Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Wiki ya 4

Jinsi mtoto anavyokua

Mtoto wako anaendelea kuwa mwenye nguvu kila siku na kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu unaomzunguka. Hawezi kuona mbali, ila anaweza kutambua pindi ukipeleka uso wako karibu yake. Kusikia kwake kwasasa kumeimarika vizuri, japo katika hali ya asili itamchukua mda kuelewa kelele zote katika ulimwengu wake.

Moja ya mabadiliko yakufurahisha kwa mtoto wako ni kwamba anaweza kuanza kuongea. Anaweza kunong’ona, kutoa sauti kali pindi anapolia, kutoa sauti za kitoto au kutoa sauti kwa kugusanisha midomo yake, akijaribu kuelezea hisia zake. Jaribu kunong’ona na kutoa sauti za kitoto pia. Mpakate karibu na wewe na ongea nae uso kwa uso ili aweze kuona jinsi uso wako unavyojielezea. Japokuwa hawezi kuona mbali, ila atapendezwa kusikia sauti yako ni vyema kuendelea kuongea nae pindi umwekapo chini na kuondoka.

Maisha yako: Hisia mchanganyiko

Kwa wamama wapya, yaweza onekana kama vimilio vya watoto wao havitaisha. Kama huwezi lala (na sio kwa sababu mtoto anakuamsha) unakula sana au pungufu au kujisikia hali ya chini au kujisikia mwenye shauku kila wakati, unaweza ukawa unakumbwa na usongo wa mawazo baada ya ujauzito. Hivyo basi hauko mwenyewe, maana katika wanawake nane mmoja kati yao anakumbwa na hili tatizo.

Bado unahisi maumivu ukiwa unaketi? Kama ulichanika vibaya kipindi cha kujifungua, pengine una shahuku ya kujua ni kwa mda gani hayo madhara yatadumu. Kama una maumivu kwenye via vya uzazi yanaotokana na kuchanika au kufanyiwa upasuaji mdogo kipindi cha kujifungua, usisubirie mpaka vipimo baada ya ujauzito. Mtafute daktari mara moja na kugundua nini kifanyike ili kujiweka katika hali ya kuridhika.

Kama una wasiwasi kuhusu jinsi yakurudisha uzito wako wa mwili katika hali ya mwanzo, pumzika kwa amani kwani bado ni mapema kuanza kufanya mazoezi. Mazoezi ya mpangilio ya sakafu ya nyonga kwa sasa yanatosha.

Njia pekee ya kurudia mwili wako wa kawaida ni kuenda taratibu. Maana ilikuchukua miezi tisa mtoto wako kukua, hivyo jiruhusu mda ule ule kurudisha mwili wako kama awali.