Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Namna ya Kuondoa Michirizi Baada ya Kujifungua

Michirizi ni kitu cha kawaida baada ya kujifungua. Utakua na mistari myembamba kwenye maeneo yenye mafuta mengi kama matiti, mapaja, tumbo na mengineyo. Huweza kutokea kutokana na mabadiliko ya homoni au kupotea kwa mafuta katika maeneo haya.

Je, inawezekana kuondoa michirizi?

Michirizi huwa myembamba kadiri ya muda unavyoenda lakini huwa haipotei. Kuna njia za asili za kuweza kuifanya isionekane kwa urahisi. Unaweza ukatumia mafuta ya “massage”, losheni, mafuta ya kulainisha ngozi nk.

Baaada ya miezi kadhaa au hata miaka michirizi hubadilika na kuwa myembamba na kufanana na ngozi

Namna ya kuondoa michirizi kiwa nyumbani

Kuna njia za nyumbani za kuondoa michirizi kwa uhakika mara baada ya kujifungua kama vile;

1. Matibabu ya mafuta

Kusugua maeneo yenye michirizi kwa mafuta huweza kusaidia kupunguza michirizi kwa kiwango kikubwa na kulainisha ngozi.

Mafuta ya olive: olive ni mafuta yenye kulainisha ngozi na pia husaidia kuzunguka kwa damu, na kupunguza michirizi kwa kiwango kikubwa.

 • Weka mafuta katika kiganja chako na taratibu sugua eneo lenye michirizi
 • Acha dakika 30 ili vitamin A,D,na E ziingie kwenye ngozi yako.
 • Oga baada ya kusugua.
 • Ingawa ni kitendo kinachochukua muda kitakupa matokeo unapokifanya kila mara
 • Au unaweza kuandaa mchanganyiko wa olive maji na “vinegar”ili upake usiku wakati wa kulala.

Mafuta ya nyonyo

 • Paka mafuta ya nyonyo kwenye michirizi na usugue taratibu kwa mduara.
 • Tumia mfuko wa plastiki ufunike uliposugua joto litafungua vinyweleo ili mafuta yaingie.
 • Safisha eneo husika na urudie kula siku, ndani ya mwezi mmoja tu, utapata matokeo mazuri.

Matibabu ya Mafuta muhimu

 • Chukua mafuta ya kawaida kama vile mafuta ya nazi
 • Dondosha matone kadhaa ya mafuta muhimu kama ya ua waridi
 • Tumia mchanganyiko huu kusugua kwenye michirizi ndani ya dakika 30 itasaidia kuondoa michirizi.

2. Aloe Vera

Aloe vera inasaidia kulainisha ngozi. Tumia inayopatikana fresh kuliko ile ya sokoni.

 • Paka juu ya ngozi, acha dakika 15 na safisha kwa kutumia maji ya uvugvugu. Rudia mara kwa mara.

3. Asali

Viwango vya viondoa sumu ndani ya asali husaidia kuondoa michirizi.

 • Chukua kipande cha nguo paka asali
 • Kiweke kipande hicho kwenye eneo lilioathiriwa acha mpaka ikauke
 • Safisha na maji ya vuguvugu
 • Au unaweza kuandaaa mchanganyiko wa asali na grycelin, upake kwenye michirizi na uache mpaka ukauke na uoshe na maji ya vugu vugu

4. Sehemu nyeupe ya yai

Maji meupe ya yai ni mazuri kwa protin na husaidia kufanya ngozi iwe na unyevu na kuonekana mpya.

 • Koroge ute mweupe wa yai na uma
 • Safisha eneo lenye michirizi na upake eneo kwa kutumia brashi laini
 • Acha ikauke
 • Paka mafuta ya olive kufanya ngozi iwe laini
 • Rudia kila siku japo kwa wiki mbili mpaka michirizi ianze kupotea.

5. Siagi ya nazi

Siagi ya nazi inaweza kutumika kama tiba, ni moja ya vilivyomo katika losheni  nyingi tu. Chukua siagi kidogo, na upake kwenye michirizi kila mara, na usuuze mara kwa mara.

Matibabu haya husaidia uvutikaji wa ngozi,kuzuia kukauka kwa ngozi na kupunguza michirizi.

6. Sukari

Sukari ni moja kati ya tiba muhimu za kuondoa michirizi, ambayo huondoa ngozi iliokufa na kufanya ngozi kung’aa

 • Chukua kijiko cha chakula cha sukari
 • Tumia kwa kusugulia kabla ya kwenda kuoga
 • Fanya kila siku ndani ya mwezi.

7. Juisi ya limao

Viwango vya asidi vilivyoko ndani ya limao huondoa michirizi

 • Paka juisi freshi ya limao kwenye eneo lenye michirizi
 • Acha kwa dakika 10 ili juisi iingie
 • Safisha na maji ya vuguvugu
 • Paka kila siku kwa matokeo mazuri
 • Au unaweza kupaka mchanganyiko wa limao na tano uliolingana kwenye eneo lililoathirika.

8. Maji

Ngozi yako lazima iwe na maji ya kutosha ili kuweza kuondoa alama za michirizi katika ngozi yako, hivyo kunywa maji japo glasi 10 au 12 kila siku ili kukinga ngozi yako na sumu mbalimbali. Achana na soda chai kahawa kwani huondoa maji mwilini.

9. Juisi ya viazi

Viazi vina kemikali zinazosaidia mwonekao wa ngozi

 • Kata kiazi vipande viwili, paka kiazi kwenye michirizi
 • Ruhusu juisi ya kiazi kuingia kwenye ngozi na uache ikauke
 • Safisha na maji ya vuguvugu
 • Na utaona mabadiliko ndani ya muda mchache.

10. Binzari na msandali (Sandalwood)

Vinajulikana kwa kuongeza mng’ao na hisia ya ngozi

 • Andaa kijiko kimoja cha “sandalwood” kwa kusugua kipande cha “sandalwood” kwenye maji
 • Andaa mchanganyiko laini wa mzizi wa binzari
 • Changanya vyote kwenye kiwango sawa
 • Acha ikauke japo asilimia sitini 60% alafu sugua kwenye ngozi yako
 • Rudia kila siku japo kwa miezi sita utaona mabadiliko.

11. Maziwa, sukari na maji ya kijani ya tango na limao

 • Changanya vijiko viwili vya maziwa , na uchanganye na matone ya juisi ya limao na tango, na nusu kijiko cha sukari
 • Weka mchanganyiko kwenye michirizi ndani ya dakika 5.
 • Safisha na maji ya vuguvugu
 • Paka maji ya nazi na uache yakauke mpaka utakapohisi kuvutika kwa ngozi
 • Alafu paka aloe vera
 • Unaweza kurudia kitendo hiki mara tatu kwa wiki ili kuondoa michirizi