Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Mwaka 1 na Miezi 9 – (Miezi 21)

Miezi 21, wiki ya kwanza

Jinsi mtoto anavyokua

Sasa mtoto wako ana miezi 21, atajumuika kukusaidia kufanya kazi za ndani kama kuosha vyombo na wakati mwingine kuiga unachokifanya. Ataweza kuvaa nguo, kunawa na kukausha mikono yake au kupiga mswaki kwa msaada wako kidogo.

Anakaribia kuweza kujisaidia mwenyewe.  Muda mchache kabla hajatimiza miaka miwili utaanza kuona dalili kama anataka kujisaidia. Anaweza chuchuma au kujificha sehemu tulivu. Ingawa anaelewa kinachoendela anaweza asiwe tayari kutumia choo chake sasa,ila anakaribia kufanikisha jambo hili.

Ikiwa hujaanzisha utaratibu maalumu wa kulala mchana,kula na kwenda kitandani usiku,msaidie mwanao kuhakikisha na kuwa na uwezo wa kujiongoza katika ratiba yake. Utaratibu huu unakusaidia kufanya maisha kuwa marahisi, kama mwanao anajua cha kutarajia wakati fulani kila siku atakua mwenye furaha na tayari kufuata utaratibu huo.

Miezi 21, wiki ya pili.

Jinsi mtoto anavyokua

Kushirikiana inaweza lisiwe jambo kuu kwa mwanao. Usitegemee mwanao kufuzu ujuzi wa kushirikiana mpaka atakapokua mkubwa. Kwanza ameanza kujifunza kumiliki kitu na muda utakaporuhusu ataanza kushirikiana na wenzake. Kwasababu bado mdogo na hajui kama akishirikiana na mwenzie mdoli ataupata tena baadae, inakua ngumu kwa yeye kukubali kushirikiana.

Mpongeze pale anapokubali kumpatia mwenzake mdoli wake. Unaweza kukuza uwezo wake wa kushirikiana na wenzake kwa kumuomba kitu chochote anachochezea na kumrudishia tena baada ya dakika chache. Hii itamsaidia mtoto kujua wazo la kupokea na kuchukua.

Katika michezo ya pamoja inaweza kuleta ugomvi katika swala zima la kushirikiana midoli, ni vizuri kuweka midoli inayofanana kwa wingi wakati wa kucheza. Lakini pia mwanao atakapomnyang’anya mwenzie mdoli mkanye mara moja na kumueleza sio tabia nzuri, unaweza kumkanya kwa  lugha ya upole zaidi.

 

Miezi 21, wiki ya tatu.

Jinsi mtoto anavyokua

Inaweza kuchosha pale mwanao atakapo weka sura za kijinga, kupiga kelele zinazosababishwa na kukasirishwa na jambo au kuvunjika moyo, anapogonga meza au ngoma. Yote haya yanamsaidia kuendeleza uchunguzi utakao msaidia kujifunza na kukua.

Kwa sasa mwanao ataweza kujaza chakula kwenye kijiko chake na kula mwenyewe na kunywa kitu kwenye kikombe chake. Kumbuka kumsifia sana pale anapopatia kufanya kitu mkiwa mezani wakati wa chakula, uwezo na ujasiri wake utaanza kukua pia.

Kwa sasa mwanao atavutiwa na simu yako, ikiwa ni kuangalia picha, kucheza game au kuongea na bibi yake. Simu za kiganjani ni moja ya maisha yetu ya kila siku hakikisha unamsimamia mwanao katika matumizi ya simu.

Miezi 2, wiki ya nne

Jinsi mtoto anavyokua

Watoto wengi katika umri huu wanapenda kula,lakini wengine wanachagua vyakula sana. Wengine wanapendelea kula vyakula vyeupe tu kama tambi, mkate na maziwa. Wengine wanapendelea kula chakula aina moja tu, mfano wali bila mboga. Kama ilivyo kawaida ya watoto wengi wa umri huu kuchukia mboga za majani hasa mboga zenye uchungu na nyinginezo zenye ladha ngumu, na mwanao nae ataanza kuchukia pia.

Usimlalamike mwanao juu ya tabia yake. Badala yake endelea kuandaa chakula cha familia chenye ubora na mruhusu achague anachokipenda. Utashangazwa kugundua watoto wadogo hawaitaji chakula kingi kuwa na afya, ila kidogo na bora.

Wakati mwingine mruhusu mwanao kufanya jambo ambalo daima unamkataza, jambo hilo lisiwe na madhara. Kufanya hivi kutakusaidia yeye kukuamini na kufuata kile utakachomkataza hapo baadae.