Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 2 na Miezi 5 – (Miezi 29)

Jinsi mtoto anavyokua

Kwa sasa mwanao anaweza kufanya baadhi ya vitu kama kuvaa nguo na kutaja sehemu kuu za mwili. Pia anaweza kutambua rangi chache na majina ya rafiki zake.

Kama jinsi anavyokua zaidi atatambua jinsi wengine wanavyofikiri na kuhisi. Atavutiwa sana kucheza na watoto wenzie tofauti na kuwa mbali nao.

Mazungumzo yakuvutia kati yako na mwanao yatamuimarisha zaidi mwanao uwezo wake wa kuzungumza, kwa mfano mtoto akisema “gari nenda” unatakiwa kusema “ndiyo, gari ya rangi nyekundu imekwenda mjini haraka” hataweza kuunda sentensi ngumu pekee ila atajifunza kutokana na mifano yako mda wote.

Uvumilivu wako unaweza ukapungua pale mtoto wako anapokujaribu au kushindwa kukuelewa, jaribu kuwa katika nafasi yake. Atajihisi kukasirika anapoona hawezi kuvidhibiti vitu vyote vilivyomzunguka hivyo msaidie kwa kumfanyia wepesi ili kuepuka ugomvi au kumkwaza.