Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 3 na Miezi 2 – (Miezi 38)

Jinsi mtoto wako anavyokua

Uwezo wa mwanao kushika baadhi ya maneno, utakusaidia kumuelewa zaidi ya robo tatu ya anachosema.

Hata kama ameweza kujisaidia mwenyewe, tegemea ajali za hapa na pale hasa usiku kwa miezi au hata miaka ijayo. Kutokojoa usiku ni hatua ya mwisho ya watoto kufanikisha na inakua ngumu kwa wakiume zaidi ya wakike. Usiwe na shaka, kwa kawaida watoto wengi wanaacha.

Mtoto wako anaweza cheza na wenzake ila sio kwa mda mrefu. Watoto wengi wenye miaka mitatu wanapenda kucheza wenyewe lakini karibu na rafiki zake, au kujumuika ila sio zaidi ya lisaa. Kwanzia mwaka ujao mtoto wako ataweza kucheza na wenzake kwa muda mrefu zaidi. Baadhi ya watoto walio na aibu watahitaji mda kidogo kuzoeana na wenzake.

Maisha yako sasa

Usifikirie ni ndoto ya kutisha pale mwanao atakapoanza kulia usiku, hii ni hali nyingine inayohusiana na hofu ya usiku.

Hofu ya usiku inatokea pale mtoto anapoamka kutoka kwenye usingizi mzito na kuwa katika usingizi mwepesi mara nyingi ni kati ya saa nne na saa sita usiku. Mtoto wako anaweza amka na kukaa kitandani kisha kupiga mayowe au kujitupa, kutoka jasho na kuhema kwa nguvu. Hata kama atakua amefungua macho anakua hajaamka au kukuitikia. Kiukweli ni vigumu kumuamsha mtu akiwa katika hofu ya usiku, hivyo usijaribu. Kaa nae na hakikisha yuko salama. Hatakumbuka lolote akiamka asubuhi.