Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Msongo wa Mawazo Baada ya Kujifungua

Msongo wa mawazo ni jambo la kawaida linalowapata angalau mwanamke (mama mpya) mmoja kati ya nane.

Dalili zake ni pamoja na kusikia mchovu, kulia, mwenye shahuku, mnyonge na mabadiliko ya kula na kulala hasa wiki ya tano za kwanza baada ya kujifungua. Wakati mwingine kuwa na huzuni, kushindwa kufurahia chochote, kukosa matumaini, kusikia mwenye hatia.

Matibabu ya msongo wa mawazo ni pamoja na matumizi ya dawa za kupunguza mawazo, ushauri nasaha au yote pamoja.

Chanzo cha msongo wa mawazo

Wataalamu hawajui kwanini baadhi ya wanawake wanapata msongo wa mawazo na wengine hawapati. Unaweza kuwa sawa kwa mtoto wako wa kwanza lakini ukapata msongo wa mawazo kwa mtoto wako wa pili.

Wakati mwingine mambo unayopitia kila siku yanakua mengi na kukufanya ushindwe kujiangalia wewe na mwanao vizuri, kula na kupumzika vizuri. Baadhi ya hali zinakufanya uone maisha magumu kukubaliana nayo, baadhi ya hali hizo ni kama:

  • Ulishawahi kupata msongo wa mawazo hapo awali katika ujauzito uliopita au una tatizo la kiafya la msongo wa mawazo.
  • Hakuna msaada mzuri kutoka kwa baba wa mtoto, familia na marafiki.
  • Kipato cha shida, na kulea mtoto inakua mzigo.
  • Ulipata shida wakati wa kujifungua
  • Kunyonyesha ni kazi ngumu kwako.
  • Kumbukumbu mbaya kama kufiwa na mzazi wako.

Jinsi gani ya kutibu msongo wa mawazo?

Kwa msaada kutoka kwa familia,marafiki na mkunga wako au mshauri wako wa afya, utapona. Kumbuka kuwa na msongo wa mawazo haimaanishi wewe ni mama mbaya. Msongo wa mawazo unaweza kutibiwa kwa njia zifuatazo:

  • Ushauri nasaha katika kliniki za mama na mtoto na kuongea na marafiki, familia na mwenza wako kukusaidia
  • Matumizi ya dawa za kupunguza shahuku na zinazosaidia kurudisha homini katika hali ya kawaida. Ongea na daktari kupata uelewa mzuri katika hatari na faida za kuhusika katika matumizi ya dawa hizi ikiwa unanyonyesha.

Nifanye nini niweze kushindana na msongo wa mawazo?

 

Jaribu kupata mapumziko ya kutosha

Lala au pumzika unapoweza. Ikiwa kuna mtu wa kukusaidia kumuangalia mtoto pumzika masaa kadhaa, sikiliza mziki unaopenda (kama unapenda mziki), kunywa kinywaji cha moto kisha pumzika.

Kula kwa afya, mlo kamili

Kwasababu ya mahitaji mapya ya mwili wako, kula vizuri ni jambo la muhimu. Usikae mda mrefu bila kula. Mlo kamili utaongeza nguvu ndani ya mwili wako na kuzuia uchovu.

Fanya mazoezi

Mazoezi yanasaidia kujisikia vizuri mwili na akili, japokua ni jambo la mwisho unalo jisikia kufanya. Mazoezi ya kujinyoosha ya yoga ni mazuri wakati huu pamoja na mazoezi mepesi uliyokua unafanya wakati wa ujauzito.

Kutana na wamama wapya wengine.

Katika kliniki za mtoto kukutana na wamama wengine itakusaidia kupata ujuzi na njia za kukubaliana na kipindi hiki.

Jipende

Kujiangalia na kujipenda wewe na mwanao ni mambo ya muhimu. Usijilundikie kazi nyingi zisizo muhimu kwako na kusahau kupumzika na kumuangalia mwanao.