Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Kulia Kupi kwa Watoto ni Kawaida?

Kujua uliaji wa kawaida kwa watoto ni ngumu, kwasababu watoto wote wanalia. Ki ukweli, baadhi ya wataalamu wametabiria kuwa watoto wachanga wanalia saa moja na nusu kwa siku, na kuendelea mpaka masaa matatu kwa siku ndani ya umri wa wiki sita.

Bado, kuna uliaji ambao unaonekana sio wa kawaida. Lakini je, tutaugunduaje, na nini cha kufanya kama kulia kunaonekana kumezidi kawaida?

Kama una mtoto anaye lia sana, utakuwa umesikia kwa marafiki kwamba huenda mtoto wako ana maumivu ya chini ya tumbo. Watoto walio na maumivu haya ya chini ya tumbo wanalia sana wakati wa usiku, na kuanza kulia hakuna tahadhari au sababu na hukataa kutulizwa. Pia wanalia kwa muda mrefu na kukunja uso wao, kama wako kwenye maumivu.

Habari njema ni kwamba maumivu haya ya chini ya tumbo yanaweza kupotea. Lakini unajuaje kama mtoto wako anasumbuliwa na hili tatizo au ni maumivu ya kawaida? Jibu ni kwamba usikae kuogopa kuomba ushauri kwa mtaalamu wako wa afya kama una wasiwasi mtoto wako analia zaidi ya kawaida. Wakati mwingine watoto wanasumbuliwa na matatizo ya chakula unachokula wakati unanyonyesha, au chakula anachokula yeye,na hili linachangia maumivu na kuongezeka kwa kilio. Kwa hiyo jiamini na usiwe na wasiwasi kuomba msaada wa kiafya.

Kama mtoto wako analia zaidi ya kawaida, au kama sauti yake ni ya juu sana, muone daktari. Unajua maisha ya mtoto wako sana zaidi ya mtu yeyote, kwa hiyo kama umegundua chochote kisicho sawa, kama kulia kwa uhafifu au kulia kwa sauti ya chini, au kulia kwa tofauti au kama inaonekana kama mtoto wako ana maumivu usisite kumwona daktari