Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ugonjwa wa Listeria kwa Mjamzito

Listeria ni ugonjwa unaosababishwa pale unapogusa bakteria aitwaye listeria. Pia unaweza kuupata ugonjwa huu pale unapokula chakula kilichoambukizwa listeria, na pia kuupata kwa kushika udongo, maji na kinyesi kilichoambukizwa.

Unapokuwa mjamzito,una kubwa nafasi ya kushambuliwa na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu mabadiliko katika mfumo wako wa kinga hayawezi kuulinda mwili wako dhidi ya maambukizo kama kawaida, kwasababu yako chini kuliko kawaida. Ugonjwa huu wa listeria unaweza kumuathiri mama mjamzito mara 20 zaidi kuliko watu wengine wenye afya.

Ugonjwa wa listeria unaweza kumdhuru mtoto wangu?

Ugonjwa wa listeria ni hatari sana kwa mtoto. Maambukizi yanaweza kumpata mtoto kwa njia ya mfuko wa mimba au wakati wa kujifungua.

Ukigundua una ugonjwa huu mapema na kutibiwa mapema kwa kutumia antibaiotiki itasaidia kumlinda mtoto. Hata hivyo, bila matibabu ya haraka ugonjwa wa listeria unaweza kusababisha:

 • Kuharibika mimba.
 • Kujifungua kabla ya wakati.
 • Kujifungua mtoto aliyefariki.

Ikiwa mtoto wako amepata maambukizi ya ugonjwa huu akiwa bado tumboni au wakati wa kujifungua, anaweza kuumwa sana baada ya kuzaliwa,na kushambuliwa na nimonia, homa ya uti wa mgongo au mtoto kushindwa kupumua vizuri(neonatal sepsis). Kawaida maambukizi kwa mtoto yanaonekana mara mtoto anapozaliwa, ila wakati mwingine dalili zinachukua wiki kadhaa kuonekana.

Nitajuaje nina ugonjwa wa listeria?

Ni rahisi sana kufananisha ugonjwa wa listeria na mafua kwasababu dalili ni ndogo sana- ni za hali ya chini kuzigundua. Unaweza kuwa na:

 • Homa
 • Maumivu ya misuli
 • Kusikia baridi
 • Kichefuchefu au kutapika
 • Kuharisha

Dalili zinaweza huonekana mpaka wiki ya 10 baada ya kugusana na bakteria. Kwa ulinzi wa afya yako ni vema kumuona daktari wako mda wowote ukiwa na homa na kusikia baridi kipindi cha ujauzito.

Mara chache maambukizi haya  huenea kwenye damu yako au mfumo wa fahamu na kuwa makali zaidi. Katika hali hii homa, maumivu ya misuli na kusikia baridi inaweza kuwa mbaya sana na kusababisha maumivu ya kichwa, shingo kukaza, kuchanganyikiwa, na kutetemeka sana. Hata hivyo, mwanamke mjamzito mmoja kati ya watatu haonyeshi dalili zozote. Inawezekana kujua umeambukizwa mara baada ya kupata shida wakati wakujifungua au mtoto anapoumwa baada ya kuzaliwa.

Jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa Listeria?

Njia nzuri ni kuepuka vyakula vyote vinavyoweza kusababisha listeria. Ulaji wa vyakula vilivyoambukizwa na listeria ni chanzo kikuu cha maambukizi.

Katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito kinga ya mwili inakua chini, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa ugonjwa huu, ni vema kula vizuri na kuangalia aina ya vyakula unavyokula ili usipate maambukizi mpaka mwisho wa ujauzito.

Ukiwa na ujauzito unashauriwa kuepuka vyakula vilivyo na hatari ya kubeba bakteria listeria,ambavyo ni kama:

 • Bidhaa za maziwa ya kupakiwa ambazo hazijapitishwa kwenye joto ili kuua vidudu hatari(zina lebo ya-unpasteurised kwenye chupa zake)
 • Jibini laini
 • Nyama mbichi za kupakiwa

Ni salama kutumia bidhaa za maziwa zilizopitishwa kwenye joto ili kuua vijidudu hatari kama mgando (yoghurts) na jibini ngumu. Pia,kuwa makini zaidi ukiwa nyumbani wakati wa kuandaa chakula:

 • Osha mikono yako kabla na baada ya kuandaa chakula.
 • Osha vyombo vyako na sehemu ya kukatia nyama wakati wote wa kuandaa chakula.
 • Tenganisha nyama iliotayari kwa kuliwa na mbichi ndani ya friji, yaani nyama mbichi iwe chini ya nyama iliyo tayari kuliwa ili damu na maji kutoka kwenye nyama mbichi yasiharibu nyama iliyo tayari kwa kuliwa.
 • Menya na osha matunda, mboga za majani na saladi vizuri kabla ya kula.
 • Pika chakula vizuri na kwa jotoridi linalofaa.

Bakteria listeria anaweza kuishi na kukua kwenye mazingira ya baridi kama ndani ya friji tofauti na bakteria wengine.

Bakteria wengi wa listeria wanaambatana na vyakula baridi na tayari kwa kuliwa ambavyo vimehifadhiwa kwa muda mrefu  au katika jotoridi lisilo sahihi.

Vyakula ambavyo ni salama kwa mama mjamzito:

 • Samaki wa kukaanga
 • Nyama zilizopikwa, kitimoto, na nyama za kutibiwa
 • Saladi zilizopakiwa, na matunda yaliyokatwa kama ndimu.

Kwa vyakula vilivyotayari kwa kuliwa, ni muhimu kufanya yafuatayo:

 • Angalia kama jotoridi la friji yako ni sawa kama ulivyoshauriwa, kawaida digrii 5 za sentigredi au chini
 • Kula vyakula kabla ya tarehe zake za mwisho za matumizi.
 • Fuata maelekezo yaliyo kwenye vipakio vya vyakula, kama vile ni siku ngapi uendelee kutumia baada ya kufungua bidhaa mfano mzuri ni maziwa fresh ya kampuni kama Azam.

Unaweza kupata listeria kutoka kwa wanyama kama kondoo, ng’ombe, mbuzi wakati wamejifungua. Kama unafanya kazi za shambani au unatembelea shamba kaa mbali na kondoo,ng’ombe na mbuzi na epuka kushika nguo na vifaa vinavyotumika kuwahudumia wanyama.

Jinsi gani ugonjwa wa listeria unatibika?

Kama una dalili zozote za mafua au umekula kitu ambacho unahisi kimekuletea dalili za mafua ongea haraka na mshauri wako wa afya.

Ikiwa mshauri wako wa afya atagundua una maambukizi ya listeria atapanga upate kipimo cha damu. Na kama majibu yataonyesha umeambukizwa, daktari atahakikisha unapata antibaiotiki kukulinda wewe na mtoto. Pia utafanyiwa uchunguzi wa “ultrasound” kuangalia kama afya ya mtoto ni salama.