Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 2 na Miezi 11 – (Miezi 35)

Jinsi mtoto anavyokua

Kwa sasa mtoto wako anweza kuhitaji kuvaa nepi mara moja kwa siku. Wakati huu mtoto atapunguza kuchafua nguo iwe mchana au wakati amelala, ataweza kumuita yeyote. Umri huu mtoto anahitaji uhuru na faragha kumfanya ajisikie kuwa huru na kutulia.

Atavutiwa na vitu tofauti tofauti kati ya wavulana na wasichana, hii ni kawaida wakati wa mtoto kukua, hivyo jitahidi usikasirike sana pindi ukigundua mtoto wako anaonyesha sehemu zake za siri kwa mtoto mwenzie. Kama unajisikia una nguvu katika hilo mkatize kwa kumpa shughuli nyingine.

Mtoto wako atazingatia vema shughuli moja na itamuendeleza zaidi katika tamaduni na ujamaa. Anaweza kuanza mapema michezo ya kuchora na mengineyo.