Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Mwaka 1 na Miezi 11 – (Miezi 23)

Miezi 23, wiki ya kwanza

Jinsi mwanao anavyokua

Uwezo wa mwanao kuongea unakua kila wakati ndani ya miezi 23 ataweza kuongea sentensi nzima. Unaweza msikia akiimba pia. Kuimarika kwa lugha yake, kutafuatana na kuimarika kwa uelewa wake. Kumbukumbu ya mwanao pia inaimarika.

Vile mwanao anavyojumuika na watoto wenzake ndivyo anapokua hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza na harara kwenye ngozi. Baadhi ya magonjwa ya kuambukiza ni pamoja na tetekuwanga

Japokua mengi ya magonjwa ya kuambukiza ya ngozi sio hatari sana, mengine yanaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa la kitiba kama homa ya uti wa mgongo, zifahamu dalili zake na tiba yake mapema.

Kama una wasiwasi na afya ya mwanao muone daktari mapema kwa ushauri ili kuondoa shaka.

 

Miezi 23, wiki ya pili.

Jinsi mwanao anavyokua

Ukuaji wa mwanao umepungua kwa haraka ukilinganisha na mwaka wake wa kwanza. Wastani wa uzito wa mwanao mwaka wa kwanza unaongezeka mara tatu, lakini mwaka wa pili unaongezeka 1.3 mpaka 2.2kg. Mwanao sasa anasimama na kutembea mwili wake unahusika kwenye mihangaiko mingi na kusababisha kupungua, kadiri mafuta yanavyopungua mwilini mwake.

Katika umri wa miaka miwili, watoto wengi wanaweza kuvuta midoli yao nyuma yao na kubeba vitu wakiwa wanatembea na wataanza kukimbia pia. Hii ni kwasababu ya kuimarika kwa mfumo wake wa kusogea na kupiga hatua.

 

Miezi 23, wiki ya tatu

Jinsi mtoto anavyokua

Ni wakati mzuri wa kufikiria usalama wa mwanao. Kwa sasa ni mrefu, anazunguka sana na amekua na uthubutu zaidi, ni vizuri kuweka nyumba yako katika usalama zaidi. Sasa anaweza kupanda juu ya meza,kabati na kufungua milango ya makabati na vyumba ambavyo hajawahi kuvitilia maanani, pia amekua na kasi zaidi unavyofikiria.

Habari njema ni kwamba mwanao anaelewa maana ya neno HAPANA mara unapomuambia. Wakati alivyokua mdogo ulizingatia kutoa vitu hatari karibu na uwepo wake, endelea kufanya hivyo hivyo. Lakini sasa unaweza kumsisitiza zaidi kwa maneno, kwa kumkanya na kumuelezea asishike kitu filani.

Bado unahitaji kuwa makini, ondoa vitu vyote hatari, mfano ondoa visu vikali kwenye kabati analofikia na hifadhi dawa na virutubisho mbali naye.

 

Miezi 23, wiki ya nne

Jinsi mtoto anavyokua

Sasa ni wakati muafaka wa kumnunulia mwanao baiskeli kama mwanao anaonyesha ukakamavu hasa katika michezo, mwanao akiendesha baiskeli ni wakati mzuri kukumbusha kiasi gani mwanao kakua.