Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Magonjwa 10 yanayoongoza kwa vifo Tanzania

Tanzania ni nchi yenye idadi ya watu inayokadiriwa kuwa 53.4 milioni kufikia mwaka 2015. Kwa Tanzania kadirio la umri wa kuishi (life expectancy) ipo kwenye miaka 62.7 kwa wanaume na miaka 65.5 kwa wanawake katika mwaka wa 2015.

Japokuwa inakadiriwa namba hizi zitaendelea kuongezeka na watanzania kuishi miaka mingi zaidi kadiri muda unavyoenda, bado kuna matatizo yanayotukumba kama nchi yoyote ile duniani ya kiafya.

Kutokana na ripoti mbalimbali yafuatayo ndiyo magonjwa kuu 10 yanayosababisha vifo Tanzania:

  1. VVU / UKIMWI (HIV/AIDS)
  2. Maambukizi ya mfumo wa chini wa upumuaji (Lower Respiratory Infections)
  3. Magonjwa ya kuhara (Diarrheal diseases)
  4. Magonjwa ya moyo (Ischemic Heart Disease)
  5. Magonjwa ya mfumo wa damu wa ubongo (Cerebrolvascular Disease)
  6. Magonjwa ya mfumo wa ukuaji tumboni (Congenital defects)
  7. Malaria
  8. Kifua Kikuu (TB)
  9. Utindio wa Ubongo (Neonatal Encephalopathy)
  10. Maambukizi ya damu kwa watoto wachanga (Neonatal Sepsis)

Haya ndio magonjwa kumi yanayoongoza kwa vifo Tanzania kwa ripoti ya mwaka 2015. Pamoja na kwamba Malaria inaonekana ni ya 7 kwenye mchanganuo huu, bado ni ugonjwa unaoongoza kwa vifo kwa watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania.

Ni vyema kuyatambua magonjwa haya kwani ndio uhalisia wa eneo unaloishi. Kuyafahamu na kujifunza zaidi kuhusu magonjwa haya ni muhimu ili kuweza kuwa katika uwezo mzuri wa kupata huduma, tiba na hata kutambua namna ya kujikinga na magonjwa haya.

Imepitiwa: July 2017

Leave a Comment

(30 Comments)