Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miaka 5

Mtoto wa umri huu:

 • Anaweza kuvaa mwenyewe isipokuwa kufunga viatu.
 • Anaweza kuruka na kutua na mguu mmoja.
 • Anaweza kutupa mpira na kudaka.
 • Anauliza maswali mengi na ana shahuku.
 • Anaigiza wengine.
 • Anatambua herufi na namba.
 • Anaweza kuiga kuimba nyimbo, hadithi.
 • Anashirikiana na wenzake kwenye michezo.
 • Anasaidia watu nyumbani.
 • Anaelewa hisia za watu wengine.

 

Ukuaji wa kimwili katika umri huu

 • Anakomaa kiakili
 • Anaweza kusimama na mguu mmoja bila kuyumba
 • Anashuka ngazi bila kujishika
 • Anakimbia na kusimama bila kuanguka
 • Anaweza kuruka juu ya matofali na miguu yote bila kuanguka
 • Anaweza kuruka urefu wa hatua tatu na kutua na miguu yote

 

Maendeleo ya mtoto katika jamii ndani ya miezi hii

 • Anapenda kujitegemea lakini bado anatumia mda wake na wazazi wake.
 • Mtoto aliye na miaka 5 anapenda kujihusisha na mengi, na mara nyingi atakataa msaada wako.
 • Wanafanya usafi wenyewe, wakati mwingine bila kuamriwa.
 • Wapenda kubembeleza wenzake hasa kama walihusika katika ugomvi.
 • Wanaweza kujielezea wanavyohisi, mfano “huzuni, hasira, kuchanganyikiwa , uoga,kuvunjika moyo” n.k
 • Wanakua kipaji cha kuwasiliana na kujadiliana na marafiki zake katika michezo yao.
 • Wanaweza kuwa na rafiki mmoja kipenzi.
 • Wana vipaji vingi vya kushirikiana na rafiki zake wengine.
 • Wanashiriki katika kazi za vikundi shuleni na wanaweza kusubiria zamu yao kuongea au kufanya onyesho.
 • Wazazi na walimu ni watu muhimu kwao, na chanzo cha habari na faraja.
 • Wanaanza kufuata kanuni na sheria na wakati mwingine wanakumbusha wenzao, bila maelekezo ya mwalimu au mzazi.

 

Hatua za ukuaji katika kuongea na kujifunza

 • Wanaelezea mahitaji, hisia, na mawazo yao.
 • Wanapenda kupata habari zaidi.
 • Wanafanya suluhisho la matatizo na kuchunguza mawazo yao.
 • Wanafanya mipango ya vitu wanavyohitaji.
 • Wanashauri wenzao na kutetea mada.
 • Wanatengeneza na kuhadithia hadithi.