Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Wiki ya 5

Jinsi mtoto wako anavyokua

Mtoto wako kwa sasa anaweza kutazama kitu kwa macho yake yote, kwa hiyo anaona ulimwengu kwa kina zaidi kuliko hapo awali. Unaweza gundua kwamba ameanza kupendelea miundo, rangi na maumbo yenye utata. Anaweza kufuatilia mwendo pia, kwa hiyo anaweza kuduwaa kwa kitu kirahisi kilichopita mbele ya uso wake. Ila muda kitakapo potea kwenye uwepo wake anasahau kama kilishawahi kuwepo.

Miezi mitatu ya mwanzo ni muhimu kwenye ukuaji wa ubongo wa mtoto. Ingawa mtoto wako atasahau vitu vipya mapema, kumbukumbu yake inakua kila wakati. Ameanza kuifahamu sauti yako tangu alipozaliwa. Inawezekana pia anakugundua harufu yako, na kuona yenye kuridhisha.

Je uko tayari kutoka nje pamoja na mtoto wako? Inaweza ikawa vigumu kujitaharisha kutoka nje ya nyumba hasa ukiwa na mtoto mdogo. Ila kubadilisha mazingira ni njia kuu ya kumtambulisha mtoto katika mambo mampya, na inaweza kukuza hali/hisia yako. Hata matembezi madogo kwenye maduka yanaweza kukusaidia kupata mapumziko ya siku.

Maisha yako: ushindani wa ndugu

Kama una watoto wengine, unaweza kugundua furaha ya kuwepo kwa mdogo mpya wa kike au kiume inapotea. Mtoto wako mkubwa anaweza kuona wivu na kutaka uangalifu wakati wa kumnyonyesha mtoto, au hata kukutaka umrudishe mtoto.

Jitahidi kuhakikisha mtoto wako mkubwa anapata mda mrefu wa pekee na wewe au mume wako. Mnaweza kuchukua kila mmoja mda kumwangalia mtoto na mzazi mwingine kutumia muda na watoto wakubwa wa kiume au kike. Kama wewe ni mzazi pekee unaweza omba msaada kwa marafiki na familia, au kutafuta mdada wa kazi.

Kama mtoto wako mkubwa anageza vitu vya kitoto unaweza ukamshirikisha kwa muda. Ni jambo la kawaida kwa watoto wakubwa kudeka na kutaka kuangaliwa zaidi pindi anapokuja mtoto mwingine. Hapo punde mtoto wako mkubwa atajirudia hali yake ya kawaida akapogundua kujidekeza kutamnyima kufurahia na kujifunza vitu vipya.