Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 2 na Miezi 7 – (Miezi 31)

Jinsi mtoto anavyokua

Mtoto wako anaweza kutambua vema jinsi vitu vinapaswa kufanyika, atajisikia vibaya kuona vitu vinakwenda isivyopangwa.

Kipindi hiki mtoto anaweza kukuuliza maswali kama vile mtoto anavopatikana wapi? Jaribu kumpa majibu rahisi na ya kweli. Huu utakua ni muda sahihi wa kumtambulisha viungo vya mwili kwa majina sahihi kama sehemu za mwili. Hakuna haja ya kumpa taarifa nyingi. Kadri unavompa majibu magumu ndivyo unavyozidi kumchanganya mtoto.