Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miezi 3

Jinsi mtoto wako anavyokua

Sasa mtoto wako ana umri wa miezi mitatu, viungio vyake vya mwili vinakua rahisi zaidi, kumruhusu yeye kupungia na kurusha mateke kwa nguvu zaidi. Jitaharishe maana kugeuka geuka kutakua kwingi kwani miguu yake itakua inapata mazoezi ya kutosha. Anaweza akawa mmoja ya watoto waumri huu ambao watafurahishwa na kufunga na kufungua vidole vyake, na kupiga mikono yake pamoja(kupiga makofi)

Ucheshi wa mtoto wa mtoto wako unaendelea kukua vizuri pia. Pindi unapomtekenya,ukicheza nae mchezo wa kujificha au kupuliza kwenye tumbo lake, utamsababishia kucheka sana.

Kwa kweli kucheka kunachukuliwa kama moja ya hatua ya ukuaji wa watoto. Tengeneza mda mwingi wa kuongea na mtoto wako, kumsomea kwa sauti kubwa au kufanya nyuso zenye kumfurahisha.

Maisha yako: Pale milio ya kitoto haikwishi.

Unahisi mwenye wasiwasi au hali ya kuwa na hisia mvhanganyiko ila unazipotezea? Mwenza wako au rafiki yako ameshawahi kukushauri huenda kulia kwa mtoto wako kumekua ni jambo la uzito sana? Sio kitu cha uhakika kwamba unasumbuliwa na tatizo la usongo wa mawazo baada ya ujauzito. Kwa bahati nzuri msaada unapatikana.

Kama unahisi unasumbuliwa na msongo wa mawazo baada ya ujauzito, usiruhusu wasiwasi au kiburi kukuzuia kumwona daktari wako au kuongea na mshauri wako wa afya. Angalau moja kati ya wanamama nane wana uzoefu na msongo huu wa mawazo na kupata matibabu kunaweza kuweka mabadiliko yote.