Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 10

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

  • Anatambaa vizuri
  • Anazunguka na kuchunguza sana
  • Mtoto ataanza kuchunguza vitu katika njia tofauti kama kugongagonga, kutupa na kutikisa

Hatua za ukuaji zinazojitokeza(nusu ya watoto wanazifikia)

  • Anasema mama au baba.
  • Ananyooshea mkono vitu vilivyo mabali.
  • Anaitikia ukimwita na anaelewa maana ya neno HAPANA.
  • Anaonyesha anachotaka kwa kuonyesha ishara.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

  • Anaweza kutumia kikombe mwenyewe.
  • Kusimama mwenyewe kwa sekunde chache.
  • Ataanza kujilisha mwenyewe baadhi ya vyakula kama matunda yaliyokatwa vizuri.