Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 2 na Miezi 9 – (Miezi 33)

Jinsi mtoto anavyokua

Mtoto wako sasa anakaribia miaka mitatu tangu kuzaliwa, utamuona sasa anakua mwelewa na hisia za watu wengine. Atashangaa kwa nini bibi yupo tofauti au dada yake ana huzuni. Muelezee sababu iliyomfanya bibi akasirike kwa hali ya upole. Jitahidi ajifunze kuelewa hisia za watu wengine na kuchukulia kawaida, ni vizuri kumuelezea hivyo mtoto itamsaidia kuiga atakapojiskia vibaya au kukosa furaha.

Mwenendo wa mtoto wako kama ukimya, mwenye kupenda kufahamu na kuongea unakua wazi. Unaweza kumuhimiza kuweka wazi utofauti wake, muonyeshe kuwa unampenda na kumkubali jinsi alivyo. Kama anajisikia aibu msisitize akutane na watoto wengine lakini usimfanye ajisikie vibaya kama anapendelea kuangalia kuliko kushiriki na watoto wenzie. Heshimu maamuzi yake itamsaidia kujiamini zaidi na kujihisi bora.