Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Anahitaji Usingizi Kiasi Gani?

Kiasi gani cha usingizi mtoto wako anahitaji?

Ni muhimu kujua ni kiasi gani mtoto wako anahitaji kulala katika kila hatua ya ukuaji wake. Kuelewa mahitaji ya mtoto wako husaidia kuwa na mpangilio mzuri. Kwa mfano, wakati mtoto wako akiwa mchanga anahitaji usingi mwingi. Watoto wengi wachanga hulala kati ya masaa 16 hadi 18 kwa siku mpaka wafikapo miezi miwili.

Lakini usitarajie usingizi huo mrefu uje wakati wa usiku, wakati mtoto wako ni mchanga, anahitaji kula kila baada ya masaa mawili. Tumbo lake ni dogo sana na hupokea maziwa kidogo kidogo kila anaponyonya. Ni asili kwa watoto wadogo kulala kwa muda mfupi. Kutarajia mtoto wako atalala zaidi inaweza kukufanya uchanganyikiwe.

Watoto wadogo hawajui kujituliza ili walale peke yao bado. Hapa ndipo kubembeleza kunapokua kugumu. Kama unajali juu ya kumuharibu mtoto wako mdogo kwa sababu ya kumbembeleza, usijali. Unaweza kumfundisha kujituliza mwenyewe wakati wa kulala.

Muda ukifika akishaweza kubeba chakula cha kutosha tumboni, atapata uwezo wa kulala muda mrefu usiku. Kati ya miezi miwili na minne, mtoto wako ataweza kulala kwa masaa tano au sita usiku. Ingawa sio masaa nane uliyofikiria, ila bado ni maendeleo kutoka kuamka kila masaa mawili mpaka matatu.

Karibia miezi minne mpaka sita, mtoto wako anaweza acha kunyonya na kulala kwa masaa sita mpaka 12 usiku. Ni vyema kujua, watoto wanatofautianana na haya yanaweza kubadilika, ila utafiti unaonyesha asilimia 60 ya watoto wanalala usiku mzima katika umri wa miezi sita. Kama mtoto wako ni miongoni mwa asilimia 40 ambayo haijafikia hatua hii bado, basi kuwa mvumilivu na subiria. Katika miezi tisa, asilimia 80 ya watoto wanalala usiku mzima.