Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Umuhimu wa Ratibu ya Kulala kwa Mtoto

Umuhimu wa kuwa na ratiba ya kulala

Utakuwa umejifunza kutoka kwenye vitabu au wamama na walezi wengine, kuhusu umuhimu wa kuwa naratiba ya kulala kwa mtoto wako. Ratiba tulivu nay a kuzingatiwa itampatia mtoto ishara ya kujua mda wa kwenda kulala. Ratiba hi nzuri ya kulala inaweza kumsaidia mtoto kupumzika na kupotelea usingizini kiurahisi.

Utaratibu mzuri wa kulala ni mda muafaka wa kuungana na mtoto wako. Ni muda mzuri wa kupumzika na kumkumbatia mtoto wako. Ikiwa mtoto wako amekata kunyonya kwa chupa,hakikisha unamnyonyesha vizuri kabla ya kulala. Wakati wa kumbembeleza na kumlaza mtoto ni vizuri na baba yake akahusika katika ratiba hii ili kuwaunganisha baba na mtoto.

Utaratibu mzuri wa kulala unasaidia watoto kujua tofauti ya mchana na usiku, hata watoto wachanga.

Kumsaidia mtoto kuelewa tofauti hii, ungana nae kadiri uwezavyo mchana. Hakikisha chumba kina mwanga wa kutosha. Cheza nae nje kidogo kama hali ya hewa inaruhusu. Shughuli zote hizi zitamsaidia mtoto kuelewa mchana ni mda wa kuwa mchangamfu na kucheza. Wakati wa usiku fanya kinyume na shughuli za mchana,hakikisha chumba kina mwanga duni na tulivu. Mfundishe mwanao kuwa usiku ni wakati wa kulala.

Msaidie mtoto kutulia wakati wa usiku. Unaweza kumuogesha na kumvalisha nguo zake za kulala, kumlisha,kumuimbia nyimbo laini za kulala na kumkumbatia sana. Ondokana na shuhuli zitakzomfanya awe mchangamfu.

Kumbuka kuzingatia utaratibu huu wa kulala na kufanya marekebisho kidogo kadiri mwanao anavyokua.