Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Kupevuka kwa yai – Ovulation

Ovulation (Kupevuka kwa yai)

Fahamu Ovulation (kupevuka kwa yai ni nini), na namna ya kutambua siku zinazohusika nayo.

Ovulation ni nini?

Ovulation (kupevuka kwa yai) ni pale yai moja au zaidi yanaachiwa kutoka kwenye moja ya ovari(mifuko ya mayai) yako. Hii hutokea karibia na mwishoni mwa muda ambao una uwezo wa kupata mimba katikati ya mzunguko wako wa hedhi.
Kila mwezi, kati ya mayai 15 hadi 20 yanakua ndani ya ovari zako. Yai lililokua zaidi hutolewa na kusukumwa kwenye mirija yako ya uzazi (fallopian tubes) inayounganisha ovari zako na tumbo lako la uzazi. Mifuko yako ya uzazi sio kwamba inapokezana kutoa yai kila mwezi. Hili hutokea bila mpangilio maalumu.

Lini nipo kwenye uwezo wa kupata mimba?

Ili kupata ujauzito kwa njia ya kawaida, moja ya yai na mbegu kutoka kwa mwenza wako lazima vikutane kwenye mirija yako ya uzazi. Yai lako haliwezi kuwa hai kwa zaidi ya saa 24 baada ya kuwa kwenye ovulation. Kwa hiyo kukutana kwa yai na mbegu lazima kutokee ndani ya muda huu.
Kwa upande mwingine, mbegu za mwanaume huweza kuwa hai hadi kufikia siku saba. Wataishi kwa raha tuu kwenye uke, mfuko wa mimba, au kwenye mirija ya uzazi kwa muda wote huu.
Hii inamaanisha, sio lazima uhesabu muda sahihi kabisa ukiwa unaovuleti kuweza kupata ujauzito. Ki uhalisia una jumla ya siku sita kwenye mzunguko wako ambazo unaweza ukashika mimba. Kwa hiyo kama ukifanya ngono katika kipindi hiki, yai lako lililopevuka tayari linaweza likakutana na mbegu yenye afya na kuchavushwa.

Ni wakati gani Ovulation inatokea?

Ovulation mara nyingi hutokea kati ya siku 12 hadi 14 kabla ya hedhi kuanza. Hii ni wastani tu wa makadirio, hivyo inaweza ikawa ni siku chache kabla au baada.

Kwa mfano, tuseme una mzunguko wa kawaida wa hedhi wa siku 28. Hesabu siku ya kwanza ya kuona hedhi yako kama siku ya kwanza. Siku za wewe kuweza kupata mimba ni kati ya siku ya 10 hadi ya 15.

Vilevile, wanawake wengi wana mizunguko inayotofautiana. Ovulation inaweza kutokea wiki moja kabla au baada kutoka mwezi mmoja hadi mwingine.

Zipi ni dalili za Ovulation?

Utaanza kuziona dalili za kuwa kwenye ovulation karibu siku tano kabla ya kuovulate. Kujaribu kuelewa mzunguko wako kwa kutumia tarehe za mzunguko wako pekee haitakupa majibu sahihi. Hii ndio maana kuwa na uwezo wa kugundua dalili za mwili wako kipindi upo kwenye ovulation na una uwezo wa kupata ujauzito ni muhimu.
Dalili kuu na viashiria vya ovulation vinajumuisha:

• Mabadiliko ya ute kwenye mlango wa uzazi
• Kuongezeka joto la mwili
• Maumivu ya tumbo
• Maumivu ya maziwa yanapoguswa
• Kuwa na hamu ya mapenzi kuliko kawaida

Mabadiliko ya ute kwenye mlango wa uzazi
Ute wa mlango wa uzazi ni ute ute unauouna kwenye chupi au kwennye “toilet paper” unapokwenda kukojoa.
Mabadiliko ya ute wa mlango wa uzazi ni alama ya kuwa upo kwenye dirisha la kuweza kupata mimba. Baada ya hedhi kuisha ute wa mlango wako wa kizazi huongezeka kwa ujazo na hubadilika pia hali yake.

Mabadiliko haya yanaendana na kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya “Oestrogen” kwenye mwili wako. Pia inaonesha umekaribia kuovulate.

Utakuwa zaidi kwenye uwezo wa kupata mimba kama ute ute ule unakuwa kama hauna rangi (clear), unateleza sana na unavutika. Utafanana kama sehemu nyeupe ya yai ukilivunja. Huu ute ute huzisaidia mbegu kuwa na spidi zaidi wakati zinaogelea kuelekea kwenye mfuko wako wa kizazi. Huilisha na kuilinda mbegu inapokuwa inasafiri kuelekea kwenye mirija yako ya uzazi (fallopian tubes) kukutana na yai lako.

Angalia mkusanyo wa picha zetu kutambua Jinsi ute wa mlano wa kizazi unavyoonekana.

Maumivu ya tumbo
Mwanamke mmoja kati ya watano huwa anasikia kitu kinaendelea kwenye mifuko yao ya mayai (ovaries) wakati wa kipindi cha ovulation. Hii inaweza ikatokea kama maumivu madogo madogo au maumivu yanayovuta na kuachia.
Kama ukizihisi dalili hizi katika kipindi kilekile kila mwezi, angalia ute ute wa mlango wako wa kizazi. Maumivu ya kipindi cha ovulation yanaweza yakawa ni njia ya kukuwezesha kutambua kuwa una uwezo wa kupata ujauzito.

Hisia za mapenzi
Hisia za mapenzi, kuwa muongeaji zaidi au kujitongozesha zinaweza kuwa ni dalili pia kuwa upo kwenye ovulation.
Unaweza ukaona hamu yako ya ngono ipo juu kabisa kipindi hiki. Unaweza ukatambua kwamba mwenza wako anakuwa karibu zaidi na matokeo yake anakupa umakini zaidi. Hili lina ushahidi wa kidaktari!
Unaweza usitambue, ila unaweza ukawa unaonesha dalili nyingine ukiwa kwenye siku za kuweza kupata mimba. Kumbuka mizunguko yako ya hedhi ya nyuma na unaweza ukakumbuka yafuatayo kutokea:

• Kuonekana na kujisikia vizuri: una uwezekano wa kujihisi una mvuto zaidi kimuonekano kadiri unavyokaribia ovulation. Unaweza ukawa unavutiwa na wengine zaidi pia katika kipindi hiki. Bila kutambua kwa mfano unaweza ukajikuta umechagua nguo zinazokuvutia na kuvutia wengine zaidi kimapenzi kwenye kipindi hiki.
• Manukato ya mwanamke: unanukia vizuri katika kipindi hiki. Harufu ya mwili wako ni nzuri na inavutia kimapenzi wanaume katika kipindi hiki. Unaweza ukahisi hakuna mtu yoyote anatambua upo kwenye ovulation, lakini harufu hizi zinaweza zikatoa siri.

Nitawezaje kuongeza uwezo wangu wa kupata mimba?

Jaribu kufanya ngono kila baada ya siku mbili au tatu. Mbegu zenye uogeleaji mzuri zitakuwa sehemu husika siku yoyote ukiwa kwenye ovulation. Ngono ya mara kwa mara kwenye mzunguko wako wote inakupa uwezo mkubwa wa kushika ujauzito.

Kufanya ngono wakati mlango wa kizazi chako una ute, unateleza na upo kwenye hali ya kuzipokea mbegu itaongeza uwezo wako wa kupata ujauzito. Kwa wapenzi wenye uzazi salama, wana uwezo kati ya asilimia 20 hadi 25 wa kupata ujauzito kwa kila mzunguko wa hedhi.

Zaidi ya asilimia 80 ya wanawake chini ya miaka 40 ambao hufanya ngono kwa kawaida bila kutumia uzazi wa mpango hupata mimba kila mwaka. Zaidi ya asilimia 90 ya wenza wapya hupata ujauzito ndani ya miaka miwili.

Imepitiwa: Aprili 2017.

Leave a Comment

(429 Comments)

shares