Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ugumba kwa Mwanamke

Ugumba ni tatizo linaloathiri takribani mmoja kati ya wanandoa 6. Utambuzi wa ugumba unakamilika pale wanandoa wanapojaribu kupata mtoto kwa  mwaka mzima bila mafanikio.

Ni nini chanzo cha ugumba kwa mwanamke?

Sababu kuu ya ugumba inahusisha matatizo ya yai kupevushwa, kuharibika mirija ya falopiani au mfuko wa uzazi(uteras), au matatizo ya mlango wa uzazi(cervix). Umri unaweza changia pia, kadiri mwanamke anavyokua kiumri ndivyo uwezo wake wa kupata ujauzito unapungua.

Tatizo la kupevuka yai linasababishwa na mambo yafuatayo:

 • Mabadiliko ya homoni
 • Uvimbe au jipu kwenye mfuko wa mayai
 • Matatizo katika mfumo wa ulaji, mfano anorexia nervosa (albamu) au bulimia nervosa.
 • Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya
 • Matatizo ya tezi ya thairoidi.
 • Uzito uliopitiliza
 • Msongo wa mawazo
 • Mazoezi makali ya mwili yenye kusababisha upungufu wa mafuta mwilini uliopitiliza.
 • Mzunguko mfupi wa hedhi.

Matatizo ya uharibifu wa mirija ya falopiani au mfuko wa uzazi (uterasi) unaweza kusababishwa na yafuatayo:

 • Uvimbe kwenye nyonga.
 • Maambukizi ya nyonga yaliyopita.
 • Ugonjwa wa “endometriosis” au uvimbe katika mfuko wa uzazi.
 • Uvimbe wenye maji ndani ya mfuko wa uzazi unaosababishwa na “endometriosis”.
 • Kovu kwenye mfuko wa uzazi au “adhesion” ( kushikana kwa tishu wakati wa kushonwa  kidonda baada ya upasuaji).
 • Ugonjwa wa kudumu.
 • Tatizo lililopita la mimba kutungwa nje ya mji wa mimba.
 • Kasoro ya kuzaliwa
 • DES syndrome (dawa, iliyotolewa kwa wanawake ili kuzuia kupoteza mimba au mtoto kuzaliwa mapema kabla ya wiki ya 37 inaweza kusababisha matatizo ya uzazi.)

Uteute  usio wa kawaida kwenye mlango wa kizazi unaweza pia kusababisha ugumba. Uteute usio wa kawaida ndani ya mlango wa kizazi unaweza kuzuia mbegu za kiume kufika kwenye yai au kufanya ugumu wa mbegu za kiume kupenya na kuingia kwenye yai.

Ugumba kwa mwanamke unatambulikaje?

Ugumba kwa mwanamke hupimwa kama sehemu ya uchunguzi wa mwili.Vipimo vinahusisha uelewa wa matibabu ya zamani na mambo yanayoweza kuchangia ugumba.

Vituo vya afya vinaweza kutumia vipimo vifuatavyo kutathimini uwezo wa kupata ujauzito:

 • Kipimo cha mkojo au damu kuangalia kama kuna maambukizi au tatizo la homoni ikiwemo ufanya kazi wa homoni ya thairoidi
 • Kipimo cha nyonga kuangalia kama unaweza kubeba ujauzito vizuri na kipimo cha titi kuangalia uwezo wa kuzalisha maziwa ukujifungua mtoto.
 • Sampuli ya uteute unaopatikana katika mlango wa kizazi na tishu kuangalia kama yai linapevushwa ndani ya mwili wako.
 • Kipimo maalumu (laparoscope) cha kuingizwa ndani ya uke wa mwanamke kuangalia hali ya ogani ndani ya mwili wa mwanamke na kuangalia kama kumeziba au kuna  kovu katika tishu za mfuko wa uzazi.
 • Kipimo maalum cha X-ray (HSG) kinachoshirikiana na kimiminika cha rangi kinachowekwa kwenye mirija ya falopiani kurahisisha wataalamu kuangalia kama kumeziba.
 • Kipimo (hysteroscopy) cha kuangalia kama kuna hali isiyo ya kawaida kwenye mfuko wa mimba, kwa kutumia kamera ndogo inayotoa mwanga.
 • Kipimo cha ultrasound kinachoangalia mfuko wa uzazi na mfuko wa mayai.
 •  Kipimo cha (Sonohystogram) kinachoambatana na kipimo cha ultrasound na majimaji ya chumvi yanayoingizwa kwenye mfuko wa uzazi kuangalia tatizo au hali isiyo ya kawaida.

Uelewa wako wa ufuatiliaji wa mzunguko wako wa hedhi na kupevuka kwa yai utamsaidia mtoa huduma kutathimini uwezo wako wa kupata ujauzito.

Jinsi gani ugumba unatibika?

Ugumba kwa mwanamke unatibiwa kwa njia zifuatazo:

 • Matumizi ya vidonge vya homoni ili kurekebisha mabadiliko ya homoni, “endometriosis” au mzunguko mfupi wa hedhi.
 • Matumizi ya dawa za kuchangamsha upevushwaji wa yai
 • Matumizi ya virutubisho vya kuongeza uwezo wa kupata ujauzito (vya kununua).
 • Matumizi ya antibaiotiki za kuondoa maambukizi ya magonjwa ya ngono.
 • Upasuaji mdogo kutoa aina yoyote ya makovu ya tishu ndani ya mfuko wa uzazi na uzibaji kwenye mirija ya falopiani,uterasi au eneo la nyonga.

Je,kuna kinga ya ugumba ?

Hakuna lolote linaloweza kufanyika kukinga ugumba uliosababishwa na matatizo ya kurithi au ugonjwa. Ingawa, kuna mambo mwanamke anaweza kufanya kupunguza uwezekano wa kuwa mgumba:

 • Chukua hatua kujikinga na magonjwa ya kuambukiza ya ngono.
 • Epuka dawa za kulevya
 • Epuka matumizi makubwa ya pombe kila mara.
 • Fuatilia ratiba nzuri ya usafi na afya.
 • Fanya vipimo na daktari wako wa mambo ya uzazi kama uko tayari kuanza kujamiana.

Lini niwasiliane na mtoa huduma wangu?

Ni muhimu kuwasiliana na mtoa huduma wako kama utakumbana na yafuatayo:

 • Hali ya kutokwa damu isiyo ya  kwa kawaida
 • Maumivu ya tumbo la uzazi.
 • Homa
 • Kutokwa  uchafu ukeni usio wa kawaida
 • Maumivu wakati wa kujamiana.
 • Kuvimba au kuwasha maeneo ya ukeni.