Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 2 na Miezi 10 – (Miezi 34)

Jinsi mtoto anavyokua

Kama mtoto amekua, atapendelea zaidi ujamaa. Mtoto wako anaweza kufikiri na kuanzisha urafiki na watoto wa umri wake pamoja na kucheza nao. Atajifunza kushirikiana ni sehemu ya urafiki.

Watoto wawili wanaweza kuwa wasumbufu lakini watoto wa umri huu ila  wanapenda  na kusaidiana , wanapenda kuwa  sehemu ya ulimwengu unaowazunguka na kuwaiga watu wanaowazunguka. Mtoto wako atataka kupanga meza na kubeba midoli. Fanya kile anachokipenda kuwa bora na mpongeze na kumsaidia. Hii itamuongezea uwezo wake wa kujiamini.