Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Miezi 9

Jinsi mtoto wako anavyokua

Msikilize kwa umakini mtoto wako anapoongea. Utafanikiwa kugundua anaweza kuzungumza silabi mbili amabazo zinasikika kama neno. Kuelewa kwake kuanaendelea kukua kila wakati pia. Haitachukua muda kabla ya yeye kuanza kuelewa maswali marahisi na maombi. Huu ni mwanzo wa muda wa kufurahisha, pindi ambapo utu wake unaanza kuchomoza kwa uwazi zaidi.

Dunia ya mtoto wako inaanza kufunguka kimwili pia. Anaweza kuchunguza kwa ujasiri zaidi, na kupima vitu anavyoviona na vinavyomzunguka.

Maisha yako: Vitafuno vya afya

Sio rahisi kula milo mitatu bora kila mara kama wewe ni mzazi mwenye kazi nyingi. Ila ni muhimu kupata kitafunio chenye lishe kwa ajili yako na mtoto.

Chaguo la kitafunio kitamu na chenye afya inajumuisha matunda safi, nafaka zenye fati ndogo,mbogamboga mbichi, nafaka imara na mtindi uliopakiwa. Au saga matunda yaliyo safi, maziwa na mtindi pamoja kwaajili ya lishe iliyojumuika na laini. Kama utashindwa kutengeneza mlo wa afya, tafuta vitafunio unaweza kutafuna bila kutumia nguvu nyingi, kama matunda yaliokaushwa na karoti zilizokatwa nyembamba nyembamba. Weka kwenye mifuko ya plastiki ili iwe rahisi kutembea nayo. Hii itakusaidia kuepuka vyakula vyenye fati nyingi, sukari na mara nyingi kuepuka gharama za hapa na pale.

Jaribu kufanya ununuzi wa vyakula ukiwa hauna hasira, kwani hasira inaweza kukusababishia kununua vyakula na vitafunio visivyo na afya.

Kula kwa afya ni mwanzo mzuri, ila kumbuka kufikiria unachokunywa pia. Vinywaji vyenye sukari, ukijumuisha juisi sio vizuri kwa afya. Jaribu kunywa maji kila unapoweza, ongeza vipande vya matunda au tango kubadilisha ladha. Kumbuka kuacha pombe na kahawa, au kuepuka vyote kwa pamoja kama unanyonyesha bado.