Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Athari za Kiafya kwa Mjamzito Mwenye Uzito Uliopitiliza

Kuwa na uzito uliozidi au unene wa kupitiliza wakati wa ujauzito inaongeza hatari ya matatizo wakati wa ujauzito. Matatizo hayo hujumuisha:

  • Shinikizo la damu wakati wa ujauzito, ambayo bila kuangaliwa kwa karibu inaweza kusababisha matatizo makubwa yajulikanayo kama kifafa cha mimba.
  • Kisukari wakati wa ujauzito uzito uliozidi au unene wa kupitiliza unaweza kusababisha aina hii ya kisukari (type2 diabetes). Wanawake ambao wameshapata aina hii ya kisukari pia wanahatari kubwa ya kupata unene wa kupitiliza maishani. Kisukari wakati wa ujauzito inaweza kusababisha kushuka kwa kiwango cha sukari kwa kichanga. Mtoto ambae hajazaliwa pia anaweza kuwa mkubwa na inaweza kumwathiri mama na mtoto pia,
  • Kuongezeka kwa hatari ya kupasuliwa wakati wa kujifungua.

 Athari za unene uliopitiliza wakati wa ujauzito kwa mtoto

Watoto waliozaliwa na wamama wenye uzito uliozidi au unene wa kupitiliza wapo katika tatizo kubwa la kiafya kama:

  • Kasoro katika neva za fahamu-spina bifida.
  • Matatizo ya moyo
  • Kushuka kwa sukari.
  • Unene wa kupitiliza na kuongezeka kwa mafuta mwilini.

Uzito duni wakati wa ujauzito una athari kwa mtoto anayezaliwa, na athari hizo ni kama:

  • Mtoto kuzaliwa njiti mtoto kuzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito.
  • Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo chini ya kilo 2.5. watoto hawa wachanga wapo katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya .