Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 32

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 32
Kama mtoto wako ni wakiume, korodani zake pengine zimeshashuka na kuhamia katika mfuko wa korodani zake. Wakati mwingine, moja au korodani zote zinaweza zikawa hazijafika kwenye nafasi yake mpaka pale atakapozaliwa. Usiwe na wasiwasi juu ya hili kwani korodani ambazo hazijashuka mara nyingi hujishusha zenyewe kabla ya kufikisha mwaka wa kwanza.

Mtoto wako ataongezeka robo tatu au nusu ya uzito wake wa kuzaliwa wakati wa wiki saba zijazo, hunenepa zaidi tayari kwa maisha ya nje ya mji wa mimba. Kutokana na safu ya mafuta chini ya ngozi yake, ngozi ya mtoto wako inakua vizuri.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 32
Kadiri mtoto wako anavyokua ndani yako, kuhakikisha unakula vizuri katika wiki chache zijazo. Tumbo lako la chakula litakuwa dogo zaidi kwani mtoto wako anachukua nafasi sana ndani yako, lakini karibu nusu ya uzito wote unaoweza kuupata sasa huenda moja kwa moja kwake.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 32
Wanawake wengi wajawazito huwa na wasiwasi kama watakuwa na uwezo wa kuzaa kwa njia ya kawaida. Huu ni wasiwasi wakawaida, hasa kama wewe unatarajia kujifungua mtoto wako wa kwanza.

Weka moyoni, kwamba kuna baadhi ya namna za kukaa wakati wa kujifungua ambazo unaweza kujaribu. Namna hizo za mikao zitakusaidia mlango wako wa uzazi kufunguka (kupanuka) wakati wa uchungu na kumfanya mtoto wako ashuke chini wakati ukifika.

Jaribu nafasi mbalimbali, ukilinganisha na kupumua, massage na njia ya asili ya kupunguza maumivu. Kupata baadhi ya mazoezi sasa itaongeza nafasi yako ya kujifungua kwa njia ya kawaida pindi ni wakati wa kujifungua.

Ujauzito Wiki ya 31

Jinsi mtoto wako anavyokua katika wiki ya 31
Je mtoto wako anakufanya uwe macho usiku? Katika wiki chache zijazo, kusogeana kucheza kwa mtoto wako kunaweza kuanza kuwa kwa haraka na kwa nguvu zaidi kwa kua anakua kwa kasi sasa.

Mtoto wako anaweza kusogeza kichwa chake upande na upande, viungo vyake vinaendelea kukomaa na safu ya mafuta inazalishwa chini ya ngozi yake.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 31
Unaweza kujisikia kuishiwa pumzikidogo wakati wa hizi wiki chache kabla ya kuzaliwa kwa mtoto wako. Hii hutokea kwa sababu mji wa mimba yako umeongezeka hivyo kubana mapafu yako na misuli mikubwa katikati ya kifua ambayo husaidia kupumua.

Kuishiwa pumzi huku kutaendelea mpaka mtoto wako atakapo shuka chini katika mlango wa uzazi. Hii hutokea katika wiki ya 36 ya mimba ya kwanza na pengine si mpaka kuzaliwa kama ulishawahi kujifungua kabla. Kama umekuwa ukifanya mazoezi katika kipindi cha ujauzito wako, mazoezi mapole yanaweza kusaidia kupumua kwako kwa sasa.

Hata hivyo, kama haukua umeelekeza nguvu katika kua kufanya mazoezi huko nyuma, kuanza kufanya mazoezi sasa hivi inaweza kufanya tu ujisikiekuishiwa pumzi zaidi.

Je uzito wa tumbo lako unakupa maumivu ya mgongo? Jaribu kutokuinua chochote kizito, kwani italeta maumivu kwenye mishipa yako laini. Ni kawaida kupata maumivu ya nyonga wakati mimba ikiendelea.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 31
Kama wewe na mpenzi wako mnapata woga kuhusu ile siku kubwa, inaweza kusaidia kupitia mlichojifunza katika madarasa ya wajawazito. Mazoezi yakupumua mliojifunza pamoja pia mnaweza kuanza kuyajaribu.

Ujauzito Wiki ya 30

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 30
Kuanzia sasa, mtoto wako anaongezeka uzito haraka. Mapafu yake na njia ya utumbo karibu zinakomaa na yeye pengine atakuwa na uwezo wa kufungua na kufunga macho yake kwa sasa, ili aweze kuona ndani kwako. Kama ukiangazia mwanga juu ya tumbo yako, mtoto wako anaweza hata kujinyoosha ili kujaribu kuugusa mwanga unaosogea.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 30
Pengine umeongezeka uzito kiasi mwezi huu. Kuongezeka gramu 450 kwa wiki ni kawaida kabisa wakati wa miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito. Mahitaji ya mtoto wako ya virutubisho ni makubwa kwa ukuaji wake wa mwisho kabla yeye kuzaliwa.

Unaweza kuwa na furaha kikamilifu na kuongezeka kwaukubwa wa umbo lako.Kama uzito unaoongezeka ni wa kiafya bora, tambua kwamba unafanya kazi kubwa ya kumpatia mtoto wako mwanzo bora katika maisha. Lakini kama wewe umechoshwa na una lindi la mawazo kuhusu ukubwa wa umbo lako kumbuka kuwa ujauzito ni jambo jema na unafanya vyema mpaka sasa kulea kiumbe ndani yako. Kuwa mwenye faraja kwani zimebaki wiki chache sasa mpaka kujifungua.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 30
Kupata usingizi mzuri usiku kunaweza kuwa kugumu tena zaidi katika miezi mitatu hii ya mwisho. Kadiri tumbo lako linavyokua, kukaa na kujisogeza vizuri inakuwia vigumu.

Unaweza kupata hali ya kubanwa na mkojo mara kwa mara. Hii ina maana nyakati za usiku safari za kwenda chooni zitakuwa nyingi kuliko kawaida. Ndotopia zinaweza pia kuathiri ubora wa usingizi wako, na kukuacha wewe kuhisi kusumbuliwa na uchovu na kushindwa kupumzika. Mnaweza mkazungumza na mwenzi wako kuhusu ndoto zake pia ili kupata wasaa wa kupunguza msongo wa mawazo.

Ujauzito Wiki ya 29

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 29
Ubongo wa mtoto wako unakua kwa kasi, na kichwa chake kinakua kikubwa ili kumudu ubongo huo. Kama wewe unatarajia mtoto wa kiume, korodani zake zinasoge kutoka eneo lake zilipo karibu na chini ya figo zake kuelekea chini sehemu yake. Kama unatarajia kupata mtoto wa kike, kinembe chake bado ni kikubwa na kinaonekana sana kwa sababumidomo yake ya uke (labia)bado ni ndogo kuweza kukifunika. Hii itatokea katika wiki chache za mwisho kabla ya kuzaliwa.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 29
Hamu yako ya kula huongezeka kulingana na ukuaji wa mtoto wako katika miezi mitatu ya mwisho, hamu hii inaweza ikawa zaidi katika keki, pipi na vyakula vya haraka “fast foods”. Jaribu kula vitu hivi mara chache chache zaidi kuliko mara kwa mara.

Kula vizuri katika hatua hii ya ujauzito ni muhimu kwa afya yako na afya ya mtoto wako. Jaribu kula chakula kingichenye wingi wa chuma, ambayo husaidia kutengeneza seli nyekundu za damu. Mtoto wako atachukua hifadhi ya chuma kutoka mwilinimwako, ili asipungukiwe ila wewe unaweza pungukiwa na kukuletea matatizo.

Ongeza madini ya chuma kwa kula milo yenye vyanzo vya chuma, kama vile nyama isiyo na mafuta,mbogamboga na matunda katika mlo wako.

Sasa ni wakati mzuri wa kujifunza baadhi ya mazoezi ya kujinyoosha ambayo yatafungua mwili wako tayari kwa kuzaa mtoto wako. Usijali kama ni vigumu kwako kujifunza mazoezi mpya. Hata kunyoosha mara kwa mara inaweza kukusaidia kuepuka misuli kubana na kuvimba miguu.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 29
Sasa ni wakati mzuri wa kujifunza baadhi ya mazoezi ya kujinyoosha ambayo yatafungua mwili wako tayari kwa kuzaa mtoto wako. Usijali kama ni vigumu kwako kujifunza mazoezi mpya. Hata kunyoosha mara kwa mara inaweza kukusaidia kuepuka misuli kubana na kuvimba miguu.

Ujauzito Wiki ya 28

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 28
Mtoto wako sasa anaweza kufungua macho yake na kuwa na ari ya kuelekeza kichwa chake kwenye chanzo endelevu cha mwanga mkali.Kucha zake zinatumbika, na tabaka/safu ya mafuta inaanza kujijenga chini ya ngozi yake akiwa anajiandaa tayari na maisha ya nje ya mfuko wa uzazi.

Kama wewe utapenda wazo la kuzungumza na mtoto wako wakati yeye bado angali ndani yako, basi kuimba na kumsomea ni njia nzuri ya kufanya hivyo. Njia za neva za masikio ya mtoto wako zimekamilika sasa. Usijali kama utahisikuwa na wasiwasi kuwasiliana na mtoto wako kwa njia hii. Sio kila mtu yupo tayari kufanya hivi, ila ni vyema kutambua kuwa mtoto wako tayari anasikia kila kitu unachosema.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 28
Simuda mrefu umebaki kwa sasa. Uko katika miezi mitatu ya mwisho, ambayo itaenda hadi mwisho wa ujauzito wako, kwa kawaida wiki 40 au zaidi. Unaweza kumwonadaktari wako au mkunga wako mara nyingi zaidi kuanzia sasa. Si lazima kusubiri mpaka siku yako ya kliniki kama unataka kujadili kitu chochote, au una tatizo ni vyema kwenda au kuwasiliana na daktari mara moja.

Pengine hupendi unavyohisi. Unaweza kufikiri, “Nimekuwa mjawazito milele”, au labda ukahisi, “siko tayari kwa hili”. Hakika haupo peke yako. Kubadilishana ujuzi na wamama wajawazito wengine kwenye madarasa ya wajawazito yaweza kukusaidia na kukutuliza kimawazo.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 28
Kama wewe ni baba, unajisikiaje kuhusu kuona mpenzi wakoakienda kujifungua? Kujua nini kinatokea wakati wa uchungu ni njia nzuri ya kujiandaa kwa ajili ya tukio hili litakalobadilisha maisha yenu.

Wakati mwingine, mambo yanaweza yasiende sawa kama ilivyotarajiwa wakati wa uchungu na kujifungua. Mtoto wako anaweza kuhitaji msaada ili azaliwe. Ongea na daktari au mkunga wako kuhusu huduma mbalimbali juu ya kusaidiwa kuzaa na kuhusu upasuaji, ili uwe umejiandaa vizuri na kuweza kumsaidia mwezi au mpenzi kupitia taratibu zote kama itahitajika.

Ujauzito Wiki ya 27

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 27
Sasa unapokaribia miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wako, mtoto wako ameshajaza nafasi ya kutosha katika mji wako wa mimba.

Mtoto wako sasa anaweza kufungua na kufunga macho yake, kulala na kuamka katika vipindi vya kawaida, na anaweza kuwa anaanza kunyonya vidole vyake, sanasana kidole gumba. Mapafu yake pia yanaweza kufanya kazi kwa msaada wa mashine kama itatokea bahati mbaya akazaliwa mapema (njiti).

Dalili za ujauzito katika wiki ya 27
Mwili wako ni unabadilika kwa kasi sana sasa. Mji wa mimba upo juu karibu na ngome ya mbavu zako na unaweza kuanza kuona misuli ya miguu inabana na unapata choo cha kubana mara kwa mara. Matatizo haya yote ya ujauzito yatatoweka baada ya kupata mtoto wako.

Katika hudhurio lako lifuatalo kliniki unaweza kupewa kipimo cha damu kuangalia kama una upungufu wa damu. Unaweza kuwa na upungufu wa damu kama huna madini chuma ya kutosha katika mlo wako, na kusababisha upungufu wa chembechembe nyekundu za damu. Wanawake wengi wajawazito hupata upungufu kidogo wa damu kipindi cha ujauzito kutokana na mabadiliko ya kawaida katika mwili.

Kama kundi lako la damu ni “Rhesus-Negative” ni lazima kupewa sindano ya “anti-D” ndani ya wiki ya 28.

Uchungu unakaribia sasa hivyo kama bado haujapanga vyema utajifungulia wapi na namna ya kufika kwenye kituo cha afya husika ni vyema kuweka mipango yako sawa sasa.

Amini usiamini, mafanikio ya mama kunyonyeshainategemeana na mtazamo wa mpenzi wake. Kama wewe ni baba-mtarajiwa, ni wakati wa kujifunzavitu vya msingi kuhusu kunyonyesha ili uweze kutoa msaada baada ya mtoto wako kuzaliwa.

Kama unataka kusafiri kwa njia ya ndege, utahitajika kutoa kielelezo kutoka kwa daktari wako kikisema kuwa upo sawa kusafiri kwa ndege. Sheria za baadhi ya ndege na nchi mbalimbali haziruhusu mjamzito aliyefikia miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito kusafiri kwa ndege.

Ujauzito Wiki ya 26

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 26
Kama ungeweza kumuona mtoto wako kwa sasa, ungeweza kuwa na uwezo wa kupata mtazamo wa macho yake, ambayo yanaanza kufunguka.

Mtoto wako anazidi kupata uwezo wa kuitikia miito ya sauti zaidi kadri wiki zinavyopita. Mwanzoni, anaweza kusikia sauti za chini kutoka ndani ya mwili wako, kama vile mapigo ya moyo wako na kutetema kwa tumbo lako. Lakini kwa sasa, ana uwezo wa kusikia sauti za juu zikipigwa kutoka nje ya tumbo lako (mji wa mimba).

Dalili za ujauzito katika wiki ya 26
Unakaribia kuifikia miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wako. Miezi mitatu yako ya mwisho huanza wakati umekamilisha wiki 27 za ujauzito. Hivi punde,utakuwa umemshika mtoto mikononi mwako na kuanza kumnyonyesha.

Wakati huu, unaweza kuona kuongezeka kidogo kwa shinikizo la damu yako, ambayo ni ya kawaida. Sharti moja wakunga wako watakuwa macho sasa ni kuhusu shinikizo la damu kipindi cha ujauzito (pre-eclampsia). Shinikizo la damu linahusiana sana na (pre- eclampsia).

Hata hivyo, kwa asilimia ndogo kama pre-eclampsia haitatambulika mapema, dalili zake ni pamoja namaumivu makali ya kichwa, kuona maruerue na mikono na miguu kuvimba. Hivyo ni vyema kumuona daktari mara moja pale unapoziona dalili hizi zinatokea. Soma kuhusu dalili nyingine kipindi cha ujauzito ambazo unapaswa kutokupuuzia.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 26
Kama ulifanya kipimo cha “vaginal swab” kuangalia kama una maambukizi ya uke wakati wa ujauzito kama vile muwasho, candida na bakteria, matokeo yake yanaweza kurudi chanya kwa bakteria wa kundi B streptococcus. Haya ni maambukizi ya kawaida ambayo wanawake wengi wanakuwa nayo bila kujua na bila kusababisha madhara yoyote, isipokuwa katika hali nadra sana. Kama utakuwa unapata homa na kupata maumivu makali wakati wa kukojoa ni vyema kumuona daktari.

Ujauzito Wiki ya 25

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 25
Sasa mtoto wako ameanza kufanya harakati za kuanza kupumua, ingawa hakuna hewa katika mapafu yake. Ufahamu wake unaendelea kukua kwa haraka. Katika hatua hii, tafiti mbali mbali zinaonyesha watoto huitikia miguso na mwanga.

Ukimulika tumbo lako kwa tochi, mtoto wako atageuza kichwa chake, hii itaonesha kwamba kiini cha mfumo wa fahamu wa macho yake “optic nerve” kinafanya kazi vizuri.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 25
Unaweza kuhisi haja ya kuweka miguu yako juu kidogo mara nyingi zaidi sasa na kupumzika mara kwa mara. Japokuwa uchovu unaweza kuwa unarejea, jaribu kukaa mchangamfu na mkakamavu. Kuogelea ni zoezi zuri kadiri tumbo lako linavyozidi kuwa kubwa. Maji yanaubeba uzito wako na kunyoosha mishipa yako. Kuogelea taratibu na kwa makini hufanyisha mazoezi mwili wako mzima.

Jaribu kutokufanya mazoezi yoyote karibu sana na muda wa kulala,kufanya mazoezi jioni kunaweza kusababisa wewe ikawa vigumu kupata usingizi.

Tukizungumzia kupata usingizi, tumbo lako linalokua linaweza kukusababishia wewe kukosa nafasi ya wewe kupumzika vizuri. Inapendekezwa kulala kwa ubavu wako badala ya mgongo wako kutoka miezi mitatu ya pili “second trimester”. Unaweza kutumia mito kama egemeo kusaidia tumbo lako katika kitanda.

Jaribu kupendelea mfumo mzuri wa mlo bora. Mahitaji ya chakula kwa mtoto wako ni makubwa zaidi katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito.

Ujauzito Wiki ya 24

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 24
Mtoto wako anaendelea kukua kwa kasi. Mwili wake unajaza na kuchukua nafasi zaidi katika mfuko wako wa uzazi lakini ngozi yake bado ni nyembamba na tete. Pamoja na haya mtoto wako ana uwezo mkubwa sana wa kuishi kama akizaliwa kabla ya siku zake kuanzia sasa.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 24
Unaweza kuanza kuona michirisi ya mvutano “stretch marks” juu ya tumbo lako, kwenye makalio na chini ya matiti.

Kupaka mafuta au krimu mbalimbali zinaweza kusaidia kulainisha ngozi na kukufanya ujisikie vizuri na kuondoa miwasho na ngozi kuwa kavu, lakini haitaweza kuziondoa alama hizi za michirizi ya mvutano wa ngozi “stretch marks”. Alama hizi za mvutano wa ngizi ni za kawaida katika hatua hii ya mimba na kuisha kwa alama hizi ni baada ya kujifungua.

Unaweza pia kugundua kwamba macho yako hayapendi mwanga mkali na ni makavu. Hii ni dalili ya kawaida kabisa kwa ujauzito. Kama macho makavu yanakusumbua sana ni vyema kumuona daktari wako au daktari wa macho. Matibabu au dawa ambazo unaweza kununua katika maduka bila mwongozo mzuri kutoka kwa daktarizinaweza zikawa hazifai wakati wa ujauzito.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 24
Ni vyema kuanza maandalizi mapema. Kama mwenza wako yupo ni vyema kuanza kuzungumza pamoja kuhusu namna mtakavyoshirikiana pamoja katika kipindi cha kujifungua kitakapofika. Kuwa na mtu anayekupa moyo, na kukumbusha kila mara kukabiliana na kukusaidia kufanya maamuzi wakati uko katika uchungu, inaweza kufanya uzoefu wa kujifungua kwako kuwa chanya zaidi.

Kuna sababu nzuri ya kuwa na msaidizi wakati wa uzazi. Kimsingi, msaidiziwako atakuwa tayari kujifunza kuhusu kujifungua, na kuwa tayari kuacha kila kitu wakati unauhitaji. Hivyo ni muhimu sana kuwa na mipango ya mbele. Kutegemea na ni kituo gani cha afya utajifungulia, msaidizi wako anaweza akaruhusiwa kukaa na wewe wakati wote wa hatua za kujifungua. Ni vyema kuuliza kwa daktari wako kama hili ni jambo ambalo linawezekana kwenye kituo unachotegemea kujifungulia.

Ujauzito Wiki ya 23

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 23
Moyo wa mtoto wako unapiga kwa nguvu zaidi na unasambaza damu nyingi zaidi mwilini mwake. Ndani ya muda huu mtoto wako ameanza kusikia sauti za karibu kwa usahihi zaidi. Anaweza pia kusikia sauti za mbali kidogo kama mlango kufungwa kwa nguvu.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 23
Kama unasumbuliwa na kutopata choo au choo kigumu au kujisikia mzembe mzembe, inaweza kuwa inasababishwa na homoni ya progesteroni. Wakati wa ujauzito chakula kinasafiri taratibu zaidi kwenye utumbo wako, hali inayopelekea wewe kupata shida ya kupata choo. Kadiri mtoto wako anavyokuwa atasukuma zaidi chini eneo la haja kubwa hivyo kufanya hali ya choo kigumu kuwa mbaya zaidi. Utaona ya kuwa kukosa choo au choo kigumu inakera, lakini karibia nusu ya wanawake wajawazito wanasumbuliwa na tatizo hili wakati fulani katika ujauzito wao. Hivyo haupo peke yako.

Ulaji wa mbogamboga na matunda itasaidia chakula kusafiri vizuri na kupunguza kuvimbiwa na tumbo kujaa gesi. Kuongeza kiwango cha maji unayokunywa pia itasaidia choo chako kuwa kilaini.

Kujikamua wakati wa haja kubwa kunaweza kusababisha kupata mipasuko midogo midogo inayoweza kusababisha kutoka damu. Hali hii ikitokea ni vyema ukapata kumuona daktari kwa matibabu zaidi.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki 23
Mtoto wako ameanza kusikia sauti mbalimbali na kuweza kuzitofautisha. Ana uwezo wa kuitambua sauti yako pia. Ni wakati mzuri sasa kuanza kuwasiliana na mtoto wenu kwa kuimba nyimbo mbalimbali za watoto na kuongea nae mara kwa mara akiwa bado tumboni. Utakuja kugundua kwamba kuziimba nyimbo hizi hizi baada ya mtoto kuzaliwa zitakuwa zinambembeleza haraka zaidi.