Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ugonjwa wa Tetekuwanga kwa Watoto

Ugonjwa wa Tetekuwanga ni nini?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kirusi kinachoitwa “varicella-zoster”, watoto wengi wanapata tetekuwanga wakiwa wadogo na inakua ugonjwa mdogo.

Mara baada ya mtoto kushika kirusi, dalili zinaweza kuchukua wiki moja na wiki tatu kuonekana.

Dalili za ugonjwa wa tetekuwanga

Dalili inayoonekana zaidi ni upele. Inaanza kama kidoti kidogo chekundu na kukua kufanyika lengelenge ndani ya masaa machache. Utaanza kuona kwanza usoni kwa mtoto wako. Viupele vitaanza kuenea kifuani na tumboni, alafu sehemu nyingine za mwili.

Alama na malengelenge yanaweza kuonekana sehemu nyingine, na zitaweza kumsumbua mwanao zaidi kama yametokea maeneo ya mdomoni na shingoni na kuzunguka sehemu zake za siri.

Mtoto anaweza kusikia kuchoka na kuumwa, na anaweza pia kuwa na:

  • homa
  • kuumwa na kupata maumivu
  • kukosa hamu ya kula.

Jinsi gani ugonjwa wa tetekuwanga unatibiwa?

Unaweza kumtibu mwanao tetekuwanga nyumbani, unaweza kutibiwa au kuzuiliwa na antibaiotiki ili vipele visipate maambukizi, ila kiuhalisia ugonjwa wa tetekuwanga hupotea wenyewe baada ya wiki.

Zifuatazo ni njia zinazoweza kumsaidia mtoto mwenye tetekuwanga:

  • Mpatie maji ya kutosha ili asipate upungufu wa maji mwilini.
  • Muogeshe na maji ya uvuguvugu. Jaribu kuongeza magadi soda, hakuna ushahidi kwamba magadi yanasaidia kupunguza muwasho ili wamama wengi wanatumia njia hii sana na inasaidia. Hakikisha unamkausha vizuri baada ya kuoga.
  • Hakikisha kucha za mwanao ni fupi, ili kuepusha mtoto kujikuna na kupata makovu baadae.
  • Mvalishe mwanao nguo za pamba zisizombana kusaidia ngozi yake kutulia na kupunguza muwasho.

Unaweza kumpa mtoto paracetamol ili kupunguza joto la mwili na kupunguza maumivu na kuumwa. Unaweza mpatia mtoto piriton kama ana umri zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuongea na mshauri wa afya.

Ni vizuri mtoto wako kubaki nyumbani mpaka tetekuwanga zitakapo kauka ili kuwalinda wengine wasipate kwasababu inaenea kwa haraka zaidi.

Ikiwa hjawahi kupata tetekuwanga kabla, unaweza kupata sasa kutoka kwa mwanao. Muone daktari kama unahisi una tetekuwanga maana ni ugonjwa mkubwa sana kwa watu wazima. Hii ni muhimu sana kama una ujauzito, au unahisi una ujauzito.

Tetekuwanga inaweza kuwa hatari kwa mtoto ambaye hajazaliwa. Kama ulishapata tetekuwanga mwanzoni, kuna nafasi ndogo sana ya kupata tena.