Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Asidi ya foliki kipindi cha ujauzito

Umuhimu wa asidi ya foliki kipindi cha ujauzito

Asidi ya foliki ni shujaa katika mimba! Kumeza vitamin kabla ya kupata ujauzito kwa kiwango kinachokubalika cha mikrogramu 400mcg kabla na wakati wa ujauzito huweza kusaidia matatizo ya kuzaliwa nayo kwenye ubongo na uti wa mgongo wa mtoto wako. Ni vyema kumeza kidonge cha aside ya foliki kila siku kama unategemea au wewe ni mjamzito tayari.

Asidi ya foliki (Folic acid) ni nini?

Asidi ya foliki ni aina ya vitamini B inayoitwa “folate” inayotengenezwa na mwanadamu maabara. “Folate” inafanya kazi muhimu kwenye utengenezaji wa chembe damu nyekundu na ndio husaidia utupu wenye taarifa za kiumbe (neural tube) kuweza kukua na kuwa ubongo na uti wa mgongo. Chakula bora chenye wingi wa aside ya foliki ni “fortified cereals”. “Folate” hupatikana zaidi kwenye mbogamboga zenye rangi kijani iliyokolea na matunda jamii ya chungwa.

Ni lini uanze kutumia asidi ya foliki?

Matatizo ya kuzaliwa nayo huanza kutokea ndani ya wiki ya 3-4 ya ujauzito. Hivyo ni muhimu kuwa na “folate” tayari kwenye mzunguko wa mwili wako kwenye kipindi hiki muhimu cha mwanzoni ambapo ndio ubongo na uti wa mgongo wa mtoto wako unajijenga.
Kama ulizungumza na daktari wako kipindi ulichokuwa unataka kupata ujauzito, inawezekana alishakushauri tayari kuanza kutumia vitamini na asidi ya foliki. Tafiti moja ilionesha wanawake waliotumia asidi ya foliki kwa kuanzia mwaka kabla ya kupata ujauzito walipunguza uwezekano wa kujifungua mapema kabla ya muda kwa asilimia 50 au zaidi.

Shirika la kuzuia magonjwa la Marekani (CDC) linashauri uanze kutumia asidi ya foliki kila siku kwa kiwango cha chini ndani ya mwezi kabla ya kuwa mjamzito, na kila siku wakati wa ujauzito wako. Vilevile shirika hili linashauri wanawake wote walio kwenye umri wa kuweza kuwa wajawazito kutumia asidi ya foliki kila siku. Hivyo hata ukiamua kuanza kutumia asidi ya foliki mapema zaidi ni vyema zaidi.

Kama utaamua kununua nyongeza ya vitamini wewe mwenyewe, ni vyema ukazungumza pia na daktari wako baada ya kupata ujauzito ili kuwa na uhakika kuwa nyongeza hiyo ya vitamini ina mjumuisho wa kila kitu unachotakiwa ukipate kwa ujauzito wako ikiwemo asidi ya foliki.

Kiasi gani cha asidi ya foliki nitumie?

Dozi inayoelekezwa kwa wanawake wote waliopo kwenye umri wa kuweza kupata ujauzito ni mikrogramu 400 au 400mcg za “folate” kila siku. Kama unatumia nyongeza ya mjumuisho wa vitamini zote, angalia kama ina kiwango kilichoelekezwa. Kama kwa sababu Fulani usingependelea kutumia asidi ya foliki ikiwa kwenye mjumuisho wa nyongeza za vitamini unaweza ukatumia nyongeza ya asidi ya foliki pekee.

Huu ndio mchanganuo wa kiasi cha asidi ya foliki kinachoelekezwa kwa wanawake wajawazito kwa siku:
• Ukiwa unataka kupata ujauzito – 400mcg
• Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito – 400mcg
• Kuanzia mwezi wa 4 hadi wa 9 wa ujauzito – 600mcg
• Ukiwa unanyonyesha – 500mcg

Asidi ya foliki ina faida gani?

Bila kuwa na asidi ya foliki ya kutosha, utupu wa taarifa (neural tube) ya mtoto wako haitakua vyema na itasababisha magonjwa yanayohusiana na utupu wa taarifa (neural tube defects).
Magonjwa haya ni kama:
Spina bifida: Kutokukamilika ukuaji wa uti wa mgongo au pingili za uti wa mgongo.
Anencephaly: Kutokukamilika kwa ukuaji wa sehemu kubwa ya ubongo.

Watoto wenye “Anencephaly” mara nyingi hawaishi muda mrefu na wale wenye “spina bifida” huwa na ulemavu maisha yao yote. Habari njema ni kwamba kutumia nyongeza ya asidi ya foliki kipindi cha ujauzito inaweza kumuepusha mtoto wako kupata magonjwa haya kwa zaidi ya asilimia 50.

Kama utatumua kabla na wakati wa ujauzito, asidi ya foliki pia inaweza kumkinga mtoto wako dhidi ya:
• Mdomo sungura
• Kuzaliwa kabla ya muda (Njiti)
• Kuzaliwa na uzito mdogo
• Mimba kutoka
• Ukuaji dhaifu tumboni

Asidi ya foliki pia inahusishwa na kupunguza hatari ya kupata:
• Matatizo kwenye ujauzito
• Magonjwa ya moyo
• Kiharusi
• Aina baadhi ya saratani
• Ugonjwa wa Alzheimer

Imepitiwa: July 2017

Leave a Comment

(32 Comments)

shares