Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ndoto za Hofu na Kutisha kwa Mtoto

Ndoto za hofu wakati wa usiku ni nini?

Ndoto za hofu wakati wa usiku zinatokea wakati wa kulala, mtoto anaamka na kukaa mara moja kitandani,na kuanza kulia,kunong’ona,kupiga kelele,kulalamika na kujitupatupa akiwa amefungua macho lakini bila kuamka usingizini vizuri. Kwasababu yupo katikati ya kuamka na usingizini anaweza asitambue uwepo wako na asiitikie chochote utakachomwambia. Hali hii inaweza kudumu mpaka dakika 40 na mwanao atarudi kulala na asiwe na kumbukumbu yeyote akiamka kesho asubuhi.

Tofauti kati ya ndoto za hofu na jinamizi usingizini

Tofauti na ndoto za hofu, jinamizi usingizini inamfanya mwanao aamke- anakumbuka ndoto yake na wakati mwingine kuhadithia na atahitaji umfariji katika hili. Kawaida watoto wanapata ndoto za hofu masaa machache baada ya kulala lakini jinamizi ndotoni hutokea katikati ya usiku yaani masaa machache kabla ya kupambazuka (kati ya saa nane na saa kumi na mbili).

Njia rahisi ya kutofautisha kati ya jinamizi usingizini na hofu ndotoni ni kujiuliza ni nani aliathirika zaidi asubuhi. Kama mwanao ataamka akiwa mwenye wasiwasi na huzuni basi ni “jinamizi usingizini” lakini kama ni wewe uliyesumbuka basi ni “ndoto za hofu”. Kuwa na amani kwasababu ndoto za hofu zinakusumbua wewe zaidi ya mwanao anayepitia.

Nifanye nini kama mwanangu ana ndoto za hofu wakati wa usiku?

Usimwamshe. Mtoto mwenye ndoto za hofu ni ngumu kumtuliza hasa kumshika kama unataka kumfariji. Unaweza kuongea nae kwa utaratibu kama yuko hatarini kujiumiza, lakini usimshike. Kabla ya kwenda kulala chukua tahadhari kama mwanao anaota akiwa anatembea usiku, watoto wenye ndoto za hofu wanatoka kitandani wakati mwingine, hivyo basi okota midoli au vitu chini sakafuni vinavyoweza kumtega, hakikisha milango na madirisha yamefungwa.

Chanzo na jinsi ya kujilinda na ndoto za hofu

Hakuna njia ijulikanayo ya kumlinda mwanao katika matukio haya, kwasababu hakuna anayejua nini chanzo chake.

Ndoto za hofu zinazaweza kusababishwa na kukosa usingizi wa kutosha au kunyimwa usingizi. Inaweza kusababishwa pia na msongo wa mawazo au kuchoka sana. Kuna ushahidi pia tatizo hili linarithiwa ndani ya familia. Jambo linalojulikana ni ndoto za hofu hazimaanishi mtoto ana matatizo ya kisaikolojia au amekasirishwa na kitu.

Tatua shida ya mwanao ya kukosa usingizi wa kutosha inayojumuisha kuamka katikati ya usiku na hakikisha anapata usingizi mara kwa mara kwa kufuata utaratibu mzuri wa kulala.