Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Hatua za Ukuaji: Mtoto wa Mwaka 1

Hongera! Mtoto wako sasa si kichanga tena, na ametimiza mwaka mmoja.

Hatua mwanao alizofuzu (watoto wengi wanazifikia)

 • Anaigiza kazi za watu wengine kama kupika,kuongea na simu-mara nyingi anaigiza kile alichoona wewe na mwezi wako mnafanya.
 • Kupiga makofi, kuaga na kuonyesha kitu kwa kidole.
 • Kutumia ishara muhimu kama kutikisa kichwa akisema hapana au kupungia mkono akiaga.

Hatua za ukuaji zinazojitokeza (nusu ya watoto wanazifikia)

 • Kuitikia na kuelewa maswali rahisi utakayomuuliza na uelekeo mfano: njoo hapa.
 • Atasema maneno kama “mama” au “baba” na mishangao kama”aaah, ooho”
 • Mtoto ataanza kutembea hatua chache bila kushikwa na mtu.
 • Kusimama mwenyewe.
 • Wanatambua vitu na kukiangalia mara utakapokitaja.

Hatua za mapema kabla ya wengine (watoto wachache wanazifikia)

 • Kutembea vizuri
 • Kutumia vitu sawa kama kunywa maji kutumia kikombe, kuchana nywele kwa chanuo.
 • Mtoto kuelewa maneno kama kunywa, gari au mpira.
 • Anasema maneno mengine mawili ukiachana na mama na baba.