Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miezi 10

Jinsi mtoto wako anavyokua

Mtoto wako anaanza kuelewa maneno na sentensi rahisi, hivyo basi ni muhimu sasa kuendelea kuongea nae. Anza kumfundisha kuongea kwa kurudia maneno anayoyasema ila ukitumia lugha sahihi.

Japo wakati mwingine inaweza kuwa ujinga, kuwa na mazungumzo na mtoto wako ni njia nzuri ya kukuza ujuzi lugha yake. Pale atakapozungumza sentensi isiyoeleweka jaribu kumjibu kwa uchangamfu mfano: oowh kweli? Inapendeza! Atacheka na kuendelea kuongea na wewe.

Wakati unaongea na mtoto wako muangalie kwenye macho na usubiri na yeye akujibu. Haijalishi ni kipi mnaongea, tumia maneno mengi ya tofauti. Jaribu kuelezea unachokifanya ukiwa unazunguka nyumbani, au kunyooshea kidole vitu vyenye kukupendeza katika mizunguko yako.

Maisha yako: Kuulinda mgongo wako

Mtoto wako anaendelea kuongezeka uzito, kwahiyo ni vema kuchukua tahadhari za kuzuia ili kuhakikisha hauko katika hatari ya kuvuta msuli au kujiumiza wakati ukimbeba au kunyanyua. Mara nyingi kunja magoti yako na kumbuka kuchuchuma, kuliko kuinama kiuno,wakati unambeba mtoto juu. Hii itasaida kutwika uzito wake wote kwenye misuli ya miguu, kuliko kuhatarisha kuuvuta mgongo wako.

Kama wewe wapenda bebeo, jaribu kutembea ili usiendelee kuchosha shingo au mgongo. Kama unambeba mtoto wako kwenye mkono, jaribu kubadilisha upande kuliko kutumia upande mmoja mda wote.

Pia fanya mazoezi marahisi yatasaidia kujenga misuli ya mgongoni, itakusaidia kupunguza maumivu ya mgongo na mvutano.

Kama unapata mivuto ya mgongo kutokana na kumbeba mtoto, maji ya moto wakati wakuoga yanasaidia kupunguza maumivu hayo ya misuli. Unaweza jaribu kukabiliana na maumivu ili kupunguza kuvimba kabla ya kwenda kitandani. Kama bado uko na maumivu baada ya siku chache, jihakikishie kwa kumuona mtaalamu wa afya.