Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Wiki ya 1

Jinsi mtoto wako anavyokua

Hongera kwa kuwasili kwa mshiriki mpya kwenye familia yako! Maisha na mtoto mpya yanaweza kuwa ya kuchosha na kufurahisha vile vile, na itachukua muda kujirudi katika hali yake ya kawaida. Kichanga chako kitahitaji mapenzi sana na kukumbatiwa mpaka aanze kuzoea maisha nje tumbo la uzazi.

Baada ya kuishi tumboni kwa miezi tisa, nafasi anayoipata nje ya mji wa mimba bado inamshangaza. Unaweza kuona kuwa anasogea kwa kushtuka shtuka kusiko na mpangilio kadiri anavyozoea na kufurahia nafasi nje ya mji wa mimba.Je, mtoto wako anaonekana kama pua zimeziba wakati amelala? Kama utamuangalia, utagundua anapumua katika mzunguko. Inaweza ikawa kwa haraka haraka na yenye kuvuta pumzi ndefu ndani ikifuatiwa na kupumua polepole na kuvuja pumzi juu juu. Unaweza pia kusikia kukoroma au kubanwa pumzi, na wakati mwingine unaweza kuona mtoto wako anaacha kupumua kwa sekunde hadi tano na kuanza kupumua tena.

Hii ni kawaida kabisa, na sio dalili kwamba mtoto wako ana mafua. Lakini kama utakuwa na wasiwasi wowote kuhusu upumuaji wa mtoto wako – au kitu kingine chochote usisite kupata kumuona daktari.

Maisha yako: Kuanza kuzoea kumlisha mtoto wako

Kama unamnyonyesha mtoto wako, inawezekana bado haujazoea swala hili. Ila itakuwa rahisi kadiri muda unavyoenda kwa hiyo kuwa mvumilivu. Kama unajisikia kukata tamaa jaribu kukumbuka faida zote za kunyonyesha kwa afya ya mtoto wako, ili kupata motisha.

Wamama wengi waliojifungua kwa mara ya kwanza huwa na wasiwasi kama maziwa anayopata mtoto yanatosha, sana sana kama mtoto anaonekana mwenye njaa muda wote au analia kila ukimuondoa kwenye chuchu. Soma ushauri kutoka kwa wataalamu wetu jinsi gani ya kutambua kama mtoto wako anapata maziwa ya kutosha.Ni lazima uwe na maswali mengi kuhusu kunyonyesha mtoto. Inakuwaga vigumu sana kwa wale ambao wamefanyiwa upasuaji na ushauriwa jinsi gani ya kumshika na kumnyonyesha mtoto vizuri.

Kumbuka unaweza kupata ushauri wa papo kwa papo kutoka kwa mkunga/daktari wako.Kama unanyonyesha kupitia chupa ni lazima utakuwa na maswali pia. Unaweza jiuliza mchanganyiko upi ni bora kwa mtoto wako au kiasi gani cha mchanganyiko anachotakiwa kupewa mtoto. kwa ushauri zaidi ongea na mkunga/daktari wako.

Kama unapata msongo wa mawazo kutokana na maisha mapya na mtoto wako, hiyo ni kawaida. Wamama wengi hupata sana shida wiki ya kwanza baada ya kujifungua mtoto kiasi cha kumfanya mama achoke na kuwa mpweke. Hii hutokana na mabadiliko ya homoni ambayo hutokea kwa masaa au siku chache. Ingawa ni kawaida, unaweza pata ushauri kutoka kwa mkunga/daktari wako kama hali hiyo itazidi.