Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Miezi 2

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaanza kutoa sauti, milio ya kitoto na minong’ono.
 • Ataanza kufuatilia vitu kwa macho na kuwagundua watu aliowazoea kwa mbali.
 • Anagundua mkono wake.
 • Atanyanyua kichwa chake juu kwa muda mfupi.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kutabasamu,kucheka
 • Kuinua kichwa digrii 45.
 • Kusogeza miguu na mikono taratibu.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kujiinua unapomlaza tumboni kwako.
 • Kuhimili uzito wake kwenye miguu yake
 • Kukihimili kichwa chake kwa uimara
 • Atajibembeleza mwenyewe kwa kuweka mkono mdomoni.

Ataanza kunung’unika na kusumbua pale anapochoshwa na kitu au mdoli.