Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Vidokezo Muhimu Kuhusu Usalama wa Mtoto Wako

Tumeongelea baadhi ya mambo mbalimbali kuhusu usalama wa mtoto unayoweza kukufanya,ufuatao ni muongozo mfupi utakaokusaidia kama mzazi kumuweka mtoto katika hali ya usalama.

Bafuni: kamwe usimuache mwanao ndani bafuni au kwenye maji mwenyewe. Kumbuka inachukua dakika chache mtoto kuzama na kufariki ndani ya maji, kuliko vile unafikiria.

Mda wa kucheza na wanyama kama mbwa, paka na kuku: kumbuka kuchukua tahadhari ukimruhusu mtoto wako kucheza na wanyama hawa. Daima kuwa karibu nao pale wanapocheza, taratibu muonyeshe mtoto wako jinsi ya kucheza na paka au mbwa bila kung’atwa.

Usalama katika dawa: watoto wanapenda kuchunguza na kupeleleza vitu. Weka mbali na watoto dawa na virutubisho vya aina yoyote,  ikiwa mwanao atafikia na kutumia dawa, mkimbiza hospitali au mpigie simu mtaalamu wa afya.

Jikoni: kadiri mwanao anavyokua na kuanza kutambaa au kutemba, ataenza kukufuata na kuiga kila unachofanya. Hii inamaanisha atajaribu kushika sufuria za moto, visu na vitu vingine hatari jikoni. Weka hali ya usalama jikoni kama kutengeneza geti dogo kuingia jikoni ili kumzuia mwanao kufika wakati unaandaa chakula. Pia jitahidi kuweka visu na vyombo vingine vya hatari mbali na sehemu mwanao anaweza kufikia.

Anza kutafuta msaidizi mzuri kwaajili ya kumuangalia mtoto.