Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Je, unaweza kuchagua jinsia ya mtoto?

Kwa muda mrefu tukiwa tunazaa watoto, wanawake wamekuwa wakichangia mawazo jinsi ya kuongeza nafasi za kuzaa mtoto wa kike au kiume. Kwa bahati mbaya hakuna ushahidi wa matibabu kwamba yeyote kati hayo inaweza kufanya kazi!

Baada ya kusema hivyo, daima kutakuwa na mwanamama ambaye atakuambia hadithi za wazee ambayo alitumia. Kwa hiyo ikiwa unafikiria kujaribu kupata mtoto mwenye jinsia unayoitaka, kwa nini usijaribu baadhi ya mapendekezo hapa chini;

Uwezekano zaidi wa kumzaa mvulana kama:

 • Ukikutana kimwili na mwenza wako siku ya kupevuka kwa yai, kama inavofikirika manii kuogelea kwa kasi na kufikia yai kwanza.
 • Ukifika kileleni kabla ya mpenzi wako, hali hii inafungua kimiminika cha bezi kinachodhaniwa kua rafiki wa mbegu ya kiume zaidi kuliko asidi iliyopo kwenye uke.
 • Uume kupenya sana wakati wa tendo, kama vile kwa nyuma (doggy style).
 • Mpenzi wako ana idadi kubwa ya manii. Hii ni kwa sababu manii zinazo kubeba mbegu ya kiume hazina nguvu kama mbegu ya kike, na hivyo nafasi zaidi ya manii ya mbegu ya kiume kufikia yai kwanza inategemea wingi wa manii.
 • Epuka kujamiiana wiki moja kabla ya upevushwaji wa yai na kisha kufanya tendo mara moja kwenye siku ya upevushwaji, ili idadi ya manii iwe ya kutosha.
 • Mpenzi wako akipendekeza kufanya tendo la ndoa.
 • Kufanya tendo la ndoa wakati wa usiku.
 • Kujamiina siku isiyo ya kawaida ya mwezi.
 • Mpenzi wako ajiachie kwa kuweka sehemu zake za siri katika hali ya ubaridi kwa kuvaa boksa na suruali za kutosha kupitisha hewa.
 • Unakula vyakula vya chumvi, nyama nyingi, samaki, unga mweupe, pasta, matunda, mboga fulani, lakini kuepuka maziwa na bidhaa za maziwa, kama vile mtindi na jibini, karanga, chokoleti, samaki na mkate wote.

Uwezekano zaidi wa kumzaa msichana kama:

 • Kujamiiana mapema katika mzunguko wako, siku chache kabla ya siku yako ya kupevushwa yai. Hii ni kwa sababu manii ya kike yanadhaniwa kuwa imara na kwa hiyo hudumu zaidi kuliko mbegu ya kiume, ambaye itakufa kabla ya kufikia yai.
 • Mpenzi wako akifikia kileleni kabla yako.
 • Kujaamiana mara kwa mara ili kupunguza kiwango cha mbegu ya mpenzi wako, na hivyo kuongeza uwezekano wa mbegu ya kike kufikia yai kwanza.
 • Mwenza wako ahakikishe asipenye kwa kina sana [shallow penetration].
 • Kujaamiana pasipo kinga kwa siku nne hadi tano kabla ya upevushwaji wa yai, ili kupunguza nafasi ya manii ya kiume kufikia yai kwanza.
 • Mpenzi wako azidi kua na joto la kawaida katika sehemu zake za siri kwa kuvaa chupi na nguo nyepesi zinazomuachia mwili wake.
 • Pendekeza kufanya tendo la ndoa.
 • Pendekeza kufanya tendo la ndoa wakati wa mchana.
 • Pendekeza kujaamiana hata siku za kawaida za mwezi.
 • Kuna dhana ya kua unaweka kijiko cha mbao chini ya kitanda chako na uzi mwekundu chini ya mto wako.

Zingatia kunywa maziwa mengi na kula bidhaa za maziwa kama vile jibini na mtindi, vyakula visivyo na chumvi, mchele, pasta, baadhi ya mboga, maji ya madini, kiasi kidogo cha nyama na viazi, lakini epuka chumvi na vyakula vingine vya chumvi, divai na bia, matunda , mchicha, nyanya na uyoga, chokoleti, kahawa na chai.