Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Mwaka 1 na Miezi 10 – (Miezi 22)

Miezi 22, wiki ya kwanza

Jinsi mtoto anavyokua

Mtoto wako anavyojifunza nini anapenda na nini hapendi, ataanza kuja na maoni yake ya jinsi anavyotaka vitu vifanyike, kwa mfano ataanza kusukuma gari lake badala ya kulibeba mkononi. Tazama tabasamu nono usoni wa mwanao pale atakapofanikiwa kufanya kitu. Atavunjika moyo pale atakaposhindwa kufanikisha jambo.

Ikiwa mwanao anataka kukuonyesha upendo dakika moja na nyingine akaondoka, usiumie sana.katika umri huu mtoto anagundua kuchagua kujumuika na wenzake. Kadiri ulimwengu unaomzunguka unavyokua ndivyo atakavyoanza kujihusisha na wenzake katika michezo zaidi. Anaweza kumuiga kaka yake anavyocheza mpira wa miguu, au anavyowakimbilia wenzake kucheza.

 

Miezi 22, wiki ya pili

Jinsi mtoto anavyokua

Katika umri huu itachukua dakika chache kupata usikivu wa mwanao. Lakini yeye anaweza kutafuta usikivu wako kwa kukukatisha katika maongezi, kuongea kwa sauti kubwa na kurudiarudia jambo.

Mtoto wako anaweza kukutisha katika maongezi yako ya simu na baba yake au mtu muhimu kazini. Jaribu kuwasiliana nao mara mwanao anapolala au akiwa anacheza mwenyewe.

Wakati unaangalia email na kuongea na watu wa muhimu kazini kumbuka kumuangalia mwanao kama anahitaji chochote kama maji au kubadilishwa nepi. Ikiwa anahitaji usikIvu wako bila sababu, usimpatie mara moja. Ukiendelea na shughuli zako atajifunza kutokukatisha katika kazi zako na hatarudia tena.

Lakini kumbuka kufanya maongezi yako mafupi, katika umri huu mtoto wako hawezi kuvumilia dakika 20 za wewe kuongea na simu bila kukukatisha.

 

Miezi 22, wiki ya tatu

Jinsi mtoto anavyokua

Kuwa na msisitizo wa kumpatia mwanao vyakula vipya kulingana na ushauri wa wataalamu wa afya, kawaida mtoto wako katika umri huu ataanza kulalamika pale unapompatia vyakula ambavyo havipendi. Endelea kumpatia mbogamboga na matunda hata asipopenda kula tena.

Mpatie kiwango kidogo cha chakula ili usimuogopeshe mtoto. Kamwe usimlazimishe mwanao kuonja kitu au kuosha sahani yake,kumbuka kila mtu ana kitu anachopenda na asichopenda. Endelea kumpatia aina tofauti ya vyakula ili apate nafasi ya kuchagua nini anapenda na nini hapendi.

Katika umri huu adabu mezani kwa mwanao ni jambo lisilowezekana, mwanao anaweza kunusa na kugusa chakula kipya machoni pake na kuchunguza mfumo wa vyakula tofauti kwa kutumia vidole vyake.
Je,nguo za mwanao zinamvuka? Kama una mpango wa kuwa na mtoto mwingine ni vizuri kuzihifadhi kwenye maboksi au masanduku kwaajili ya baadae.

Miezi 22, wiki ya nne

Jinsi anavyokua

Mwanao anaanza kuonyesha kufurahishwa na uwepo wa midoli na vitu hatari kwa umri wake. Ikiwa una mpango wa kumnunulia mwanao midoli kama zawadi ya siku ya kuzaliwa jaribu kuangalia midoli salama kwa mtoto wa umri wake, ambayo si hatarishi kwa afya yake.

Kila familia ina majina yenye kumaanisha neno “kujisaidia”. Chagua maneno yanayoeleweka kwa wote na rahisi kutumia. Ni wakati mzuri wa kuanzisha tabia nzuri ya kunawa mikono, wakati wa kumfundisha mtoto kujisaidia. Himiza familia nzima kuendeleza usafi mzuri ili kumlinda mtoto na wewe.