Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

“Drone” kuanza kusambaza damu vijijini Tanzania. 

Zipline kuanza kufanya shughuli za kusafirisha damu kwa kutumia “drone” nchini Tanzania. 

Kampuni ya kutengeneza”robots” ya California nchini Marekani – Zipline imetangaza rasmi nia yake ya kuanza shughuli za kusambaza damu vijijini nchini Tanzania kwa kutumia drones. Kampuni hii ilianza kutoa huduma kama hii nchini Rwanda mnamo mwaka jana na kuwa kampuni ya kwanza duniani kusafirisha damu na vifaa-tiba mbalimbali kutoka hospitali kubwa mijini na kuzipeleka vijijini kwa njia ya ndege ndogo zisizo na dereva “drone”.

CEO wa Zipline alisema kuwa kupelekea mafanikio yaliyoonekana huko Rwanda, kampuni yake ikishirikiana na wizara ya afya na MSD wanategemea kujiunga na mashirika mengine matatu, Human Development Impact Fund, Bill and Melinda Gates Foundation na Saving Lives at Birth Foundation kuweza kukamilisha mradi huu unaotegemea kuanzisha vituo vinne vya kurushia “drone” hizi ndani ya miaka minne ijayo.

Tanzania itakuwa ni nchi ya pili sio Afrika tuu bali duniani kote kuwa na huduma hii ya kusafirisha damu, madawa na vifaa tiba muhimu kwa kutumia teknolojia ya “drones”.

Kampuni ya Zipline hutengeneza drone zake yenyewe na huwa na uwezo wa kusafiri hadi kilometa 150 kwa chaji moja. Drone hizi zina uwezo wa kubeba hadi kilo moja na nusu ya mzigo.

Teknolojia hii ambayo inategemea kuanza mapema mwakani itasaidia huduma za damu na dawa muhimu kufika maeneo ambayo usafiri ni wa shida na ngumu kufikika. Sehemu ambayo gari lingetumia masaa manne inaweza kufikiwa kwa drone ndani ya nusu saa. Hivyo kuokoa muda, gharama na maisha ya wagonjwa.

Imepitiwa: August 2017

Leave a Comment

(33 Comments)