Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miaka 3 na Mwezi 1 – (Miezi 37)

Jinsi mtoto wako anavyokua

Ulimwengu wa ukuaji kwa mwanao unahusisha vitu vingi kuanzia mda anapokua kwa daktari wa meno mpaka anapoenda kucheza na rafiki zake, labda hata chekechea. Tabia nzuri inaanza kuonekana sasa, na kama mzazi mwenye subira utamfundisha ujuzi mpya mtoto na kumsaidia kujifunza kujisaidia (kukojoa na haja kubwa) pale anaposhindwa.

Watoto wenye miaka mitatu wanaanza kujifunza rangi. Wanaweza kuonyesha rangi ya kitu pale unapowauliza na kuzitaja kwa majina mbili au tatu akifika miaka mitatu na nusu. Jaribu kufanya maongezi na mtoto wako kwa kuhusisha rangi,kwa mfano : fulana yako ina rangi gani leo?

Maisha yako sasa

Kupata mda wa kupumzika sasa ni njia nzuri ya kurudisha nguvu. Hivyo, usijisikie vibaya kumuacha mwanao nyumbani na kutoka ili kujipatia mda wako mwenyewe. Na usimfiche mwanao unapoenda, muage na mueleze ukweli kwamba unatoka na rafiki zako kuenda kuangalia sinema. Ni vizuri mwanao kukuona ukiwa na furaha itamjengea tabia ya kuwajali watu. Mfahamishe nini kitatokea mara utakapoondoka,kama vile nani atabaki nae.