadi na mkunga wako. Atapima kama mkojo wako una protini ikiwa ni dalili ya kifafa cha mimba, na atapima maambukizi ya mkojo. Atakupima shinikizo la damu, uzito na urefu.

Mwisho wa miadi utapewa taarifa za uzazi kuenda nazo nyumbani mpaka miadi yako ijayo. Wakati huu pia unaweza ukafunguliwa kadi yako ya kliniki ya mama mjamzito.

Wiki 10-14

Picha yako ya “ultrasound” itakua tayari. Mtaalamu wa ultrasound atachunguza ukuaji wa mwanao na kuhakikisha siku ya kujifungua kwako. Atakuambia pia kama una mtoto zaidi ya mmoja.

Wiki 15-20

Utapatiwa kipimo cha damu kuangalia viwango vya protini na homoni katika damu yako ili kuangalia kama mwanao ana magonjwa ya kurithi ya akili. Kama majibu yataonyesha mtoto wako anaweza akawa na magonjwa ya akili, matibabu ya haraka yataanza kufanyika kwa mtoto aliye ndani ya tumbo.

Wiki ya 16

Mkunga wako atajadiliana na wewe matokeo ya kipimo cha damu na mkojo vilivyofanyika katika miadi yako ya kwanza (wiki ya 10). Kama kiwango cha chuma ni kidogo, anaweza kukushauri kutumia virutubisho vya chuma.  Na kama ana wasiwasi wowote, atakupeleka kwa mtaalamu wa mambo ya uzazi kwa huduma ya ziada.

Mkunga wako ataangalia shinikizo lako la damu na kuchukua sampuli mpya ya mkojo wako kuangalia kama kuna uwepo wa protini,na atafanya hivi kila mara ukienda kumwona.

Na kwa kila miadi, ni muda mzuri wa kuuliza maswali na kuongea tatizo lolote linalokupa wasiwasi.

Wiki ya 18-21

Uchunguzi (scan) ya kasoro za ukuaji utafanyika. Uchunguzi utaangalia jinsi mtoto anavyokua na kwa baadhi ya hospitali zitakuambia jinsia ya mtoto wako kama ungependa kujua.

Wakati mwingine kondo la nyuma (plasenta) huziba mlango wa uzazi, na kufanya ugumu kupata vipimo sahihi wakati wa kipimo cha skani. Kama hii imetokea kwako utapangiwa muda mwingine wa kipimo.

Wiki ya 25 (kwa mimba za kwanza tu)
Kama kawaida mkunga wako ataangalia shinikizo la damu na kupima mkojo wako kama kuna protini. Pia atapima umbali kutoka mfupa wa sehemu za siri mpaka juu ya tumbo lako na tepu kuangalia kama mtoto wako anakua vizuri.

Wiki ya 28

Mkunga wako watachukua sampuli ya damu katika miadi hii. Hii itatumika kuhakikisha viwango vya chuma ni vya kawaida na kuandalia kingamwili. Iwapo una kiwango kidogo cha chuma, atashauri uchukue virutubisho vya chuma atakayokuandikia.

Kwa kila miadi kuanzia sasa, mkunga atakupima tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri. Ataangalia pia shinikizo la damu na kupima mkojo wako kama kuna protini.

Wiki ya 31 (wenye ujauzito wa mara ya kwanza)

Mkunga atakupima tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri. Ataangalia pia shinikizo la damu na kuima mkojo wako kama kuna protini. Atakupatia majibu ya vipimo vya damu vilivyochukuliwa wiki ya 28.

Upate pia mda wa kuuliza maswali, kama unayo na kujadiliana masuala yanayohusiana na afya yako.

Wiki ya 32

Uchunguzi wa kasoro (anomaly scan) uliofanyika wiki ya 18 lakini majibu hayakuonekana vizuri kwasababu wakati mwingine kondo la nyuma au kirutubisho mimba (plasenta) ilikuwa inaziba mlango wa uzazi, na kufanya ugumu kupata vipimo sahihi wakati wa kipimo cha skani unaweza ukarudiwa tena kipindi hiki. Sasa ni wakati mwingine wa kufanya kipimo hichi.

Wiki ya 34

Mkunga atakupima tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri. Ataangalia pia shinikizo la damu na kupima mkojo wako kama kuna protini na kupima ukubwa wa tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri ndani ya tumbo lako.

Kama huu ni ujauzito wako wa pili, mkunga wako atakupa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa wiki ya 28. Kama atakua na wasiwasi atajadiliana na wewe. Pata nafasi ya kuongea na mkunga wako kuhusu matayarisho ya uchungu na kuzaa. Mkunga atakuelezea hatua za kujifungua na lini utapata uchungu.

Wiki ya 36

Mkunga wako atafanya vipimo na uchunguzi wa kawaida. Atashika tumbo lako kwa mkono kuangalia mlalo wa mtoto wako.

Baadhi ya watoto wengi watakua wamegeuka kichwa chini katika wiki ya 36, tayari kwa kuzaliwa. Kama mtoto wako bado hajageuka, mlalo wa kutanguliza matako. Mkunga wako atakupa miadi mingine ili huduma ya kumgeuza mtoto huku mimba ikiwa inaendelea kukua ifanyike.

Sasa umekaribia miezi tisa, mkunga wako ataanza kuzungumzia nini kitatokea baada ya mtoto kuzaliwa. Ataelezea vipimo na uchunguzi vitakavyofanywa kwa mtoto wakati ukiwa hospitali na wakati ukienda nyumbani.

Wiki ya 38

Mkunga atakupima tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri. Ataangalia pia shinikizo la damu na kupima mkojo wako kama kuna protini na kupima ukubwa wa tumbo lako kuangalia kama mtoto anakua vizuri ndani ya tumbo lako. Mkunga wako ataanza kukuelezea kwa undani kama mimba yako itachukua mpaka wiki 41.

Utaanza kupata hofu na wasiwasi ukifikiria siku ya kwenda kujifungua. Ondoa shaka kwasababu mkunga wako atafurahi sana kuongea na wewe kuhusu wasiwasi wako na kujibu maswali yote.

Wiki ya 40 (wajawazito wa mara ya kwanza)

Mkunga wako atakupima ukubwa wa tumbo lako na kupima shinikizo la damu na kipimo cha mkojo kama kawaida. Ni wakati mzuri kuongelea wakati gani ni wa kwenda hospitali kujifungua na nini kitatokea baada ya mtoto kuzaliwa.

Kama uchungu wako haujaanza ni wakati mzuri wa mkunga kukufanyia huduma itakayosaidia kuanzisha uchungu kwa kuingiza vidole vyake ukeni taratibu na kuvizungusha kwa ukakamavu (membrane sweep)

Wiki ya 41

Kama hakuna dalili yeyote ya uchungu mpaka wiki ya 41, mkunga wako atakupatia huduma ya “membrane sweep” (kuingiza vidole taratibu ndani ya uke wako na kuvizungusha kwa ukakamavu) ili kuuanzisha uchungu. Kama ulifanyiwa huduma hii wiki ya 40 unaweza kuchagua kama unataka kufanyiwa mara ya pili au la. Mkunga wako atakupima shinikizo la damu na vipimo vya mkojo kama kawaida, pia atapima ukubwa wa tumbo.

Kufikia wakati huu mkunga wako atakuandalia huduma nyingine ya kuanzisha na kuchochea uchungu iitwayo “induction” (hii inasaidia kuchochea mikazo ya ukuta wa kizazi wakati wa kujifungua badala ya kusubiria uchungu kuja, mkunga atakupatia dawa au huduma ya kimatibabu) huduma hii itafanyika pale “membrane sweep” imeshindikana. Ikiwa umechagua kuendela kusubiri na ujauzito wako ukafika wiki ya 42 au zaidi,utaangaliwa kwa karibu zaidi, ikiwemo kufanyiwa kipimo cha “ultrasound” na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto.

Fahamu Mambo Muhimu ya Kufanya Katika Kila Hatua ya Ujauzito

Hatua ya kwanza: Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito

1. Panga kuonana na mkunga wako

Mara baada ya kujua una ujauzito, mjuliswhe daktari wako ili uweze kupanga kuonana naye. Kwenda na wakati ni jambo la msingi pindi unaonana na daktari, inategemea unaishi wapi na lazima uwe umepanga kuonana na daktari wakati una ujauzito wa wiki 10, lakini inaweza kutokea wiki ya 8 au 12.

Kuonana na daktari inaweza ikachukua masaa 2 ikiwa ni nyumbani, kliniki au chumba cha upasuaji. Wakati umeonana na daktari unaweza kufanya yafuatayo;

  • Akakuuliza kuhusiana na historia ya matibabu yako, ikiwemo ujauzito uliopita na jinsi ya maisha yako.
  • Akakupa taarifa kuhusu namna ya kujihudumia wakati wa ujauzito kama vile kula vizuri na kufanya mazoezi.
  • Akakupima shinikizo la damu (presha)
  • Akakupima uzito na urefu, atachukua vipimo hivi ili kuweza kujua hali ya uzito wako kiafya (BMI)
  • Akachukua vipimo vingine vya mwili.

2. Tumia vidonge vya virutubisho-lishe kwa siku mara moja

Anza kula kidonge lishe cha asidi ya foliki mara moja. Asidi ya foliki ina virutubisho vya muhimu ambavyo vinamlinda mtoto asipate matatizo ya mgongo wala ubongo kama vile mgongo wazi “spina bifida”. Unahitaji mikrogramu 400 (400mcg) ya kidonge lishe cha foliki ya asidi (vitamin ya b9). Unaweza kununua vidonge hivi kwenye duka la dawa au maduka makubwa. Vivyohivyo unatakiwa kutumia vidonge vya vitamin B kila siku pia unaweza ukatumia vidonge vya vitamini za ujauzito kama unapenda, lakini kula mlo kamili utakusaidia kupata vitamini zote unazohitaji.

3. Pima kabla hujatumia madawa

Unahitaji kuwa muangalifu wakati wa kutumia dawa hasa za kununua madukani kwani zinaweza zikawa siyo nzuri kwa mtoto wako. Ongea na daktari wako kuhusiana na madawa yoyote utakayotumia au pia unaweza ukamuuliza muuza madawa kuhusiana na dawa husika.

4. Kama unavuta sigara ni muda wa kuacha

Kuvuta sigara wakati wa ujauzito siyo nzuri kwa mtoto wako unaweza kusababisha mimba kuharibika au kupata matatizo wakati wa kujifungua na pia inaweza kumletea mtoto matatizo wakati wa ukuaji. Hujachelewa sana kuacha sigara kama unahitaji msaada ongea na daktari wako anaweza kukupa msaada kwa namna ya kuacha kuvuta sigara, sigara zote huwa na nikotini, hivyo kama unatumia ongea na daktari wako namna ya kuacha.

5. Acha pombe

Hakuna njia ya uhakika kujua kama pombe ni salama wakati wa ujauzito ndio maana wataalamu wengi hushauri kuacha pombe kabisa wakati wa ujauzito.

6. Acha kunywa vinywaji vyenye kafeini

Wakati wa ujauzito unaweza kuendelea kunywa kahawa lakini punguza hadi 200mg kwa siku ambayo ni sawa na kikombe kimoja au viwili. Ikiwa unaweza kutumia zaidi ya 200gm za kafeini kwa siku wakati wa ujauzito inaweza kuongeza uwezekano wa mimba kuharibika. Kiwango cha 200mg kinajumuisha vyanzo vyte vya kafeini ikiwemo chai, cocacola, vinywaji vya kuongeza nguvu na chokoleti.

7. Jifunze nini cha kula na nini siyo cha kula

Mlo kamili utahakikisha unapata mahitaji yote yanayotakiwa kwa ajili ya ukuaji wa mtoto. Inaweza ikakushangaza kujua kwamba unahitaji nguvu nyingi miezi mitatu ya kwanza au miezi mitatu ya pili. Lakini utatakiwa uache baadhi ya vyakula wakati wa ujauzito kwani inaweza ikawa na vijidudu au sumu ambayo inaweza kumdhuru mtoto, hii inaweza ikajumuisha vyakula vya maziwa, nyama ambayo haijaiva kama maini na samaki wabichi.

8. Pata ahueni katika magonjwa (magonjwa ya asubuhi) yanayoambatana na ujauzito

Wamama wengi wanapata magonjwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Kula kidogo lakini mara nyingi, jaribu kutambua vyakula gani vinakufaa na vipi havikufai. Kula vyakula kama biskuti, karanga, mkate vinaweza kusaidia. Kuumwa kwako kutaanza kupungua kuanzia wiki ya 16 mpaka 20. Kama unatapika mara nyingi kwa siku wasiliana na daktari wako mapema iwezekanavyo, unaweza ukawa na ugonjwa unajulikana kama “hyperemesis gravidarum” unaohusisha kupata kichefichefu kilichopitiliza na kutapika sana.

9. Tambua ishara hatarishi

Kuna baadhi ya ishara wakati wa ujauzito ambazo ni hatari kwako na sio za kupuuza. Wakati tumbo la uzazi linakua utaanza kuhisi vichomi na nyonga kuuuma, kila mara jaribu kuwasiliana na daktari wako.Kama utakuwa na vichomi vinavyoambatana na damu wasiliana na daktari wako mapema iwezakanavyo.

10. Pata Mapumziko yakutosha iwezekanavyo

Ni kawaida kuhisi uchovu wakati wa miezi mitatu ya kwanza. Hii ni kwasababu mwili wako unapata mabadiliko mengi ya haraka ya homoni na viwango vyake. Weka miguu juu ukiwa na nafasi ingawa hii huweza kuwa ngumu kama unafanya kazi. Jaribu kupanda kitandani mapema japo mara moja katika wiki. Hatakama hutaweza kulala mpaka baadae kupumzika na kitabu au mziki laini itasaidia kukutuliza. Zima simu na sahau kuhusu kazi. Mtoto akija usingizi utakua mgumu kupata kwahiyo jaribu kuupata vyema kwa kipindi hiki. Ni vyema ukaanza kujizoesha kulala na ubavu kwani jinsi tumbo lako linavyokua utashindwa kulala kwa tumbo au mgongo. Kwani ukilala na mgongo utaathiri mzunguko wa damu katika mwili wako hatahivyo mpaka miez mitatu ya mwisho kulala kwa ubavu husaidia kupunguza hatari ya mtoto mfu, ukilinganisha na kulala na mgongo. Kwahiyo ni vyema ukaanza sasa.

11. Jiandae kumwona mwanao

Kama hauna tatizo lolote katika kipimo cha ultrasound cha kwanza, kipimo hiki hufanyika wiki 10 au 14 za kwanza.Daktari wako atamwangalia mtoto mapigo ya moyo na kukwambia lini utampata mtoto wako kwani kipimo hiki huchukua dakika 20 tu au huweza kuchukua zaidi hivyo ni vyema kumsubiri mtoto ageuke.

12. Amua lini uwajulishe watu kuwa wewe ni mjamzito

Baadhi ya wanawake hupenda kuwaambia ndugu zao na marafiki kuwa ni wajawazito papo hapo wengine husubiri mpaka miezi mitatu ya pili kwani tumbo halifichiki. Kama umepata matatizo au kazi yako ni hatarishi na inachosha ni vema ukawaambia mapema.

13. Mazoezi

Mazoezi ya mara kwa mara huweza kusaidia mahitaji ya kimwili na kiakili. Hakuna sababu ya kukuzuia kufanya mazoezi ikiwa wewe ni mjamzito, kufanya mazoezi kutakusaidia kupata wepesi na kuwa mchangamfu.

14. Fanya kazi zako kiusalama

Kuwa muangalifu na kemikali za kusafishia nyumba, vaa kinga muhimu kuzuia hatari wakati unatumia kemikali hizi hatarishi na wakati unafanya usafi fungua madirisha yako na milango. Kumbuka ujauzito unaweza ukaathiri utendaji kazi wako, hasa kama unafanya kazi na x-ray au kemikali.

15. Anza kufanya mazoezi ya nyonga

Mazoezi ya nyonga yanaweza kusaidia kuzuia kuvuja kwa mkojo wakati wewe ni mjamzito na baada ya mtoto kuzaliwa. Kama hujaonyeshwa namna ya kufanya mazoezi ya nyonga wakati umeonana na daktari basi muulize unapoenda kuonana naye tena.

16. Muhusishe mwenza wako

Wamama wengi watarajiwa kupata uzoefu mapema wakati wa ujauzito, mazoezi wakati wa ujauzito yanasaidia kuunganika na mtoto tangu akiwa tumboni.

17. Nunua sidiria ya uzazi

Maziwa yaliyojaa yanaweza yakawa ishara mojawapo ya kuwa wewe ni mjamzito na kama sidiria zinakuumiza fikiria njia mbadala.

18. Fanya mapenzi kama una hamu

Kama miezi mitatu ya kwanza unajihisi umechoka basi usifanye mapenzi lakini kama hujapata matatizo yoyote hakuna sababu ya kuacha kufanya kipindi chote cha ujauzito.

19. Fanya “massage”

Kuna unapata matatizo ya kuumwa kichwa mgongo au unataka tuu upumzike basi nenda kafanye “massage” ya wajawazito au muombe mwenza wako akukandekande mabega, mgongo na kichwa kupunguza maumivu.

20. Fanya bajeti kwa ajili ya mtoto

Anza kufikiria kuhusu namna gani utamuhudumia mtoto kama vile nguo,chakula, nepi(diapers) nk.

Hatua ya pili: Miezi mitatu ya pili ya ujauzito

1. Jifunze kuhusu kipindi hiki na ratiba ya kumuona daktari

Katika wiki ya 16 daktari wako na mkunga wako watakuambia kuhusu vipimo vitakavofanyika ukiwa wiki ya 18 au 21 na kipimo hichi kitaangalia namna mtoto anavyokua. Utaenda kumuona daktari wiki ya 25 na 28 kujua ukubwa wa mfuko wa uzazi na kupima shinikizo la damu (pressure) na kuangalia kama umeathirika na ugonjwa wowote ikiwemo UTI.Lakini miezi mitatu ya pili utapata vipimo hivi kila mara uendapo hospitali.

2. Amua kama unataka kujua jinsia ya mtoto

Je ni wa kike au wa kiume? Wakati wa kipimo ni rahisi kujua jinsia ya mtoto kama hajifichi kwa mpimaji.

3. Mwanao akisogea kwa mara ya kwanza

Katika wiki ya 18 na ya 20 ya ujauzito utaanza kumsikia mwanao akisogea ndani ya mfuko wa uzazi. Kama ni ujauzito wako wa kwanza inaweza ikakuchukua muda kuweza kutambua mtoto akisogea.

4. Chagua mzazi mwenzako

Katika kipindi cha miezi mitatu ya pili ni wakati mzuri wa kujua unataka nani awepo wakati wa kujifungua, kuwa na mtu anayekusaidia anaweza akafanya mabadiliko makubwa hasa wakati unakaribia kupata mtoto.Mzazi mwenzako siyo lazima awe baba mtarajiwa, anaweza akawa rafiki, mama yako au mama mkwe.Unaweza ukawa na wazazi wasaidizi zaidi ya mmoja.

5. Angalia kuongezeka kwa uzito wako

Ni kawaida kuongezeka uzito kidogo wakati wa ujauzito. Kula mlo kamili kutahakikisha unaongezeka uzito kidogo, kadiri mtoto anavyokua . Angalia namna uzito wako unavoongezeka. Pumzisha mwili na akili yako wakati wa ujauzito kwa kufanya mazoezi malaini kama yoga.

6. Kunywa maji ya kutosha

Wakati wa ujauzito ni muhimu kunywa maji, ni vizuri kunywa japo glasi 8 ambayo ni sawa na lita 1.5 kila siku, jaribu kutembea na chupa ya maji kila uendapo.Maji husaidia kubeba mahitaji ya muhimu kwenye damu kwenda kwa mtoto. Kunywa maji pia husaidia kuzuia magonjwa kama maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI), kuvimbiwa nk. Yote ni kawaida wakati wa ujauzito.Kama una tatizo la mwili la kutunza maji (oedema) kunywa maji ya kutosha kwani husaidia kutunza maji mwilini.

7. Panga muda wa mapumziko

Muda wa mapumziko unaweza ukapunguza matumizi ya hela na muda. Miezi mitatu ya pili ni kipindi muhimu cha kupumzika, kwa kawaida kichefuchefu kinakua kimeisha na uchovu utakua umeisha. Ni salama kusafiri kwa ndege wakati wa ujauzito mpaka wiki ya 36.

8. Chagua jina la mtoto

Kwa sasa tayari utakua na majina machache unayodhani yanaweza kumpendeza mwanao na pia ni vema umshirikishe mwenzi wako. Chagua idadi ya majina kumi unayoyapenda wewe na mwenzi wako, alafu futa yale usioyapendelea, endelea mpaka mtakaporidhia majina machache.

9. Anza manunuzi ya nguo za uzazi

Kama tumbo bado halijaanza onekana, ni vizuri kuanza kununua nguo za uzazi, nunua kidogo sasa na nyingine baadae tumbo linavozidi kukua.

10. Anza kutafuta huduma kwa mtoto

Ni vema kuanza fikiria kuhusu huduma kwa mtoto hata kama unadhani bado muda ni mrefu, tafuta vipeperushi vya watoa huduma kwa watoto. Anza kufanya utafiti wa mtu wa kumuangalia mtoto na kukusaidia mara baada ya kujifungua na ulizia watoa huduma wazuri mtaani kwako.

11. Muandae dada mtu au kaka mtu kwa ndugu anayekuja

Kama una mtoto tayari ni vema ukamuandaa kwa ujio wa mdogo wake, mwambie kwamba kuna mtoto anayekuja na ikiwezekana nenda naye kwa daktari wako.

12. Tembelea daktari wa meno

Ni vema kufanya hivi kwani muongezeko wa homoni mwilini unaweza kuathiri meno yako na fizi zinaweza kuvimba na kutoa damu hivyo kuna nafasi kubwa ya kupata maambukizi wakati huu.

13. Sherehekea nusu ya kipindi cha ujauzito

Katika wiki ya 20 ni nusu ya kipindi cha ujauzito hivyo ni vema ukajipongeza na kufurahia kipindi hicho.

14. Lala kwa ubavu

Tumbo lako linavyozidi kukua linaongeza msukumo wa damu katika mishipa mikuu kwa hiyo haishauriwi kulala na mgongo kwani utaathiri ufikaji wa oksijeni kwa mtoto, hata hivyo miezi mitatu ya mwisho hupunguza hatari ya kujifungua mtoto mfu, ukichangia kulala kwa mgongo. Kwahiyo kama hujaanza kulalia ubavu ni vema uanze mapema.

15. Andika ndoto zako kipindi cha ujauzito

Utaanza kugundua unakumbuka ndoto nyingi kipindi hichi ni vema kuandika ndoto hizo wewe pamoja na mwezi wako.

16. Andaa mahala salama kwa mtoto

Mahali salama kwa mtoto wako ndani ya miezi sita ya kwanza ni chumba unacholala wewe, haina haja ya kuhangaika awali, unaweza omba msaada mtu mwingine akusaidie kuandaa mahitaji hayo.

17. Omba vitu vya mtoto visivotumika kutoka kwa rafiki au mwanafamilia

Kununua vitu vya mtoto inaweza ikawa gharama kubwa kwahivyo ni bora kuomba kutoka kwa rafiki au mwanafamilia (mama yako, dada yako, wifi au mama mkwe) vitu visivotumika kwa ajili ya mtoto.

18. Fikiria kuhusu likizo ya uzazi

Kama unafanya kazi ni vizuri ujue unastahili mda gani na toa taarifa kwa muajiri wako kwamba wewe ni mjamzito japo wiki 15 kabla mtoto hajazaliwa na umuombe akuandikie likizo ya uzazi.

19. Tuliza akili

Kama unahisi unachanganyikiwa, kuvaa nguo zilizotengenezwa kwa pamba inaweza kusaidia kukutuliza au kama kuna baridi vaa nguo ambazo ni rahisi kutoa pindi ukisikia joto.

20. Chagua mazoezi au mchezo salama

Kufanya mazoezi wakati wa ujauzito ni vizuri kwako na kwa mtoto hivyo mazoezi ya kuogelea hufanya uwe mchangamfu kipindi tumbo lako linakua, maji yanabeba uzito wako na kunyoosha misuli. Tumbo lako linavyokua mchezo wowote hatarishi hauruhusiwi.

21. Ungana na mwanao

Mwanao anaanza kusikia sauti wiki ya 23 ya ujauzito ambapo inasemekana mfumo wa kusikia unafanya kazi vizuri ili kukusaidia uungane na mwanao. Kuongea na kumuimbia mwanao ni jambo la msingi la kuwaunganisha pamoja mpaka utakapozoea.

22. Pata muda na mwenzi wako

Katikati ya maandalizi za mtoto wako unahitaji kupata muda na mwenzi wako, mnaweza  kutoka kuangalia sinema au kwenda kula au kupumzika popote, kama una watoto tayari ni vema utafute msaidizi wa kazi ili uwe na muda wa peke yako.

Hatua ya tatu: Miezi mitatu ya tatu ya ujauzito

1. Tambua kusogea kwa mtoto wako

Mtoto wako anakua kila muda na kumbuka kusogea kwake kunaongezeka kila mara. Kila mtoto ana utaratibu wake wa kutembea na kulala na wewe utatambua wa mwanao utahisi mtoto anavyosogea mpaka kipindi cha kujifungua, kama utahisi mabadiliko yoyote mtaarifu daktari au mkunga wako haraka iwezekanavyo.

2. Jifunze kuhusu miezi mitatu ya mwisho

Katika kipindi hiki mkunga wako atakuambia ujiandae kwa ajili ya kujifungua na mengine ikiwemo dalili za uchungu na namna ya kukabiliana nazo. Mkunga wako atapima ukubwa wa tumbo lako na namna mtoto anavyokua kila mtakapoonana kama kuna haja ya kipimo zaidi atakuambia.

Kama  ni mtoto wako wa kwanza na umekaribia  tarehe ya kujifungu na hakuna dalili zozote za uchungu, mkunga wako atakufanyia  huduma yenye kusaidia uchungu kuanza(membrane sweeping) .

3. Tambua dalili za ujauzito ambazo sio za kupuuzia

Kifafa cha mimba ni tatizo linalopatikana kipindi cha ujauzito wakat plasenta haifanyi kazi vizur inaweza kutokea wiki ya 20 lakini hasahasa miezi mitatu ya mwisho.Mkunga wako ataangalia dalili za tatizo hilo pindi unapoenda kumuona. Vipimo mkunga wako atakavyochukua ni vya muhimu kuweza kutumia. Ni vizuri kuweza kutambua dalili zake. Angalia sana maumivu ya kichwa, kutokuona vizuri, kutapika, kuvimba mikono na miguu wasiliana na mkunga au daktari wako haraka iwezekanavyo.

4. Kula vizuri

Katika kipindi hichi ni vizuri kula vyakula vyenye afya na vyenye kuongeza madini ya chuma, kwahiyo kula vyakula vinavyosaidia kutengeneza chembechembe nyekundu za damu ambazo zitamsaidia mwanao. Kula vyakula kama vile nyama, mboga za majani, juisi zitakazosaidia kuongeza madini hayo.

5. Nyoosha mwili

Sasa ni wakati muhimu wa kunyoosha mwili kujiandaa kujifungua, miezi mitatu ya mwisho mazoezi hayo yatakusaidia kupunguza maumivu wakati wa kujifungua.

6. Massage tumbo lako

Tumbo lako linavozidi kukua ni vema ukaanza kumjua mwanao kabla hajazaliwa, ni salama kabisa wewe au mwezi wako kulikandakanda tumbo lako kwa ustaarabu.Ni jambo la upendo kwenu kuwa karibu na mtoto wenu, na utahisi akipiga mateke au kusogea kama kukujibu kutokana na “massage” unayomfanyia.

7. Weka sawa mahitaji ya mwanao, zikiwemo nguo na vifaa

Hii ni kazi mahususi kwa mwenza wako kupanga na kuweka vizuri mahitaji ya mwanao, ni vizuri ukiwa na marafiki waliotayari kukusaidia, ukikosa usingizi ni wakati mzuri wa kuandaa mahitaji ya mwanao.

8. Ongea na mwanao

Mtoto wako anasikia sauti yako, kuongea nae ni sehemu ya kuwa karibu na mwanao, kama kuongea na mwanao unaona ni jambo la ajabu, unaweza ukasikiliza mziki, ukaimba, ukasoma kitabu kwa sauti akusikie.

9. Jifunze kuhusu hatua za uchungu

Ni vigumu kutabiri nini kitatokea lakini jambo la busara kujifunza hatua za uchungu kabla wakati huo haujafika, kitu ambacho kitakusaidia kuwa tayari kwa kipindi hicho.

10. Andaa mpango wa kujifungua

Mpango wa kujifungua ni namna ya kuwasilisha mahitaji yako kwa wakunga na daktari wako ambao wanakusaidia wakati wa uzazi. Kitu ambacho kitafanya utaratibu mzima wa kujifungua kuwa sawia, unachotaka kutokea na kitakachotokea. Unaweza pia ukaandika mambo unayohitaji ili yakusaidie wakati wa kujifungua.

11. Jua uchungu wako

Baada ya kupita nusu ya kipindi chako cha uzazi, utaanza kusikia misuli ya tumbo lako kuanza kukaza mara kwa mara kukaza inajulikana kama “Braxton hicks contractions”. Sio kila mtu anayo, ukipata misuli kukaza huku andika namna inavyotokea na kwa kipindi gani ili uweze kujua jinsi gani inatofautiana na uchungu wa kujifungua.

12. Nunua nguo kwa ajili ya mtoto wako

Anza kufikiria kuhusu nguo na kitanda cha mtoto wako kama nepi, ambazo mtoto atahitaji, nunua mahitaji muhimu kabla mtoto hajazaliwa na uweke akiba ili ununue nyingine baadae. Kumbuka kwamba utapata nguo nyingi kwa marafiki na ndugu, safisha kila kitu kabla ya kutumia ili kuepuka muwasho kwa mtoto wako.

13. Andaa begii la hospitali

Ni jambo la muhimu kuwa na begi lako la hospitali tayari limeandaliwa kabla ya siku yako ya kujifungua,hata kama huendi kujifungulia hospitali.Kama unapendelea unaweza kuwa na mabegi mawili moja kwa ajili ya siku ya uzazi na nyingine kwa ajili ya siku baaada ya uzazi.

14. Pata usingizi wa kutosha

Kama unapata wakati mgumu kupata usingizi, jaribu kuwa na mito mipya na ilio bora kukusaidia. Kuweka mmoja katikati ya mapaja na mwingine mgongoni na mwingine chini ya tumbo itakusaidia sana kuweza kupata usingizi wa kutosha. Kumbuka kulala kwa ubavu ili uendelee kupunguza nafasi ya kuzaa mtoto mfu.

15. Andaa mahitaji ya ndani ya familia

Fanya maisha yawe rahisi, kwa kuandaa   mahitaji ya muhimu kama mboga mboga, dawa za kufanyia usafi nk.

16. Andaa kiti cha mtoto kwenye gari

Kama unapata mtoto wako hospitali utahitaji siti kwa ajili ya mtoto wako.

17. Kuwa mbunifu katika mapenzi ndani ya miezi mitatu ya ujauzito

Kama una ujauzito ambao hauna shida, unaweza kuendelea kujamiana mpaka pale kufikia kipindi mfuko wa uzazi kupasuka, au wewe kwenda kujifungua, na pia utahitaji kujua ni mikao gani itakua nzuri kwa mwenza wako kuweza kuwa huru wakati wa kufanya mapenzi.

18. Waite wasaidizi

Usijiskie vibaya marafiki wakija kukusaidia, au wanafamilia. Watapendelea kusikia na kuona wanafanya jambo la msingi kwa ajili yako. Kuwa na mtu wa kufanya usafi ndani kuosha vyombo, kukupikia ambaye atakuwa msaada mkubwa kabla  ya mtoto wako kuzaliwa na kuja nyumbani.

19. Ijue hospitali

Kama unatarajia kujifungua hospitali, fahamu utaratibu wa wodi za uzazi.

20. Epuka maumivu ya mgongo

Je,tumbo lako linakupa maumivu ya mgongo? Usiinue kitu chochote kizito, kitakuumiza misuli yako, jaribu kutafuta mkanda wa uzazi utakaokusaidia kuweza kuepuka maaumivu ya mgongo.

21. Jiandae kujifungua

Hakikisha wewe na mwenzi wako mna namba zote za muhimu, namba ya mkungwa wako, namba ya daktari na namba ya hospitali, kama una watoto au mifugo itakua bora kumtafuta mtu wa kuweza kuwatunza ndani ya kipindi hichi.

22. Jifunze kutunza kichanga chako

Kama bado hujajifunza, wakati huu ni mzuri sana kuweza kujifunza kuhusu kichanga chako kutoka kipindi cha ujauzito mpaka kuwa na mtoto jifunze kuhusu wiki ya kwanza ya mtoto wako kuzaliwa.

23. Jiandae kunyonyesha

Unavyojua zaidi kuhusu kunyonyesha, ndivyo itakavyokua rahisi kwa wewe kunyonyesha. Uliza mkunga wako kuhusu unyonyeshaji, mkunga wako atakujuza zaidi na itakusaidia sana.

24. Saidia kuleta uzazi kwa njia ya kawaida

Madaktari bado hawajajua nini kinasababisha uchungu wa uzazi, lakini wamama wengi wanasema kwamba ukitembea, ukifanya mapenzi au kula vyakula vyenye pilipili itasaidia kuleta uchungu mapema.

Vitu vya Kufanya Katika Maisha Yako Kabla ya Kujaribu Kupata Ujauzito

Haya ni mambo ya muhimu ya kuzingtia kabla kujaribu kupata ujauzito.

Acha maadili mabaya.

Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe wa kupitiliza vyote uweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito na matatizo ya kiafya kwa mwanao atakapozaliwa. Cha msingi kujua ni muhimu kumtunza mtoto vizuri na kuachana na vitu hivi,ikiwemo pia matumizi ya kahawa kupitiliza. 

Badilisha ulaji wako kuwa bora.

Kuanzia muda unapata ujauzito ukuaji wa mwanao unahitaji ulaji wa chakula bora kuweza ili kumtunza vyema mtoto wako, hivyo ili mwili wako uweze kujenga lishe bora kwa ukuaji wa mtoto ni jambo la busara kula lishe bora.

Kuwa na uzito uliozidi au uliopunguwa unaweza kufanya uwe na wakati mgumu kuweza kupata mtoto ambayo pia inaweza kuleta matatizo ya kiafya kwako na kwa mtoto. Kuzingatia lishe bora unaweza kuwa na BMI nzuri kwa ajili yako na mtoto. Unatakiwa pia uanze kutumia foliki asidi (mcg 400) kila siku kabla hujapata ujauzito.

Anza kufanya mazoezi mara kwa mara

Ni muhimu ukianza kufanya mazoezi mara kwa mara ambayo yatakupa nguvu zaidi, kuwa imara kutakusaidia kupata ujauzito wenye nguvu. Na pia utakupa nafasi ya kujifungua njia ya kawaida. Mazoezi ni njia ya muhimu kupata uzito bora.

Pumzika

Mazoezi mengi yanaweza yasiwe mazuri sana kwa afya ya uzazi, kupumzika sana kunaweza kukupa nafasi nzuri ya kujifungua na hata kupata ujauzito.

Kama unaweza kujitoa japo lisaa limoja kila siku kila wiki kuondoa mawazo kichwani na shinikizo la damu. Unaweza pia kufanya yoga. Hakikisha unajiandaa kwa kuanza  kuweka  akiba ya hela sasa.

Angalia uchumi wako

Kuwa na mtoto ni gharama! Tambua ni namna gani na kiasi gani gharama ya mtoto itakuathiri katika wiki ya kwanza na miezi ya kwanza. Hakikisha umejiandaa kwa kuanza kuweka akiba sasa.

Zungumza maswala ya uzazi na mwenzi wako.

Kuwa mzazi ni jambo zuri na ni gumu pia. Wewe na mwenza wako lazima mjiandae kwa ukweli kwamba maisha yenu yatabadilika sana. Zungumzeni kuhusu woga wenu na ndugu na marafiki. Kama utaona tatizo popote kati yako na mwenza wako na ni gumu kutatua, jaribuni kuwa na msululishi. Ni vyema kufanya mambo yakawa mazuri sasa, wakati kichanga kikiwa njiani. Mwisho usisahau kuongelea mambo mazuri pia,nini kinakufurahisha na kwa kiwango gani malengo yako yamefanikiwa.

Vipimo na Tafiti Muhimu Kufanya Kabla ya Kupata Ujauzito

Vipimo na tafiti muhimu kufanya kabla ya kupata ujauzito

Ikiwa umeamua kufanya vipimo vya awali kabla ya kupata ujauzito, mtaalamu wako wa afya au nesi anaweza kukuliza kuhusu:

  • Kazi yako-atakuuliza kama kazi yako inahusisha kufanya kazi na vitu hatari
  • Kama una tatizo na siku zako za hedhi
  • Hali yako ya afya na maisha kiujumla
  • Mazoezi unayofanya na kiasi gani
  • Unajisikiaje-kihisia (emotional wellbeing)
  • Utaratibu wako wa kula

Daktari wako atapenda kujua hali yoyote ya kiafya ulionayo kama:

  • Kisukari
  • Pumu
  • Shinikizo la damu
  • Kifafa
  • Matizo ya tezi
  • Matatizo ya moyo
  • Magonjwa ya akili

Mambo mengine yakujadili katika vipimo hivi vya awali kabla ya kupata ujauzito ni kama:

  • Kama katika familia yenu kuna magonjwa ya kurithi. Mueleze mshauri wako wa afya kama kuna historia ya magonjwa ya kurithi katika familia yenu kama selimundu, magonjwa ya mfumo wa upumuaji(uvimbe wa viriba hewa) au anemia.
  • Matumizi ya uzazi wa mpango. Mara nyingi, njia za uzazi wa mpango ulizotumia haziwezi kuathiri mda gani umekaa bila kupata ujauzito. Lakini kama ulikua unatumia sindano, inaweza kuchukua mpaka mwaka mmoja baada ya sindano yako ya mwisho, taratibu za uzazi wako kurudi hali ya awali.
  • Daktari wako anaweza kuuliza kuhusu mimba ulizotoa, zilizoharibika au kutungwa nje ya mji wa uzazi(ectopic pregnancy), kuongelea matukio haya inaweza kurudisha huzuni, hivyo ni vizuri kumwambia daktari wako ili aweze kukupa ushauri na huduma nzuri sasa.

Je, nifanye vipimo na matibabu kabla ya kujaribu kupata mtoto?

Ndio, ni muhimu kufanya vipimo, ila inategemea na hali yako na afya kwa ujumla. Muulize mshauri wako wa afya au muuguzi kama unahitaji kufanya vipimo kabla ya kupata ujauzito. Uchunguzi wa kawaida na vipimo kabla ya ujauzito ni pamoja na:

Vipimo vya magonjwa ya zinaa:

Kama uliwahi kufanya ngono isio salama, ni vema kufanya uchunguzi wa magonjwa ya kuambukizwa ya ngono, hatakama hakuna dalili. Ni vema kufanyiwa vipimo vya:

  • Homa ya ini
  • Klamidia
  • Kaswende
  • Virusi vya Ukimwi (HIV) . Kufanya matibabu ya magonjwa ya ngono mapema kabla ya kupata mimba kunaongeza nafasi ya kuwa na mafanikio kwenye ujauzito.

Vipimo vya kizazi:

 Ikiwa unatoka kufanya uchunguzi wa kizazi fanya mwaka mmoja kabla ya kujaribu kupata ujauzito. Hii ni kwa sababu uchunguzi wa kizazi haufanyiki wakati wa ujauzito, kwani mabadiliko ya asili ya kizazi chako hufanya matokeo kuwa magumu kutafsiri.

Vipimo vya damu:

Ikiwa unafanya vipimo vya awali kabla ya ujauzito, na mshauri wako wa afya au muuguzi wako akawa na wasiwasi una anemia, atakushauri ufanye vipimo hivi. Hii ni kwasababu wanawake wenye anemia mara nyingi wanahitaji kutumia madini ya chuma ya ziada kipindi cha ujauzito.

Kulingana na asili ya kabila na historia yako ya matibabu, kuna uhitaji wa kufanya vipimo vya magonjwa ya kurithi kama siko seli na anemia. Vipimo hivi vitakupatia uhakika na ufahamu wa kujua ni kiasi gani utamrithisha mwanao hali hii ya kiafya.

Ikiwa hauna uhakika kama umepatiwa chanjo ya rubella, unaweza kufanyiwa vipimo vya damu kuangalia.

Je, nipate chanjo kabla ya kujaribu kupata mtoto?

Maambukizi mengi yanaweza sababisha uharibifu wa ujauzito au kasoro baada ya kuzaliwa, hakikisha unapata chanjo kwa mda. Kama unahitaji chanjo ya magonjwa ya virusi kama rubella, inabidi kusubiri mwezi mmoja kabla ya kujaribu kupata mtoto. Chukua tahadhari, kwani inasadikika mwili wako unahitaji muda wa kuangamiza kirusi kabla ya kubeba mimba.

Kama uko katika hatari za ugonjwa wa homa ya ini, unaweza kuamua kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huu. Hivyo basi kama hii ni chanjo pekee ulionayo, unaweza kuanza kujaribu kupata mtoto mara moja.

Mkunga wako atatumia taarifa uliyompatia kuamua kama unahitaji huduma zaidi kutoka kwa mtaalamu wa afya ya uzazi au vinginevyo.

Pia atakushauri:

  • Kufanya mazoezi wakati wa ujauzito hasa mazoezi ya sakafu ya nyonga
  • Kutumia virutubisho kama foliki asidi na vitamin D
  • Kula kwa afya

 

Vidokezo 9 Kukusaidia Kupata Ujauzito kwa Haraka

Vidokezo 9 kukusaidia kupata ujauzito kwa haraka

Unajaribu kupata ujauzito? Mabadiliko rahisi ya maisha ya kila siku yanaweza kukusaidia kuongeza nafasi ya kupata ujauzito. Tazama vidokezo hivi:

Hatua ya kwanza: Acha sigara

Uvutaji wa sigara unajulikana kupunguza nafasi ya kupata ujauzito kwa wanawake na wanaume. Ni hatari pia kwa mtoto kama bado unavuta sigara na una ujauzito.

Hatua ya pili: Fanya mazoezi pamoja

Kuwa imara kimwili ni njia kubwa ya kuongeza nafasi ya kupata ujauzito. Kama hujazoea kufanya mazoezi, anza sasa. Kwa mfano, unaweza kushuka kituo kimoja kabla ya nyumbani ili upate kutembea zaidi au kutumia ngazi badala ya lifti. Unaweza kujiunga na darasa la kucheza au kukimbia mchakamchaka pamoja.

Hatua ya tatu: Kula chakula chenye afya

Chakula na uzazi vinahusiana. Chakula cha pamoja chenye mlo kamili, kinaweza kuongeza nafasi ya kupata ujauzito. Jaribu pia kutafuta ni vyakula vipi vizuri kwa wanaume na wanawake wanapojaribu kutafuta mtoto.

Hatua ya nne: Pumzika!

Kujaribu kupata ujauzito kunaweza kuchosha. Kwa bahati mbaya, kuwa na mawazo sana inaweza kufanya ugumu kupata ujauzito, hivyo jaribuni kuchukulia mambo kiurahisi. Jipatieni mda wa kupumzika kwa kufanya masaji, mazoezi ya kupumua kwa kina au kufurahia milo ya usiku pamoja. Chochote kinachoweza kuwafanya mpumzike na kuwa katika hali ya utulivu.

Hatua ya tano: Acha pombe

Pombe inaweza mdhuru mtoto kama unakunywa sana baada ya kupata ujauzito,hasa wiki za kwanza kabla ya kugundua una ujazito. Kunywa kwa kupitiliza kunaweza kupunguza nafasi ya kumpa mwanmke ujauzito kwa wanaume. Hivyo, ni vyema wewe na mwenzi wako kuepuka pombe, au kupunguza kabisa, mara mnapopanga kutafuta mtoto.

Hatua ya sita: Mwanaume kuepuka korodani kuwa katika hali ya joto sana.

Wakati korodani zikipata joto sana, mbegu za kiume zinateseka. Kukaa mda mrefu kutumia laptop kwenye mapaja, au kufanya kazi katika mazingira yenye joto inaweza kuleta madhara katika utengenezaji wa mbegu za kiume. Inashauriwa, kuepuka kuvaa nguo za ndani (boxer) zenye kubana, ingawa hakuna ushahidi mwingi kwa hili. Ikiwa una matumaini ya kuwa baba ni wakati mzuri wa kuacha kutumia laptop kwa kuweka kwenye mapaja na kuvaa nguo zenye kukupa uhuru.

Hatua ya saba: Chukua likizo pamoja

Mapumziko au wikiendi ndefu pamoja inaweza kuwasaidia kupunguza msongo wa mawazo, na kufurahia mapumziko pamoja. Kiukweli, baadhi ya wazazi wameapa mapumziko ya pamoja yenye nia ya kutafuta mtoto (conceptionmoon) ni njia kuu ya kupata mimba.

Hatua ya nane: Fufua nuru katika mapenzi

Kama imeshindikana kuenda mapumziko,au kupata likizo, jaribu njia nyingine za kufufua mapenzi. Baadhi ya wanandoa wengi wanahisi wanafanya mapenzi kujaribu kupata ujauzito. Kama hili ni jambo linalokukumba, jaribu kurudisha mwanga katika mapenzi yenu.

Hatua ya tisa: Fanya mapenzi (kujamiana) mara kwa mara

Kujamiana ni muhimu sana! Hata kama unaja lini yai litapevushwa, kufanya mapenzi mara mbili hata tatu itakupa nafasi nzuri ya kupata ujauzito.

Mikao Mizuri ya Kujamiana Ili Kupata Ujauzito Haraka

Je, kuna ukweli juu ya maneno yanayosambaa kwamba mikao inayofanyika wakati wa kufanya ngono inaweza kufanya urahisi wa kupata ujauzito? Tukumbuke jambo moja kwamba hakuna ukweli wowote unaothibitisha baadhi ya mikao ya ngono ni bora zaidi ukiwa unatafuta mtoto? Lakini bado kuna wanawake wengi kutoka pande nyingi za duniani wanaodai kuwa baadhi ya mikao inasaidia kupata ujauzito haraka lakini pia kusaidia kupata ujauzito wa jinsia fulani.

Mkao wa kifo cha mende kwa ajili ya kupata mtoto (Missionary style):

Ni ukweli kwamba watoto wengi wanakuja duniani kupitia mkao huu, mkao wa kifo cha mende ni mkao mzuri na usiochosha wa kutengeneza mtoto. Mwenza wako anakuwa juu na wewe ukiwa umelala chini kwa mgongo, mbegu za kiume zinapata njia nzuri kwenda kwenye mfuko wa uzazi kwa ajili ya kurutubishwa. Watu wengi wanakiri mkao huu ni muafaka kama unatafuta mtoto wa kike, mkao huu unazuia uume kupenya sana hivyo kuzipa mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kike (female sperms) nafasi zaidi katika kurutubisha yai. Hii ni kwasababu mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kike zinasafiri polepole zaidi kulingana na mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume. Kuzuia upenyeaji wa uume itasababisha mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume kuchukua mda mrefu kufika kwenye yai la mwanamke kwaajili ya kurutubishwa, hali hii inaruhusu mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kike kusafiri haraka na kulifikia yai.

Mkao wa mbwa (Doggy-style):

Kuna uhakika ya kuwa mwenza wako atakubaliana kuwa mkao wa mbwa ni mkao bora zaidi. Lakini wasichojua ni kwamba ni mkao bora pia kupata ujauzito kiurahisi. Mkao huu wa unakusaidia kupata ujauzito kwasababu uume unakwenda mbali zaidi. Pia unafungua mfuko wa uzazi kuliko mikao yote na kufanya mbegu za kiume kupita na kupenya kwa urahisi ndani ya mayai. Mkao huu unaruhusu upenyaji wa uume wa mwenza wako ndani zaidi na kusababisha mbegu za kiume kumwagwa karibu na mlango wa kizazi. Hali hii inasaidia mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume kusafiri haraka kwasababu ya umbali mfupi kuelekea kwenye yai kwaajili ya urutubishwaji.

Mkao wa “Glowing Triangle”:

Huu ni mkao unaofanana na mkao wa kifo cha mwende. Mwanamke anakuwa umelala kwa mgongo na mwenza wako juu yako. Tofauti iliyopo hapa ni kuwa mwanamme anakuwa amesimama vidole vya miguu na magoti yake hayagusi chini. Kwa kunyanyua kiuno chako unaweza kumbana mwenza wako.  Mkao huu unasababisha uume kufika mbali zaidi na hivyo kuchangia kupata ujauzito kwa urahisi.

Mkao wa “Anvil”:

Huu ni mwendelezo wa mkao wa kifo cha mende (missionary). Katika mkao huu mwanaume anakuwa juu yako lakini wewe unanyanyua miguu juu ya kichwa chako kabla hajaingiza uume ndani ya uke wako. Ni njia nzuri ya uume kufika mbali na inasaidia kugusa “G spot”, ambapo husaidia kutungisha mimba. Mkao huu pia ni bora kwa ajili ya kutungisha mimba kwa haraka.

Mkao wa “Magic Mountain”:

Huu ni mkao bora na unasaidia kutungisha mimba kwa urahisi.Tofauti na mkao huu ya ile ya “doggy-style” ni kwamba hapa mwenza wako anakuinamia kiasi kwamba mgongo wako unakuwa kifuani kwake unaweza kuweka mito ili kupata usawa.  Mkao huu ni mzuri ambao husababisha mbegu kusafiri kwa haraka, na pia hukufanya kufika kileleni kwa haraka.

Mkao wa “Spooning”:

Mkao huu ni mkao mzuri kwa ajili ya kutengeneza mtoto na mkao mzuri wa kimapenzi. Katika mkao huu unalala upande wako na mwenza wako anakukumbatia kwa nyuma. Mkao huu unakuhakikishia kuwa uke unakuwa katika nyuzi tisini. Mkao huu unazuia uume kupenya sana,kwasababu miguu yako inazuia mwenza wako kupenya zaidi ndani ya uke. Mkao huu unaruhusu mbegu za kiume kumwagwa karibu na uke, ili mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume zisifike kwenye yai haraka na kuruhusu mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kike kusafiri salama kwenye yai.

Mkao wa “the Splitting Bamboo”:

Ukiwa unaongelea mikao ya kimapenzi kwa ajili ya kusaidia kupata ujauzito mapema mkao huu unahusika sana. Mkao huu ni moja kati ya mikao mashuhuri katika mikao ya Kamasutra. Katika mkao huu unatakiwa unyooshe mguu wako mmoja juu kupitia kifuani kwa mwenza wako mpaka mabegani. Yeye ataushika mguu wako kwa ajili kupata stamina. Ukiachilia kugusa “G spot”, mkao huu una kuhakikishia uume kufika ndani zaidi na kukupa uhakika zaidi wa kupata ujauzito (mtoto wa kiume).

Mkao wa “The Reverse Cowgirl”:

Mkao mzuri wa kupata mimba na mwanamke kuwa juu! Mkao mzuri kwa wanandoa wenye uthubutu! Katika mkao huu mwenzi wako analala kwa mgongo, na wewe unamkalia ukiangalia miguu yake. Mwanamke akiwa juu,ni mkao unaopendekezwa unapotaka kujifungua mtoto wa kiume. Kitu muhimu cha kukumbuka ni kwamba mkao huu mwanamke anatakiwa adhibiti upenyaji wa uume wa mwenza wake. Ikiwa unataka kujifungua mtoto wa kike, hakikisha uume wa mwenza wako usipenye sana, pengine na hapo utaongeza nafasi ya kujifungua mtoto wa kiume.

Mkao wa “the Sphinx”:

Mkao huu,mwanamke analala na tumbo, uzito wake ukibebwa na mikono yake. Mguu mmoja unakunjwa na mwingine unanyooka nyuma yako. Mwenzi wako atakubana kwa nyuma na mikono yake ikishika juu kidogo ya kiuno. Mkao huu ni mzuri kuruhusu uume wa mwenza wako kuingia ndani zaidi na kusaidia kupata ujauzito mapema.pia ni mkao mzuri wa kupata ujauzito wa mtoto wa kiume kwasababu uume wa mwenza wako unapenya zaidi ndani.

Mkao wa “The Union Of The Oyster”

Wakati unataka kushika mimba, katika kitendo cha kufanya mapenzi kinaweza kukufanya uchoke. Ndio maana twashauri kufanya kwa style tofauti tofauti. Huu ni mkao utakaokufanya uone maisha ya mapenzi kuwa mazuri sana. Lakini pia itakufanya wewe uweze kushika mimba. Katika mkao huu utalala chini kwa mgongo wako wakati miguu yako ukiivuta kuja kichwani wakati huo mwenza wako atakuwa ameinuka  huku akiwa ameshikilia chini na kuendelea na tendo.

Mkao wa “The Padlock”

Huu ni mkao mwingine ndugu zangu, Mkao huu unakutaka ukae pembezoni mwa kiti au samani iliyojuu kujishika kwa mikono yako kwa nyuma. Mwenza wako atahitaji kusimama mbele yako na wewe kuzungusha miguu yako kumbana. Huu sio mkao wa wapenzi walio na uthubutu ila ni mkao mzuri unaoruhusu kupata ujauzito wa mtoto wa kiume- mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume kusafiri haraka kurutubisha yai, kwasababu ya upenyaji wa uume uliorahisisha umwagaji wa mbegu hizi karibu kabisa na mlango wa uzazi wa mwanamke.

Kumbuka

  • Inashauriwa mwanamke asifike kileleni akiwa anajamiana kama anataka kupata mtoto wa kike. Hii ni kwasababu kila mwanamke anapofikia kileleni, uke wake unakua na alkali zaidi,amabyo ina faida sana kwa mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kiume. Mbegu za kiume zilizobeba jinsia ya kike zinastawi zaidi katika mazingira yenye asidi. Hili ni jambo la muhimu kukumbuka wakati wa kutafuta mtoto wa jinsia fulani.
  • Kila mkao unaoruhusu uume kupenya zaidi ndani ya mlango wa uzazi wa mwanamke, unachangia mwanamke kupata ujauzito wa mtoto wa kiume.
  • Mikao kama “doggy-style”, “padlock”, “missionary”, “spooning” ni mizuri kama ungependa kupata ujauzito wa mapacha.