Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Miadi ya Mama Mjamzito Baada ya Kujifungua

Vipimo gani ninaweza kufanyiwa?

Daktari wako anaweza kukupima shinikizo la damu na kushika tumbo lako kuangalia kama mfuko wa uzazi umejirudi na kujibana vizuri. Anaweza kukupima uzito na kukushauri njia tofauti za kupunguza uzito ulioongezeka kipindi cha ujauzito.

Anaweza kukupima zaidi upungufu wa damu, kidonda ulichochanwa wakati wa kujifungua. Kidonda cha operesheni na matiti yako kama atakua ana wasiwasi.

Unaweza kushindwa kujizuia hasa ukiwa unasikia mkojo au wakati mwingine kukosa choo.Kama ulichanwa sana wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida ili kuongeza njia ya mtoto, utagundua unajamba bila kutegemea au kujisaidia haja kubwa(kidogo). Mazoezi ya sakafu ya nyonga yanaweza kusaidia kurejesha udhibiti wa mwili wako na daktari anaweza kukuelekeza njia nzuri ya kufanya.

Daktari anaweza kukuliza unajisikiaje juu ya ujio wa mwanao. Anaweza kuuliza kama unapata msaada wa kutosha kutoka kwa ndugu zako. Huu ni wakati mzuri wa kuleta hoja yeyote inayokusumbua, sema pia kama una wasiwasi au una kosa mda wa kulala.

Ni salama kujamiana tena baada ya wiki sita?

Sio lazima, maana kuamua kuanza kufanya mapenzi tena ni jambo binafsi. Ikiwa una wasiwasi juu ya hili au ulijaribu ukapata maumivu ongea na daktari wako.

Hata kama hujaanza kujamiana tena, daktari atakuuliza kama utapendelea kutumia njia za uzazi wa mpango. Uwezo wako wa kupata ujauzito utarudi haraka, hasa kama hunyonyeshi, hata wanawake wanaonyonyesha mayai yao yanaanza kupevushwa baada ya miezi michache baada ya kujifungua.